Mambo 8 ya kushangaza yanayofanywa na mwili wako kukulinda pasipo wewe kujua

Mambo 8 ya kushangaza yanayofanywa na mwili wako kukulinda pasipo wewe kujua

asante ndugu kwa mada nzuri,ila kuna sehemu kama sijaelewa vile! kwenye hio dayafram umesema hubakia mahali pake wakati hewa ikitoka, lakini ikiwa inaingia hushuka chini, sio inapanda na kushuka kama ulivyo upumuaji?
Ongezea;Ukipata kwikwi tulikuwa tunaambiwa kunywa maji na ukinywa tu kwikwi inakata,je ni sawa? Je kuna uhusiano ktk hili?
 
Mwili wa binadamu unafanya mambo mengi ya kibaiolojia ambayo mara nyingi ni vigumu kuyaelewa.

Mwili una mifumo mbalimbali ya ulinzi ambayo inatulinda na hatari zinazoweza kutudhuru. Mifumo hiyo inatulinda masaa 24 ya siku, Siku zote 7 za wiki, katika mambo yote yanayoweza kuhatarisha maisha yetu.

Yafuatayo ni mambo yanayofanywa na mwili ambayo ni kati ya hiyo mifumo ya ulinzi wa mwili wa binadamu.

1. KUPIGA MIAYO (YAWNING)
Lengo kubwa la kupiga muayo ni kuupoza ubongo baada ya joto kuzidi kwenye ubongo au baada ya ubongo kuchoka kufanya kazi.

Vile vile kama ukiwa umechoka au una njaa husabababisha oxygen kupungua kwenye damu na kwenye mapafu, hii hupelekea tatizo la kupumua, hivyo kupiga miayo husaidia kuingiza oxygen ya ziada mwilini ili irudishe mwili katika hali yake ya kawaida.

2. KUPIGA CHAFYA (SNEEZING)
Mara nyingi tunapiga chafya pale pua zetu zinapokua zimejaa bakteria wa magonjwa ambao hawahitajiki mwilini, Vumbi pamoja na takataka mbali mbali zilizoingia kupitia pua.

Hivyo kupiga chafya ni kitenda cha mwili kujisafisha kwa kuyatoa hayo matakataka nje yaliyoingia mwilini.

3. KUJINYOOSHA (STRETCHING)
Kuninyoosha mwili ni kitendo kisicho cha hiari ambacho lengo lake ni kuuandaa mwili kwa ajili ya kazi mbalimbali za kutumia nguvu utakazokabiliana nazo kwa siku nzima. Lakini pia kujinyoosha kunaipa misuli ya mwili mazoezi na kuiweka sawa vilevile kunarudisha mzunguko wa damu katika hali yake ya kawaida na kumtoa mtu katika uchovu.

4. KWIKWI (HICCUPING)
Najua umewahi kupata kwikwi, na mara nyingi mara baada ya kumaliza kula chakula. Je umeshawahi kujiuliza ile sauti ya ajabu ya kwikwi inasababishwa na nini au kwa sabababu gani watu hushikwa na kwikwi?

Hiyo yote husababishwa na DIAPHRAGM (tamka DAYA - FRAM) kiungo kinachopatikana ndani ya mwili wa binadamu chini kabisa ya kifua baada ya mapafu(lungs). Kazi kubwa ya diaphragm ni kusaidia katika upumuaji, (inhale) na (exhale). Pale unapoingiza hewa ndani (inhale) diaphragm hushuka chini ili kusaidia kuivuta hewa ifike kwenye mapafu. Na unapotoa hewa nje (exhale) diaphragm hutulia kwa kubakia sehem yake ili kuwezesha hewa chafu kutoka nje kupitia pua na mdomo.

Sasa basi, kuna wakati diaphragm kubugudhiwa na kuisababisha kushuka chini kwa kasi sana jambo linalosababisha wewe kuvuta hewa (inhale) kwa kasi isiyo ya kawaida kupitia koromeo la sauti, hewa ikifika kwenye box la sauti (larynx), sehem hiyo hujifunga kwa haraka sana ili kuzuia hewa isipite huko na ndipo KWIKWI hutokea.

Mambo mengine yanayoweza kuibugudhi diaphragm na kuisababisha kufanya kazi vibaya mpaka kupelekea kwikwi ni kitendo cha kula haraka haraka au kuvimbewa.

5. KUJIKUNJA KWA NGOZI YA VIDOLE VYA MIKONO BAADA YA KULOWA AU KUKAA MUDA MREFU KWENYE MAJI.
Je umewahi shuhudia jinsi ngozi ya vidole vyako inavyojikunja baada ya kufua nguo muda mrefu au kushika maji muda mrefu? Unajua ni kwa sababu gani ngozi hujikunja kama ya mtu aliyezeeka angali yu kijana mara baada ya kukaa sana kwenye maji?

