Mambo ambayo Babu zetu walitusihi tuyafuate kwenye mahusiano lakini tuliyapuuza sasa tunaonja joto la Jiwe

Mambo ambayo Babu zetu walitusihi tuyafuate kwenye mahusiano lakini tuliyapuuza sasa tunaonja joto la Jiwe

Taikon umesahau jambo la Muhimu sana, Mwanaume tahiriwa jandoni na peleka kijana wako Jando

Hili linasaidia sana kulinda hulka za kiume namaadili pia yanayopatikana kwenye mafunzo ya jandoni

Tabia ya Wanawake kupeleka Watoto tena wadogo kutahiriwa hospitalini ni mbaya inatengeneza mashoga

Excuse me kama ni nje ya mada yako

Jambo lingine ni Mwanaume kufanya KAZI na kuprovide kwa familia na sio Mwanamke ndio alete mkate wa nyumbani, hii inaleta dhana mbaya kwa watoto
 
Mkuu, hakuna ulichokosea, ulichofanya ni kuongeza nyama.

Ipo haja ya kufanya mapitio katika mambo haya
 
Kwema Wakuu!

Nashukuru Kwa sababu mpaka sasa Nina mialiko mitatu ya Idi, nawashukuru wote mlionialika. Nirejee kwenye mada.
Kama kichwa kinavyojieleza hapo juu, Hii ni orodha ya mambo tuliokatazwa na kusisitizwa na Wazee wetu linapokuja suala la mahusiano ya ndoa, sasa Vijana wanapiga mayowe.

1. OA BIKRA
Hii ilikuwa moja ya hoja kuu Kwa kijana anayeenda kuoa. Mimi kama Taikon ninawaelewa wazee na nina sababu ya kufanya hivyo. Ingawaje inaweza kuwa ni Mtazamo wa kizamani lakini Kwa wanaouzingatia wengi wao wanapata matokeo chanya.

2. OA Kabila lako au mnaolingana Mila na desturi. Achana na hawa Watoto wasiojua maana ya kabila, sijui Mila na desturi, hawa waliozaliwa mjini. Hao hawawezi kuwa kitu kinachoitwa ukabila.

Mahusiano hayajawahi kuwasumbua Watu wanaofuata mambo ya Mila na desturi za makabila Yao. Mapenzi yanayosumbua Wenye kuiga Mila za kigeni, wasomi na wadandia Mambo kama dini za kigeni.

3. Mwanaume ni kichwa cha Nyumba.
Kichwa kina ubongo, macho, masikio, mdomo. Mwanaume lazima uwe mwanaume, ukisema umesema, ukisimamia Jambo umesimamia, mchakarikaji, unayejituma kwaajili ya familia na jamii yako.

Hakuna usawa baina ya Mwanamke na Mwanaume. Mwanaume hapswi kufuata matakwa ya MKE au Mwanamke. Wote wanaofuata Kanuni hiyo mahusiano hayawezi kuwasumbua. Hata hivyo mwanaume kama kichwa cha Nyumba hapaswi kuwa muonevu na kutowatendea Haki Watu wa nyumba yake.

4. Mwanaume Halii
Mwanaume kujilizaliza, kutia Tia huruma, sijui. Kupiga magoti au kuwa chawa na mpambe mpambe kijingajinga Huko ni kujiingiza kwenye ushoga. Hakuna Mwanamke anayempenda mwanaume lainilaini, mliaji liaji, dekaji dekaji, hakuna.
Mahusiano lazima yakusumbue tuu!
Umetongoza Mwanamke kakukatalia Achana naye, usibembeleze na kujiliza Liza kama lipuuzi, usije ukadhani kujiliza ndio kutaugeuza moyo WA Mwanamke, zaidi Sana atakudharau.

Umepata matatizo kidogo unalia, sasa unalia nini kama mtoto, sasa Baba mzima unalia Mkeo na watoto wafanye nini. Mwanaume lazima uwe ngangari.

Hawa Wanawake wapo hivi walivyo Kwa sababu siku hizi wanaume wengi wamekuwa kama Wanawake.

Wanawake wanapenda Wanaume washoka, wahuni, wenye Roho ngumu, wasioogopa, wenye Akili, wenye maamuzi.

Nipumzike Sasa.

Taikon wa Fasihi
Dar es salaam
I think kikubwa ambacho watu wamepuuza ni "Uzuri wa mwanamke si sura ni tabia"
 
I think kikubwa ambacho watu wamepuuza ni "Uzuri wa mwanamke si sura ni tabia"

Wanaume tumejisahahu Kwa mambo mengi.
Mbali na hivyo, baadhi ya wanaume wamekuwa wakifanya ukatili na unyanyasaji Kisa wajibu wao wa kuhudumia familia.

Taikon ninafuata mfumo dume kwani ndio mfumo salama Kwa familia na Jamii. Lakini wengine Mfumo dume wanautumia kufanya Isivyo Haki.

Uzuri WA Mwanamke ni Tabia, Sura itatokana na matunzo Kutoka Kwa mumewe
 
Back
Top Bottom