msuyaeric
JF-Expert Member
- Dec 18, 2014
- 842
- 1,197
Je wajua serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imeanza utekelezaji wa Kongani ya viwanda(Industrial Park) ya Kwala? Awamu ya kwanza inatarajiwa kukamilika ifikapo 2024.
Ujenzi huu ukikamilika unatarajia kuwa na viwanda 200, kuzalisha ajira za moja kwa moja 100,000 na zisizo za moja kwa moja 300,000. Uwekezaji katika eneo hili unakadiriwa kugharimu Dola Bilioni 3.
Mambo mengine matano(5) muhimu yanayotarajiwa kufanywa ndani ya miezi 12 ijayo katika Kuchochea biashara na uwekezaji nchini;
1. Kuimarisha mifumo ya kushughulikia changamoto za uwekezaji na kutafuta fursa za masoko na kuwaunganisha na wajasiriamali wa ndani
2. Kuratibu masuala ya uwezeshaji wananchi kiuchumi na maendeleo ya sekta binafsi na kuratibu ufanikishaji wa uwekezaji ikiwemo kuongeza ufanisi wa miradi ya uwekezaji kupitia
3. Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Kuratibu uanzishaji na uendelezaji wa miradi mikubwa ya uwekezaji na kuboresha mazingira wezeshi ya kuendeleza viwanda na biashara.
4. kuimarisha na kuhamasisha uwekezaji wa Sekta Binafsi katika Maeneo Maalum ya Kiuchumi (SEZ) na Maeneo Maalum ya Uwekezaji kwa ajili ya uzalishaji wa bidhaa zitakazouzwa nje (EPZ).
5. kuimarisha taasisi za utafiti na kufanya tafiti kwa ajili ya maendeleo ya viwanda, kuhamasisha uwekezaji wa viwanda vinavyotumia malighafi zinazopatikana nchini.
Rais Samia anaendelea kuonyesha utofauti katika uongozi wake kwa kufanya yale ambayo watanzania tunayataka kwa wakati sahihi kabisa. Hongera sana Rais Samia kwa kazi kubwa unayoifanya kuijenga Tanzania yetu. Mwenyezi Mungu azidi kukubariki.