Watu wengi kabla walizani kwamba kujikunja kwa ngozi hiyo hutokana na maji kuingia kwenye ngozi na hivyo ngozi hujikunja baada ya kulowa.

Lakini wanasayansi baada ya kufanya utafiti kwa muda merefu juu ya nini hasa hupelekea ngozi kujikunja? Walisema HAPANA si kwa sababu ya ngozi kulowana. Na walikuja na majibu haya.

Mwili unapokutana na majimaji mara moja hupeleka taarifa na kutafsiri kwamba mazingira hayo yana UTELEZI (Slippery) hivyo kutasababisha mikono kushindwa kushika (Grip) au kukamata vitu kwa urahisi kutokana na utelezi huo. Hapo mwili huchukua hatua ya haraka kuikunja ngozi ya mikono yako ili kurahisisha ushikaji wa vitu vinavyoteleza ndani ya maji pamoja na kutembea kwenye utelezi.

6. VIPELE VIPELE VYA BARIDI KWENYE NGOZI (GOOSEBUMPS)
Kazi kubwa ya vipele hivi ni kupunguza kiasi cha joto la mwili linalopotea kupitia matundu ya ngozi. Hivyo kwa kufanya hivi humfanya binadamu kutunza joto la mwili hata katika mazingira ambayo hali yake ya hewa si rafiki kwa mwili wa mwanadamu au ni yenye baridi sana.

7. MACHOZI (TEARS)
Zaidi ya kuwa majimaji (MUCOUS MEMBRANE ) yanayopatikana kwenye Macho ambayo kazi zake ni kulilinda jicho dhidi ya kitu chochote kigeni kinachoingia jichoni (mfano unapokata vitunguu au mdudu anapoingia jichoni huwa unatoa machozi mengi eeeh!! Pia dhidi ya upepo na moshi) na pia hutumika kama kilainishi cha jicho pale linapokuwa linazunguka zunguka (blink).

Vilevile machozi yana kazi ya kupunguza HISIA ZA HUDHUNI zinazozalishwa mwilini. Wanasayansi wanaamini kuwa mtu anapokua mwenye msongo wa mawazo (stress) mwili hutengeneza kitu kipya ili kwenda kubugudhi na kuharibu maumivu yote ambayo mtu anajisikia. Hivyo machozi yanayozalishwa hapa huwa na kemikali na yanafahamika kama NATURAL PAINKILLER. Machozi haya ni tofauti na machozi ya kawaida, lengo lake hasa la kuzalishwa ni kwa ajili ya kuondoa kabisa maumivu yaliyozalishwa mwilini

Hivyo mpaka hapa tumeona kua kuna machozi ya aina tatu ambayo ni
i. Basal tears (vilainishi)
ii. Reflex tears (mlinzi)
iii. Emotion tears (mtuliza maumivu)

8. KUSHTUKA USINGIZINI (MYOCLONIC JERKS or HYPNIC JERK).
Je! Ushawahi kutokewa na hali hii? umelala halafu ghafla unashtuka usingizini kwa mguvu nyingi kama umepigwa na shoti ya umeme na akili inakurudi ghafla huku mapigo ya moyo yakikuenda mbio? Na hali hii ikakutokea pasipo hata kuota ndoto yoyote?

Basi usiogope au kuwasingizia watu uchawi, hii ni hali ya sayansi ya mwili.na ni njia moja wapo katika ile mifumo ya mwili kujilinda.

Je hutokeaje?

Hii ni hali ya ajabu sana isiyofanywa kwa hiari ambayo huwatokea watu mara tu wamejinyoosha kitandani na kupitiwa na usingizi, mwili hutetemeshwa na kusukumwa kwa nguvu na mtu hushtuka katika hali kama vile kapigwa na shoti ya umeme. Hali hii inaweza kupelekea mtu hata kuanguka kitandani na humwamsha mara moja kutoka usingizini.

Wanasayansi wanatuambia kua, pale tu unapopata usingizi kiwango cha upumuaji kinashuka ghafla, mapigo ya moyo nayo taratibu yanapungua, misuli inatulia kwa ku-relax, Kitu cha AJABU hapa ubongo unatafsiri hali hii kama ni DALILI ZA KIFO (brain's misinterpretation of muscle relaxation), hivyo huchukua hatua za haraka za kuushtua mwili kwa kuutetemesha au kuuskuma kwa nguvu, hali ambayo humfanya mtu kuamka kutoka usingizini kwa KURUKA kitu ambacho ni hali isiyo ya kawaida.

Hali hii ikimtokea mtu huambatana na kuongezeka kwa mapigo ya moyo (rapid heartbeat), kuhema haraka haraka, na wakati mwingine mtu hutokwa na jasho jingi.

Wakati mwingine mtu huamka ametoa macho na kama ukimwangalia, nae huishia hukuangalia tu huku akikosa la kukujibu endapo utamuuliza vipi kuna tatizo gani?

