Victor Mlaki
JF-Expert Member
- May 1, 2016
- 4,151
- 4,277
Binadamu ameumbwa katika hali ya kuwajibika kipekee sana kwa ajili ya maisha yake kuliko viumbe wengine wengi tunaowaona katika uso wa Dunia.
Kuna mambo mengi mno ambayo binadamu akiyafanya yanamuua taratibutaratibu na mara nyingi zaidi kabla ya kifo halisi.
Siyo jambo la kushangaza kukutana na mtu anatembea lakini alishajiua mara nyingi mno kuelekea kifo chake.
Mambo saba yanayodhihirisha njia hizo ambazo ni hatari ni:-
1. Kuhifadhi kinyongo-Mfano kutunza watu waliokuudhi moyoni mwako kwa muda mrefu "keeping toxic people in your life"
2. Kuamini maoni ya watu kuhusu wewe na kuwafanya kana kwamba ni maisha yako."Maoni ya watu kuhusu maisha yako hatupaswi kuwa uhalisia wa maisha yako".Ukiona unaamini unachoambiwa kuhusu wewe na unakifanya kuwa uhalisia wa maisha yako jua hiyo siyo dalili nzuri.
3. Kufikiri furaha ni suala la baadae. Furaha katika maisha siyo suala la kughairisha kwa ajili ya baadae.Ukiona unaamini katika kuhuzunia na kusinoneka sasa kwa ajili ya baadae elewa hiyo ni dalili ya hatari kwa sababu furaha ni kile unachofanya kwa ajili ya sasa "something you design for the present"
4. Ulalamishi sugu (chronically complaining).
5. Kuishi kwa hofu. William Shakespeare Mtu anayeishi kwa hofu hujiua mara 1000 zaidi kabla ya kifo halisi.
6. Kutokuzingatia muda. Uhai unaweza kukudanganya kuwa unaendelea na ukizubaa ukachezea muda unaopita unaweza ukajikuta umejiweka kwenye hatari kubwa mno.
7. Kutokuwajibika. Hakuna mwenye wajibu wa kuyalinda maisha yako kama unavyopaswa kufanya wewe mwenyewe na unaposhindwa kuwajibika kikamilifu kwa ajili yako elewa hayupo atakayeweza kuchukua nafasi yako ya uwajibikaji juu yako.
Amua sasa "Maisha yako ni kwa ajili yako"
MoT.