Mambo 7 yanayopelekea kufa taratibu kabla ya kifo halisi

Biblia haijawahi kudanganya wala kukosea, biblia ni kila kitu katika maisha yetu, sema shida yetu Ni upungufu wa Imani, au kuyumbishwa na Imani za wasioamini, niseme tu usimwamini mtu yoyote duniani ila tu ishi nao kwa akili na tahadhari kubwa, kuna watu waliwaamini ndugu zao wakawaangamiza, kuna waliowaamini wazazi wao wakawaangamiza, kuna wengine waliowaamini wenza wao wakawamaliza, Hali kadhalika hata watoto waliowazaa au marafiki wakawaamini wakawaangamiza, haya maisha hayana formula, bila Mungu kusimama upande wako hakika dunia itakuangamiza hadi ukashangaa, na kinachotuponza Ni kutanguliza mapenzi/upendo wetu kwa watu pasipo kumtanguliza Mungu, kumbuka Shetani yupo duniani na kazi yake Ni kutafuta wafuasi, Mara nyingi hushughulika na wanaomwamini Mungu ili awaangushe, hivyo basi yeyote umpendaye na kumwamini anaweza kutumiwa na Shetani na akakuangamiza, hatuwezi kukwepa Ila tukimtanguliza Mungu hakika hawatatudhuru, tuendelee kuwapenda na kuwakmbea tuwapendao. Tuzidishe maombi na kumtegemea Mungu tu.
Mambo Ni mengi sana, Mungu aturehemu kwa pendo lake.
Tafadhali,kama ni mkristo soma Yeremia 12:6 halafu naomba mrejesho. Nimewahi kufanyiwa kitu kibaya sana na ndugu zangu kwa matumaini yao kwamba ninaweza kujiua. Kwa kweli ilikuwa mtihani mkubwa sana. Nashukuru sana Mungu hali sasa imetulia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimefurahi na kufarijika sana. Tafadhali on a pia Zaburi 55:12-14, 16
 
ukweli mtupu, iyo ya mwisho naigongelea msumari kabisa.
 
Kweli, kweli, kweli tupu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mi kinachonipunguzia furaha katika maisha ni kukosa Economic freedom!

Mpaka sasa sijafikia level ambayo naweza ku relax. Kuhusu kusamehe na kupotezea niko vyema na sina kawaida ya kusikiliza watu wanasema nini juu yangu so walimwengu hawaniumizi kwa maneno.
 
Ridhika na ulichonacho huku ukiendelea kupambana, kamwe huwezi ridhika hata ukifikia kiwango kikubwa cha uchumi endapo hutawajali wahitaji, kuwa mwema kwa wengine (kufanya udiakonia) itakusaidia kiasi
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimefarijika sana ndugu juu ya namna ulivyoonesha unafahamu ni kipi hasa unahitaji yaani "economic freedom".
Kutambua hitaji ni jambo moja na kupata unachohitaji ni kitu kingine.Tunapaswa kuwa makini sana katika kubaini ni kipi hasa tunahitaji.
Katika uzoefu wa maisha kwa mfano Mimi mwenyewe kuna wakati nilikuwa nafahamu kuwa nahitaji kitu fulani ila nilipokipata nilijikuta sijaridhika nahitaji kitu kingine zaidi.Hali hii ilinipa fundisho kuwa sikuweka utayari katika kubaini hitaji langu hasa ni lipi.
Tumeumbwa kwa namna ambayo tunaweza kuumba tuyatakayo au kutafuta tuyatakayo ili mradi mawazo yetu,hisia zetu,akili zetu na kani za uhai wetu zinaelekea kwenye uelekeo mmoja tunaouhitaji.Baadhi ya wataalamu wanamfananisha binadamu na sumaku kubwa "big magnet"inayoweza kuyavuta inayoyahitaji na kusukuma ambayo haiyahitaji.
Unakosa furaha kwa sababu ndiyo haswa unayoihitaji.Ngoja niandike taratibu huenda itaeleweka kiasi.
Economic freedom sicho hasa unachohitaji ila unachohitaji ni kuzalisha thamani zitakazokupatia uchumi ambao unadhani utakupa furaha "kwa maana nyingine economic freedom is not an end bu a means to an end.
You are welcome Brethren.
 
Kwa maana hiyo, wabongo wengi ni wafu wanaotembea. ๐Ÿšถ๐Ÿป๐Ÿšถ๐Ÿป
 
Naam!.. na siyo wabongo tu ila ni kizazi chote cha binadamu.Kifo na uhai ni pande mbili za sarafu ile ile moja.
Kwa maana hiyo, wabongo wengi ni wafu wanaotembea. ๐Ÿšถ๐Ÿป๐Ÿšถ๐Ÿป
 
Ridhika na ulichonacho huku ukiendelea kupambana, kamwe huwezi ridhika hata ukifikia kiwango kikubwa cha uchumi endapo hutawajali wahitaji, kuwa mwema kwa wengine (kufanya udiakonia) itakusaidia kiasi

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu kuna contradictory argument hapo.
Sidhani kama unaweza ukaridhika halafu ukaendelea kupambana kwa tafsiri ya neno ridhika".
Uumbaji wetu unaonesha hatuna asili ya kuridhika ila kukua na kujua zaidi na zaidi.Ndiyo maana yupo hai hatujafa kifo halisi lakini tunatamani kujua habari na uzoefu wa kifo halisi.
 
Peace


The Two Most Important Day In your Life Are The You Were Born And The Day You Find Out Why "

PEACE
 
Kuridhika Ni kuikubali Hali halisi na sio kuacha kusonga mbele

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiyo ndiyo maana ya kuridhika au uliyomaanisha wewe Mkuu?.
Kama ndiyo uliyomaanisha naunga mkono hoja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