MWILI WAKO NI ZAIDI YA UNAVYOUJUA. JAMBO LA MSINGI NI KUONDOA HOFU KWANI MWILI WAKO UNAJUA NINI UFANYE NA WAKATI GANI ILI KUKULINDA USIKU NA MCHANA KATIKA SIKU ZOTE ZA MAISHA YAKO.


0c5d4ca51800dde9a60c56e39d445160.jpg
4dc76569183c5e8a2a1778f8ae374a5e.jpg
b970ba04b00b649424c4b505a48519f7.jpg
a924a449d823a9bcfa8f30e01dd43652.jpg
121502feb394da6e444f4984e50018bc.jpg
97a509b00a12e26efc93d2fe9e3234f6.jpg
9)Kujigeuza geuza mara kwa mara ukiwa usingizini;Wataalam wanasema unapokuwa umelala upande mmoja kwa muda upelekea upande kuchoka kwa misuli na mishipa ya damu na kufanya mzunguko wa damu kuwa mdogo upande huo so automatic utajikuta unajigeuza mwenyewe bila kujua na kurelease upande huo wa mwili
 
Vipi kuhusu ngozi kutetemeka hususani kama unatembea usiku kwenye maeneo yalikuwa na ukimya sana
 
Mwili una njia nyingi za kujilinda mpaka unasababisha kero ya allergy
 
Kwa kuongezea pia mwili unakupa taarifa au taadhari kupita hisia mbali mbali zifuatazo ni hisia kumi
Action Signals

According to Tony, here are what the 10 Action Signals mean:

01. Uncomfortable – When you feel uncomfortable, this is a signal to change your state. Clarify what you want, then take action in that direction.
02. Fear – Fear is a signal to prepare ourselves or get prepared. Get yourself prepared to deal with something that’s about to come. If it’s beyond your control, then change your perception and let it go.

03.Hurt – Hurt is a signal that you have an expectation that’s not being met or you have a sense of loss. Evaluate whether there really is a loss. Next, change your perception or change your way of communicating your needs or change your behavior.

04.Anger – This is a signal that an important rule that you have in your life has been violated by somebody else or maybe even you. Clarify your rules or adjust them. Your rules might not match other people’s rules so if you don’t change them, you might be angry the rest of your life.

05.Frustration – The signal is you’re doing the same thing over again and expecting a different result. You need to change your approach to achieving your goal.

06. Disappointment – This is a signal that you need to realize that an expectation or an outcome you had won’t happen, and you need to change your expectation. For example, maybe your timeframe was too short.

07 Guilt – Guilt is a signal that you violated one of your own standards. Don’t stay in guilt, but don’t deny it. Make things right when you screw up. When you can’t change the past, change your present and future behaviors. Recognize when you’re feeling guilty when you shouldn’t be, change your perception, and let it go.

08. Inadequacy – This is a signal that you need to do something to get better. Get up and do something to get better or change your criteria. Maybe your rules are too harsh. You don’t have to be perfect – you simply need to start taking action, such as go practice, to improve at whatever it is.

09. Overloaded – This is a signal to reevaluate what is most important to you in this situation. Distinguish between what is a necessity versus. what is a desire. Prioritize your list. Take the first one on your list and do something about it. Do something to take control of events instead of let them control you. The simplest way is to chunk it down, take one thing, and act on it.

10. Loneliness – The signal is we need a connection with people. Clarify what kind of connection you need: basic friendship, somebody to laugh with, somebody to listen to you, etc. Then change your approach or change your perception..

I have to say, this is some of the most effective and actionable guidance I’ve heard on mastering emotions.
 
Pale kwenye namba 8 umesema
Kuna machozi ya vilainishi, ya ulinzi na ya uchungu, na kila aina umeifafanua vizuri na imeeleweka vyema

Je pale mtu anapofurahi sana hadi akalia, ile nayo unaisemeaje?

Au furaha na uchungu katika sayansi hiyo vina tafsiri sawa?
 
Pale kwenye namba 8 umesema
Kuna machozi ya vilainishi, ya ulinzi na ya uchungu, na kila aina umeifafanua vizuri na imeeleweka vyema

Je pale mtu anapofurahi sana hadi akalia, ile nayo unaisemeaje?

Au furaha na uchungu katika sayansi hiyo vina tafsiri sawa?
Ndiyo mkuu, kwa jina jingine tunayaita MACHOZI YA HISIA furaha na uchungu zipo sehem moja
 
Ongezea;Ukipata kwikwi tulikuwa tunaambiwa kunywa maji na ukinywa tu kwikwi inakata,je ni sawa? Je kuna uhusiano ktk hili?
Zipo njia nyingi zinazoelezwa ambazo zinzweza saidia kuondoa kwikwi, mojawapo ni kunywa maji, nyingine ni kupata mshtuko kwa kushtuliwa.
 
Back
Top Bottom