N'yadikwa
JF-Expert Member
- Aug 10, 2014
- 7,427
- 10,905
Kama unayajua piga kimya.
Kama huyajui haya hapa:-
Mambo 7 muhimu kuhusu Aircraft Carrier ya Marekani:
Kama huyajui haya hapa:-
Mambo 7 muhimu kuhusu Aircraft Carrier ya Marekani:
- Idadi ya Waajiriwa – Kila aircraft carrier ya Marekani ina wastani wa 5,000 – 6,000 waajiriwa, wakiwemo marubani, wahandisi, wahudumu wa meli, wataalamu wa silaha na wahudumu wa matibabu.
- Ukubwa na Uzito – USS Gerald R. Ford, carrier mpya zaidi, ina urefu wa takribani 337m (1,106 feet) na uzito wa zaidi ya 100,000 tons ikiwa imejaa.
- Supermarket na Huduma za Kijamii – Aircraft carriers zina maduka ya chakula na mahitaji ya msingi yaani supermarket, migahawa, hospitali ndogo, sehemu za burudani na hata barbershops kwa wahudumu wake.
- Nishati ya Nyuklia – Meli hizi hutumia reactors za nyuklia ambazo huziwezesha kusafiri kwa miaka 20 bila kuhitaji kuongeza mafuta.
- Idadi ya Ndege – Kila aircraft carrier hubeba wastani wa ndege 70 – 90 za kivita, zikiwemo F/A-18 Super Hornet, F-35 Lightning II na helikopta za kijeshi.
- Gharama ya Ujenzi – Carrier mpya kama USS Gerald R. Ford imegharimu takribani $13 bilioni, na hii haijumuishi gharama za uendeshaji na matengenezo.
- Kasi na Muda wa Baharini – Carrier inaweza kufikia kasi ya zaidi ya 30 knots (56 km/h) na inaweza kukaa baharini kwa muda mrefu, mara nyingine kwa miezi 6 hadi mwaka mmoja bila kurudi bandarini.