Mambo 4 Yatakufanya Uwe Na Subira

Mambo 4 Yatakufanya Uwe Na Subira

Travis Walker

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2017
Posts
323
Reaction score
334
Habari kwenu wana wa JF.
Leo nimechukua nafasi ya kuandika makala hii ili ikusaidie katika suala la kuondoa haraka ili uwe na uwezo mkubwa wa kuvumilia.Haraka ni kitu kibaya sana.Mtu ambaye ana haraka mara nyingi anakuwa ni mjinga mbele ya jamii anaweza kuchukua maamuzi yaliokuwa sio sahihi halafu ikapelekea kujuta.Pia haraka inasababisha kufeli kwa mambo mengi sana na hukatisha tamaa mapema.Hata hivyo haraka husababisha kuharibika kwa mahusiano na kuto-elewana.
Tafiti za wanasayansi zinaonesha kuwa subira hufanikisha mambo katika maisha.Ila kujiongoza na kuidhibiti haraka hali hiyo inakuwa ngumu kwa kila mtu.Lakini haya mambo 4 ukiyafanya utajifunza kusubiri na hatimaye utakuwa unafanya mambo yako kwa uwerevu pasi na kukurupuka.

1.KUJIFUNDISHA KUSUBIRI.
Unapotaka kufanya kitu chochote jaribu kukichelewesha halafu pambana na hisia zinazokutia haraka kwa kutolifanya jambo hilo kwa muda huo.Njia hii itakufanya ujifunze kuvumilia.Ingawa ni ngumu kwa mara ya mwanzo ila kadri unavyofanya utaweza.

2.JARIBU KUJISEMEA NAFSINI.
Unapokuwa na haraka sana jisemee moyoni kwa kujipa nasaha ya kusubiri.Inasadikika kujisemea moyoni kunashawishi ubongo kubadilisha hisia kwa haraka.

3.JARIBU KUVUTA PUMZI HALAFU USITE

Unapohisi una haraka mno.Jaribu kuvuta pumzi halafu sita kwa sekunde 10 baadae ndipo ushushe pumzi tarartibu.Zoezi hili linafaa sana.

4.JARIBU KUPATA MUDA MZURI WA KULALA.
Kulala ni kupumua kwa ubongo.Hivyo kulala masaa machache kunapelekea kudhoofika kwa ubongo.Hivyo utakuwa na uwezo mdogo wa kujiongoza.hivyo unashauriwa kuapa alau masaa manane ya kulala .

KWA USHAURI, MAONI WHATSAPP NO.
0778867423
 
Wakuu nimerekebisha
Shukrani...
Ila hapa kwenye subira nadhani inategemea na jambo lenyewe.Maana kuna mambo mengine ukivuta subira ndo unazidi kupotea bora ungefanya haraka haraka

Kingine vipi kwa wale ambao wakipanga jambo wanataka lifanyike hapo hapo,yaani haijalishi ni la muhimu au sio la muhimu..hivi hao wana matatizo ya kutokuwa na subira ama ndio nature yao ilivyo?
 
SWALI ZURI
 
MKUU UNA MADINI YA KUTOSHA NIMEYAKUBALI...VIPI WEWE NI MWANA SAIKOLOJIA??
 
Shukrani...
Ila hapa kwenye subira nadhani inategemea na jambo lenyewe.Maana kuna mambo mengine ukivuta subira ndo unazidi kupotea bora ungefanya haraka haraka

Kingine vipi kwa wale ambao wakipanga jambo wanataka lifanyike hapo hapo,yaani haijalishi ni la muhimu au sio la muhimu..hivi hao wana matatizo ya kutokuwa na subira ama ndio nature yao ilivyo?
Ahsante Jolie kwa suali lako zuri.
Haraka ni hisia ambayo ipo kwa kila kiumbe humsaidia kujilinda kama self defense.Lakini pia kuna watu huwa na haraka kila pahala ambapo wakati mwengine hawastahili kuwa hivyo.Wanageuza hisia kuwa tabia.Hivyo ndio maana sayansi ikatupatia njia ambazo tuwe tunaweza kujiongoza na kujitambua wakati tukiwa na hisia kama hizo : haraka,hasira n.k.Ili zitumike wakati husika na pasipostahili tuwa tunajitambua na kuweza kujiongoza
 
Back
Top Bottom