Mambo 5 ya kufanya ukiwa umechoka kila kitu

Mambo 5 ya kufanya ukiwa umechoka kila kitu

Rakims

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2014
Posts
5,002
Reaction score
4,571
Habari wakuu,

Nini cha kufanya ukiwa umechoka na kila kitu?

Katika maisha kila mtu huexperience maisha kwa mtindo wake wapo ambao huona maisha ni mazuri wapo ambao huona maisha ni kawaida na wapo ambao huona maisha ni machungu'-

Makundi yote matatu ya watu hawa basi hufikia sehemu mwili hukosa amani kila kona na kupelekea akili kukosa ufanisi mzuri huenda ikawa ni siku nzima ama wiki nzima au mwezi mzima hadi pale linapotokea jambo la kushtua akili yake na kuanza kuishughulisha.

Kufupisha maelezo kulingana na uchovu ulionao muda huu hata wa kusoma thread hii basi nikujuze ni mambo gani matano ya kufanya ukiwa umechoka kila kitu.

1: KWENDA MIAYO (Yawning)
Hii njia husaidia mtu ambaye kachoka akili na pia anakosa hata nafasi ya kuipa fikra mpya akili yake basi Ikiwa unajihisi umechoka kila kitu na hata akili haifanyi kazi vizuri na hata usingizi hauji pia basi nenda miayo ambayo sio ya asili mara 3 na moja kwa moja utaanza kuona miayo inakuja yenyewe kwa mfululizo mara nyingi.
Miayo husaidia ufunguzi wa akili na mawazo mapya na kupoteza ama kuanzisha jipya tofauti na lile uliyokuwa ukifikiria ukipiga Mingi zaidi basi moja kwa moja hata kama huna usingizi macho yataleta kishawishi kikubwa cha kulala.

2: KUFUTA PAJI LA USO
Hii njia husaidia mtu ambaye anakuwa kachoka mwili na kuanza kupata maumivu ya kichwa kama kipanda uso basi kwa hakika yoyote mwenye kusugua mafundo ya viganja vyake na kupata umoto kisha akabandika kwenye macho yake huku kafumba na kupandisha kwenye paji lake la uso akifanya hivyo mara saba moja kwa moja kipanda uso kitaisha vile vile kwa mtu mwenye kisirani.

3: KUVUTA PUMZI
Ikiwa mtu atakuwa kachoka kiroho yaani mtu mwenye kuchoka hadi kufikia hatua ya kuona suluhu ni kujiua basi ni vema zaidi akavuta pumzi ndefu puani kwa sauti na kisha akatoa kwa sauti mdomoni mara saba moja kwa moja hata waza tena kujiua na ataanza kuogopa kujitoa nafsi yake mwenyewe na ataepukana na kukata tamaa.

4: KUONGEA NA ROHO:
Kila kiumbe hai kina roho hivyo ikiwa uchovu wako umesababishwa na jambo moja tu lenye kujirudia kila mara basi ni vevma zaidi ukaongea na Roho (Mungu/Malaika/Jini/Shetani/roho yako mwenyewe) nimejaza roho hizo kwa maana kila mtu ana imani yake hivyo ukiwa uchovu wako unasababishwa na mikwamo ya kila kitu basi fumba macho na ongea na kichwa chako mithili kwa wenye imani ya Mungu unaweza kusema.
"Hakika hakuna anayejua yaliyopo rohoni na moyoni kwangu Isipokuwa wewe uliyenipa roho na kuniumba wewe unajua nini mimi nataka na nini mimi sitaki, unajua hasa ni ipi dhamira yangu ikiwa ni nzuri unajua mwanzo na mwisho wake na ikiwa mbaya unajua mwanzo na mwisho wake na hakika hili umenijalia wewe na utanisaidia wewe" Kisha sikiliza majibu.

5: KUJICHEKA AU KUCHEKA:
Ikiwa uchovu wako umetokana na hasira au kisirani au jeuri na kiburi basi kaa pembeni faragha peke yako kisha anza kujicheka au cheka na hakikisha kicheko chako kinakuwa straight yaani kisiwe cha uongo kama vile mambo yakikupiga na ukakosa raha na ukaanza kulia basi kaa vile vile na ujicheke mwenyewe kwa maana mkwamo mkubwa wa maisha na uchovu huletwa na kukosa furaha na furaha humuweka mtu karibu na malaika na huzuni humuweka mtu karibu na shetani. Hivyo ni vyema kucheka peke yako kama vile unavyolia peke yako hii itamfanya shetani wako akuone wewe ni mwehu na akukimbie kwa maana mitihani anayokuletea mategemeo yake uadhirike na uchukie hukumu za Mungu wako sasa anaona unafurahia matatizo muda huo yeye ndio atanuna. hii ni msaada pia kwa watu wenye msongo wa mawazo.

