demigod
JF-Expert Member
- Jan 2, 2015
- 8,292
- 15,250
1. Nasorro Kapama ni mzuri katika ile nafasi aliyocheza leo ukilinganisha na Onyango. Kapama ni mtulivu zaidi ili hali Onyango hana composure.
2. Dejani apewe muda zaidi. Ni vyema tukampa muda Mzungu Dejani kwani ni hazina kwa Simba. Mikimbio yake bado ni mizuri tatizo ni kwamba wenzake bado hawajaweza kuisoma mikimbio yake.
3. Asilimia kubwa ya wachezaji wa Simba ni wafupi hivyo watapata shida sana kucheza mipira ya juu. Viungo wengi wa Simba ni wafupi kiasi kwamba wanashindwa kumuona alipo Dejani wakati wa shambulizi hata kupelekea mzungu kukosa mipira ya kufunga.
4. Tactical changes za zoran ni za kitaalamu sana hasa paale alipo amua kucheza na maforward 2 na kuamua kuua kiungo kimoja. Ninachoweza kusema ni kwamba huyu jamaa (Zoran) anaujua sana mpira. Atawasaidia sana simba mechi za kimataifa.
5. Sakho ni kama pilipili hoho. Yaani haiwashi wala nini. Nashauri dirisha dogo mumchukue Denis Nkane kwa mkopo kutoka Yanga huenda akawavusha katika kipindi kigumu ambacho simba watakuwa wakipitia. Sakho anaweza kupelekwa kwa mkopo Singida Big Stars ili akakuze kiwango chake.
6. Chama tangu apewe kitambaa cha Ukaptein amekengeuka. Sijui ni ushamba au ni nini haswa kinachomsibu. Amekuwa akifanya faulo za kijinga (unsportmanship fouls) mara nyingi. Alimkanyaga mkono chezaji wa kotoko leo anamkanyaga kiatu mchezaji wa al hilal. Kocha amuonye mapema.
7. Simba inapaswa kuachana na Manzoki kwa kuwa sio tiba ya tatizo la ushambuliaji. Manzoki atakuja kiwapotezea muda kama wenzenu Yanga walivyo potezewa muda na Sarpong. Watafute striker mkali wa kiafrika ambaye atakiwa back up kwa Mzungu dejani.
-mwisho-