Mambo 7 Muhimu Pre Season ya Simba Nchini Sudani

demigod

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2015
Posts
8,292
Reaction score
15,250
1. Nasorro Kapama ni mzuri katika ile nafasi aliyocheza leo ukilinganisha na Onyango. Kapama ni mtulivu zaidi ili hali Onyango hana composure.

2. Dejani apewe muda zaidi. Ni vyema tukampa muda Mzungu Dejani kwani ni hazina kwa Simba. Mikimbio yake bado ni mizuri tatizo ni kwamba wenzake bado hawajaweza kuisoma mikimbio yake.

3. Asilimia kubwa ya wachezaji wa Simba ni wafupi hivyo watapata shida sana kucheza mipira ya juu. Viungo wengi wa Simba ni wafupi kiasi kwamba wanashindwa kumuona alipo Dejani wakati wa shambulizi hata kupelekea mzungu kukosa mipira ya kufunga.

4. Tactical changes za zoran ni za kitaalamu sana hasa paale alipo amua kucheza na maforward 2 na kuamua kuua kiungo kimoja. Ninachoweza kusema ni kwamba huyu jamaa (Zoran) anaujua sana mpira. Atawasaidia sana simba mechi za kimataifa.

5. Sakho ni kama pilipili hoho. Yaani haiwashi wala nini. Nashauri dirisha dogo mumchukue Denis Nkane kwa mkopo kutoka Yanga huenda akawavusha katika kipindi kigumu ambacho simba watakuwa wakipitia. Sakho anaweza kupelekwa kwa mkopo Singida Big Stars ili akakuze kiwango chake.

6. Chama tangu apewe kitambaa cha Ukaptein amekengeuka. Sijui ni ushamba au ni nini haswa kinachomsibu. Amekuwa akifanya faulo za kijinga (unsportmanship fouls) mara nyingi. Alimkanyaga mkono chezaji wa kotoko leo anamkanyaga kiatu mchezaji wa al hilal. Kocha amuonye mapema.

7. Simba inapaswa kuachana na Manzoki kwa kuwa sio tiba ya tatizo la ushambuliaji. Manzoki atakuja kiwapotezea muda kama wenzenu Yanga walivyo potezewa muda na Sarpong. Watafute striker mkali wa kiafrika ambaye atakiwa back up kwa Mzungu dejani.

-mwisho-
 
Nilikua nimelala ila nilivyoona ni ww na umetoa vitu positive hivi nikasema hapana lazima nimsabahi mtani umekua mtu sana mtani. Yani kumbe sasa umekua mchambuzi wa soka umewiva. Ila kuhusu Sakho tuachie tuu najua mnamwogopa.
 
Uchambuzi wa hovyo kabisa. Mechi ya leo kocha katufungisha. Ana wachezaji wazuri lakini hajui jinsi ya kuwatumia. Dejan sio mchezaji wa kuanza.
 
ungeondoa unazi kwenye andiko lako ningekulewa vema,ila sio mbaya umejitahidi kuficha kiasi chake.
 
Hivi mkuu mtunza Kinyesi, 'Pre season' maana yake nini?

Au umeandika tayari ukiwa na Kinyesi?
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]ety simba waachan na manzoki kwa ww unaishi dunia ipi manzoki ashasajiliw china huko

- pil chama kafany foul leo sbb wale jamaa walicheza foul za htr had makocha wakamind, nakuongezea chama hajavaa kitambaa cha ucaptain leo kavaa had timu ya taif yule
 
Natafuta tusi kuubwa nikutukane maana wewe ni chawa wa Barbara.

Simba inaendeshwa kwa propaganda kama hizi.
Unawezaje kusema upumbavu kama huo na mashabiki tumeona mechi wote?

Hukuona faulo mbaya zilizochezwa isipokuwa za chama?
Unawezaje kumu under rate Sakho?
Unawezaje kuwaambia Simba wamvumilie mzungu eti ana mikimbio?Huu si ni uchizi kabisa?

Asee uongozi wa Simba umezingua sana hatuma mwalimu wa timu.Ni utopolo mtupu
 
Simba vipasi vingi tena mara nyingi vya kurudi nyuma visivyo na madhara kwa mpunzani. Kuna wakati Simba inacheza utazani kashashinda goli nyingi kumbe ashafungwa, yaan slow slow
 
Hii sio pre season, utopolo acheni ushamba. Hii tournament ipo wakati season imeshaanza kwa hiyo haiwezi ikaitwa hivyo, ila ni kuutumia muda huo kwa maandalizi ya mechi za kirafiki za kimataifa wakati baadhi ya timu za taifa zikicheza kuwania CHAN qualifications
 
Uchambuzi wa hovyo kabisa. Mechi ya leo kocha katufungisha. Ana wachezaji wazuri lakini hajui jinsi ya kuwatumia. Dejan sio mchezaji wa kuanza.
Aanze nani sasa. Au Andunje PHIRI?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…