Gyole
JF-Expert Member
- Sep 20, 2013
- 7,008
- 7,059
Biblia haijawahi kudanganya wala kukosea, biblia ni kila kitu katika maisha yetu, sema shida yetu Ni upungufu wa Imani, au kuyumbishwa na Imani za wasioamini, niseme tu usimwamini mtu yoyote duniani ila tu ishi nao kwa akili na tahadhari kubwa, kuna watu waliwaamini ndugu zao wakawaangamiza, kuna waliowaamini wazazi wao wakawaangamiza, kuna wengine waliowaamini wenza wao wakawamaliza, Hali kadhalika hata watoto waliowazaa au marafiki wakawaamini wakawaangamiza, haya maisha hayana formula, bila Mungu kusimama upande wako hakika dunia itakuangamiza hadi ukashangaa, na kinachotuponza Ni kutanguliza mapenzi/upendo wetu kwa watu pasipo kumtanguliza Mungu, kumbuka Shetani yupo duniani na kazi yake Ni kutafuta wafuasi, Mara nyingi hushughulika na wanaomwamini Mungu ili awaangushe, hivyo basi yeyote umpendaye na kumwamini anaweza kutumiwa na Shetani na akakuangamiza, hatuwezi kukwepa Ila tukimtanguliza Mungu hakika hawatatudhuru, tuendelee kuwapenda na kuwakmbea tuwapendao. Tuzidishe maombi na kumtegemea Mungu tu.
Mambo Ni mengi sana, Mungu aturehemu kwa pendo lake.
Sent using Jamii Forums mobile app
Mambo Ni mengi sana, Mungu aturehemu kwa pendo lake.
Tafadhali,kama ni mkristo soma Yeremia 12:6 halafu naomba mrejesho. Nimewahi kufanyiwa kitu kibaya sana na ndugu zangu kwa matumaini yao kwamba ninaweza kujiua. Kwa kweli ilikuwa mtihani mkubwa sana. Nashukuru sana Mungu hali sasa imetulia
Sent using Jamii Forums mobile app