Chanzo:
Vitabu elfu vya maarifa

Rakims
 
unadhani skuizi naongea na roho ndani kwa ndani kama Druid..
naongea kwa sauti kabisa maana naona kama nikoongea ndani hainiskii msisitizo wangu.

nmeanza kuwaelewa wanaoongea pekeyao njiani
Yes, japo asilimia kubwa ya wenye kuongea peke yao njiani ni wenye msongo wa mawazo.

Rakims
 
Katika yote hayo bado unakuta mtu kasongwa na machungu. Nashauri mtu yeyote mwenye msongo wa mawazo (stress) au mfadhaiko/upweke (depression), aanze kufikiria au kufanya lolote lililo jema, lolote lenye sifa njema, lolote lenye staha, lolote lenye heshima au kitu chochote chenye kupendeza au kufurahisha.

Mathalani, sikiliza nyimbo au muziki mzuri, fanya usafi, fanya mazoezi ya mwili, angalia picha au filamu unazopenda, tembelea mandhari nzuri kama vile mito, misitu, milima, fukwe au angalia ndege na wanyama wakupendezao.

Zaidi sana, mshukuru Mungu kwa kukupa uhai na uzima ulionao, na ndio maana bado unapumua na kutembea wakati wengine wamelazwa hospitalini au wameishakufa. Sema ahsante Mungu kwa kuniongezea siku ya kuishi leo, naomba kusudi lako la kunileta duniani litimie.

Baada ya hapo, tubu kwa Mungu makosa yako na tubu kwa uliowakosea kama wapo karibu au unaoweza kuwasiliana nao. Aidha, malizia kwa kuwasamehe wote waliokukosea.

Kisha, kwa kumaanisha sema hivi: "Yesu Kristo karibu moyoni mwangu uniokoe niwe mwana wa Mungu Baba kwa kuzaliwa upya rohoni na kuongozwa na Roho Mtakatifu." Amani utakayoipata moyoni/ rohoni ni ya pekee sana!

Umeeleza vema, lakini bado unakuta mtu kasongwa na machungu moyoni na akilini mwake.

Nashauri mtu yeyote aliye katika hali hiyo ya msongo wa mawazo (stress) au mfadhaiko/upweke (depression), aanze kufanya au kufikiria lolote lililo zuri, lolote lililo safi, lolote lenye haki, lolote lenye staha, lolote lenye sifa njema, lolote lenye ukweli, lolote lenye kupendeza na lolote lenye heshima.

Inaweza kuwa ni kufanya usafi, kusikiliza nyimbo au muziki aupendao, kufanya mazoezi au kutembelea mandhari nzuri kama milima, misitu au fukwe. Aidha, atazame picha, michezo au filamu anazopenda, au aangalie ndege na wanyama wampendezao. Ila yote hayo yanatuliza tu machungu kwa muda mfupi sana.

Kwa suluhisho la kudumu, anza kumshukuru Mungu kwa kukupa uhai na uzima ulionao sasa, ambapo unapumua vizuri wakati wengine wamelazwa hospitalini au wameishakufa. Mungu kakuongezea siku ya leo ili utimize kusudi lake alilokuleta duniani, ikiwemo kumwabudu Yeye pekee katika roho na kweli.

Baada ya hapo, tubu kwa Mungu makosa yako na tubu kwa uliowakosea kama wapo karibu au unaoweza kuwasiliana nao. Aidha, malizia kwa kuwasamehe wote waliokukosea.

Kisha, kwa kumaanisha moyoni mwako sema hivi: "Yesu Kristo karibu moyoni mwangu uniokoe niwe mwana wa Mungu kwa kuzaliwa upya rohoni na kuongozwa na Roho Mtakatifu." Amani utakayoipata moyoni mwako ni ya pekee sana!
ASante kwa kuchangia japokuwa wewe bado upo juu juu sana mimi nimeingia ndani zaidi kwa mtu ambaye hata kufukiria tu kwake teyari imekuwa tabu na mwisho elewa kwamba hii nimeweka kwa watu wote wenye imani na wasiokuwa na imani sasa wewe ukiwa selective na watu kundi fulani fulani basi bado utakuta watu unawachosha katika kufikiria kabla ya kufika hayo uliyotaja wewe mtu anatakiwa kwanza aamshe ubongo wake kwa maana ndio chanzo kizuri cha utambuzi na hapo hayo yote yanaletwa na uchovu wa akili.

