SoC01 Mambo 5 ya kuzingatia kabla hujawekeza mafao yako ya ustaafu popote

SoC01 Mambo 5 ya kuzingatia kabla hujawekeza mafao yako ya ustaafu popote

Stories of Change - 2021 Competition

Dr. Zaganza

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2014
Posts
1,414
Reaction score
2,181
retire.PNG



Ni wazi ofisi na mtaani ni mazingira mawili tofauti kabisa,hivyo yanahitaji mbinu tofauti kupata kipato cha kuendesha maisha yako.


Kwa kuwa wastaafu wengi wametumia muda mwingi kazini ( hadi unafika miaka 55 au 60), muda huu unapostaafu unapaswa kujifunza mazingira mapya kwa uharaka bila kujali kujifunza huko itakuwa rahisi au gharama.

Moja ya njia ya kujifunza haraka jambo jipya ni kuangalia walotangulia kisha kufanya marekebisho kidogo (Reverse Engineering).

Hapa Chini Nimeandaa dondoo 5 za kuongoza kujifunza kwako , Zipite mwenyewe.

1. Usimkabidhi mtu umiliki wa 100% wa mradi utakaowekeza

Kama umenunua gari la abiria na kumpa kijana wa mtaani kwako, hapa unakuwa hujui huenda malengo yake ni kupata mtaji afungue saloon na si kuendeleza gari lako hatimaye lizalishe gari lingine. Namjua mstaafu mmoja anaishi Kibaha, amerudi nyuma kimaendeleo na hata kupata stroke kwa kutozingatia hili.

2. Jishughulishe na Mradi uliowekeza Kila siku au mara moja kwa wiki

Je, wewe ni sehemu ya mradi? Kuna sehemu ya majukumu umejipatia ndani ya mradi? Hapa kuna faida mbili. Moja unashughulisha mwili ili usikae bure na kukaribisha maradhi. Pili, unapata fursa ya kushauri na kufuatilia mradi husika. Nilipoanzisha mradi wa ngozi asilia, kila mwaka anapojiunga muwekezaji mstaafu, tunampa uwakala wa eneo aliko kudeliver kwa wateja yeye mwenyewe akipenda au kijana wake.

3. Tofautisha Wazo la Biashara na Biashara

Unapoona group la whatsapp mahesabu ya kilimo cha matikiti yanavyolipa, utawehuka!! Ukipata story za kilimo cha miti ya mitiki (Teak) huko Iringa kinavyotajirisha waliolima, Utatamani uwekeze kabla jua kuzama!! Tambua hayo ni mawazo tu. Biashara ni ile ulofanya tafiti na kujiridhisha, kisha ukaanza kidogo kidogo.Kwa sisi tuna njia mbili, muwekezaji anaweza kuja na idea,tukaifnyia marketing research kuona italeta faida? (ROI) au anaweza akatumia biashara ambazo tayari zimeanza kuingiza kipato.

4. Usiweke Mayai Yote Kapu Moja

Biashara ina pande mbili,faida na hasara. Hivyo anza na kiasi kidogo mfano robo ya mtaji ulokusudia ili kupima ukuaji wa biashara. Kisha ongeza robo nyingine miezi michache mbele. Ukiridhishwa na maendeleo ongeza tena iwe robo tatu kabla mwaka kuisha Kisha utamalizia mtaji kamili bada ya mwaka wa kutathmini.Hapa tunaanzaga na ofisi ya nyumbani,mpaka biashara ioneshe uelekeo ndipo tunakodisha ofisi rasmi.

5. Fedha Zako Wekeza Kwenye Mshirika sahihi na Usimamizi Bora

Kwa kuwa ulikuwa kazini muda mwingi, ni wakati wa kuanza mradi na mshirika (business partner) mwenye sifa kuu mbili. Moja uaminifu na mbili uweledi (proffesionalism) kwenye eneo hili. Endapo partner atakuwa na sifa ya uweledi bila uaminifu, atatumia uweledi wake kukumaliza.

Dr.Mussa Zaganza ni msimamizi bobezi wa miradi ya kati na mikubwa,
 
Upvote 1
Back
Top Bottom