Mambo 5 mwanamke hapaswi kumwambia mume wako! Never!

Mambo 5 mwanamke hapaswi kumwambia mume wako! Never!

Jaji Mfawidhi

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2016
Posts
15,835
Reaction score
23,776
i.jpeg


MAMBO HAYA USIMWAMBIE MWANAUE WAKO, HATA KWA KISU SHINGONI:-
  1. Mwanaume aliyekutoa Bikra [aliyeku'bikiri], hapa hata kama wewe ni malaika utamu-umiza sana mwanaume, hatokaa asahau, ataumi sana, akikuuliza mpige chenga! Usimwambie kama uliwahi kufikishwa kileleni ama la, kuwa mjinga wa mapenzi kwake!
  2. Idadi ya wanaume ulio jamiiana nao kabla ya kuoana na mume wako: Hupaswi kumfahamisha mpenzi wako wa kiume au mume wako ni wanaume wangapi ulikutana nao kimwili kabla ya kuishi naye. Wanandoa CHANZO CHA PICHA,. Sababu ni kwamba unaweza kufikiri hautamkosea mume wako siku sijazo. Na kama idadi ya wanaume uliyomwambia ni wengi anaweza kufikiri wewe ni kahaba au mzinzi. Kwahiyo, iwapo atakuuliza ni wanaume wangapi ulishawahi kukutana nao kimwili, unaweza kucheka tu na umwambie: ''Ebu acha, tuanachane na hayo, lakini suala la ni wangapi halihusiani na safari ya mapenzi.
  3. Kusema siri za mpenzi wako wa kiume au mume wako wakati mmoja .Ukiulizwa maswali kumuhusu mwanaume, mjibu machache. Usiseme mambo ambayo yanaweza kumfanya mume au mpenzi wako ahisi kwamba sio bora, au ajihisi kuwa mtu mbaya. Usizungumzie kuhusu -ungependa kuwa na uhusiano na mwanaume tajiri kiasi fulani, mwenye uwezo wa kingono kiasi gani, na ni kwa vipi ungependa ampende mke wake.
  4. Usimwambie mume wako kwamba unampenda sana rafiki yako au shemeji yako. Sote tunafahamu kuwa inawezekana kwa rafiki au shemeji kutaka kukuoa. Lakini, ni hatari kumwambia mume wako kuhusu wazo hili . Sababu ni kwamba mume wako anaweza kuanza kuwa na mashaka kuhusu tabia zake na vitendo vyako kumuhusu mwanaume huyo, jambo linaloweza kusambaratisha ndoa yako.
  5. Usijaribu kumwambia kuwa unamchukia mama yake au familia yake. Hata mama mkwe awe ni mtu mbaya kiasi gani, usimwambie mume wako kuwa unamchukia. Au unaichukia familia yake. Hata kama umekasirika kiasi gani, usijaribu kusema mambo mabaya kuwahusu, au kumuona mume wako sawa na familia yake. Kama haupatani na yeyote katika familia ya mume wako, elezea kwa utulivu, ukiwa na matumaini kuwa ataelewa ni kwanini haupatani nao. Mume wako pia ataweza kukusaidia kutatua tatizo, na pia itazuwia matatizo mengine ambayo yanaweza kusababisha matatizo makubwa zaidi.
  6. Usimtishe mume wako kuwa utakuja kuachana naye . Siku utakapomwambia mume wako kuwa utaachana naye wakati mnazozana, jua ndio mwanzo wa malumbano ndani ya ndoa.
Ndoa itaanza kukumbwa na misukosuko, wasi wasi na kutoaminiana. Kutishia kutoa talaka katika ndoa inamaanisha kuwa hauna moyo wa imani katika ndoa, na hauoni umuhimu wake.
Isipokuwa kama katika ndoa kuna unyanyasaji au uhalifu mwingine mbaya, ni vyema kujaribu kushirikiana kutatua changamoto zozote mlizonazo.
bbc.
 
Wanawake gani hao unawaambia haya mambo? Wenzako wako mbele balaa wanasuguana wao kwa wao, hivi wewe bado uko local sana nini, mume ni nani wakati wazazi tu wanakemewa au hawasikilizwi ng’o, dawa ya mwanamke ajue kabisa mume wake akimzingua anapata adhabu au moto mkubwa utamwakia ikiwa pamoja na kurudishwa kwao haraka..!! Na mwanaume hata kama unampenda mkeo acha kucheka cheka hovyo, atakudharau, wakati mwingine cheka nae shortly, ila akikuangalia anajua kabisa hili jamaa nilizingua tu analianzisha moto mbaya sana… codes zako hazisomi kwake.. Ujue hapo maisha yatakuwepo..!!
 
Mama mmoja tuliwahi kufanya naye kazi ofisi moja, ilikuwa mara kwa mara anafunguka kuhusu habari za familia yake hadi za chumbani. Anafika asubuhi yuko na mnuno mmoja wa hatari....kwa madai ya kwamba eti jana yake usiku mumewe alimtaka akampa halafu asubuhi tena mumewe anataka tena lakini yeye kamnyima. Mtu anayeelezea hadi size ya uboor wa mumewe!!

Unamtazama unamtafakari kisha unamuacha na mipasho yake unaendelea na kazi zako.
 
Back
Top Bottom