Energy yako nyingi usiweke watu katika kuamini jina tu bila kujua kiumbe husika. hapo ni sawa na kumuamsha mlevi kutoka usingizini kafumbua tu macho unamwambia unamjua yesu.
Si ajabu akakujibu yeye ni mgeni mtaa huo labda uulize wenyeji.
Yote kwa yote umejitahidi kwa uelewa wako finyu wa makala hii kuchangia.

Rakims
 
Nimeanza na suluhisho la muda mfupi kama la kwako japo halifanani kabisa. Kisha nikamalizia na suluhisho la kudumu kwa mtu yeyote yule, si wa Imani fulani.

Soma upya bandiko langu pengine utajua kama uelewa wangu ni finyu au mpana! Na nitaheshimu mtazamo wako wowote ule - iwe wa kukubali au kukataa.
Pumzika mkuu huenda unapirika za akili maana hata nilichoandika bado hujaelewa
 
Basi hongera sana kwa kuelewa ulichoandika mwenyewe kuhusu kuchoka. Mimi nimeandika kuhusu machungu na kukata tamaa ya maisha au kuchoka maisha. Nakuachia na kuuheshimu uelewa wako, nabaki na uelewa wangu wa kuyachoka maisha au kukata tamaa.
Hongera pia maana kwa sasa ndio naona umeanza kuelewa maana
 
5: KUJICHEKA AU KUCHEKA:
Ikiwa uchovu wako umetokana na hasira au kisirani au jeuri na kiburi basi kaa pembeni faragha peke yako kisha anza kujicheka au cheka na hakikisha kicheko chako kinakuwa straight yaani kisiwe cha uongo kama vile mambo yakikupiga na ukakosa raha na ukaanza kulia basi kaa vile vile na ujicheke mwenyewe kwa maana mkwamo mkubwa wa maisha na uchovu huletwa na kukosa furaha na furaha humuweka mtu karibu na malaika na huzuni humuweka mtu karibu na shetani. Hivyo ni vyema kucheka peke yako kama vile unavyolia peke yako hii itamfanya shetani wako akuone wewe ni mwehu na akukimbie kwa maana mitihani anayokuletea mategemeo yake uadhirike na uchukie hukumu za Mungu wako sasa anaona unafurahia matatizo muda huo yeye ndio atanuna. hii ni msaada pia kwa watu wenye msongo wa mawazo.
Kuna nguvu katika kucheka, naamini na ni nguvu ya asili.
 
ASante kwa kuchangia japokuwa wewe bado upo juu juu sana mimi nimeingia ndani zaidi kwa mtu ambaye hata kufukiria tu kwake teyari imekuwa tabu na mwisho elewa kwamba hii nimeweka kwa watu wote wenye imani na wasiokuwa na imani sasa wewe ukiwa selective na watu kundi fulani fulani basi bado utakuta watu unawachosha katika kufikiria kabla ya kufika hayo uliyotaja wewe mtu anatakiwa kwanza aamshe ubongo wake kwa maana ndio chanzo kizuri cha utambuzi na hapo hayo yote yanaletwa na uchovu wa akili.

Energy yako nyingi usiweke watu katika kuamini jina tu bila kujua kiumbe husika. hapo ni sawa na kumuamsha mlevi kutoka usingizini kafumbua tu macho unamwambia unamjua yesu.
Si ajabu akakujibu yeye ni mgeni mtaa huo labda uulize wenyeji.
Yote kwa yote umejitahidi kwa uelewa wako finyu wa makala hii kuchangia.

Rakims
Jamaa ameingia kidini zaidi wakati hii ni free mind,.
at all nimekuelewa rakims.

ukitaka kujua ukweli wa mambo mengi usiegemee dini yeyote.
 
Jamaa ameingia kidini zaidi wakati hii ni free mind,.
at all nimekuelewa rakims.

ukitaka kujua ukweli wa mambo mengi usiegemee dini yeyote.
Asante mkuu, Tupo pamoja
 
Back
Top Bottom