Mambo ambayo yametokea toka Man utd iliposhinda taji la EPL mwaka 2013

Mchochezi

JF-Expert Member
Joined
Feb 29, 2012
Posts
10,962
Reaction score
7,830
Ni miaka takribani mitano sasa toka Man Utd walipotwaa ndoo ya Ubingwa wa EPL chini ya uongozi wa Legendary, Sir Alex Ferguson.

Miaka mitano ni mingi sana, hapo ndani ya miaka mitano kumetokea mambo mengi sana kama yafuatayo;

Magufuli alikuwa Waziri wa Ujenzi, akaja akagombania Urais na sasa amebakiza miaka miwili amalize muhula wake wa kwanza.

Leicester City imepanda daraja na kubeba ubingwa wa EPL huku Man Utd wakiendelea kuyumba.

Chelsea imeshinda mataji mawili ya EPL ikiwa na makocha wawili tofauti ambao ni Mourinho mwaka 2015 na Conte mwaka 2017.

Mbappe katoka timu ya mtaani akasajiliwa Monaco kisha akavunja rekodi ya usajili kwa mchezaji kijana kwa kusajiliwa PSG na kuitumikia Ufaransa mpaka kutwaa ubingwa wa Kombe la Dunia huku akiwa na tuzo ya mchezaji bora kijana wa mashindano hayo.

Halotel ikaja Tanzania, ikajinyakulia wateja kwa kuwa ni mtandao wenye spidi, kisha sasa imepoteza mvuto.

Real Madrid wametwaa klabu bingwa Ulaya mara nne ikiwa na makocha wawili tofauti.

Marekani ilikuwa ikiongozwa na Obama ila sasa yupo Trump.

Bei ya Sukari ilikuwa nchini Tanzania ilikuwa ni Tsh 850.

Staa wa muziki wa Bongofleva alikuwa Juma Nature

Ongeza na ya kwako unayoikumbuka...
 
Inatufundisha nini mkuu?
 
Keely Navas alikua akichezea timu ndogo tu ya la liga na mwenyewe akijiona maisha kashayamaliza karidhika kabisa kutoka alipotoka mpaka kufika la liga, na aliona wazi kuwa yale ndio mafanikio ya juu kabisa katika maisha yake, na wala hakutarijia ziada ya pale. Lakini ndani ya miaka hii toka 2013, Ameng'ara ndani ya world cup, Akachukuliwa Real Madrid na akawa Real madrid No 1 (Jambo ambalo hajawahilifikiria hata ndotoni) na amewin 3 times Champion league, 3 times club world cup, 1 Spanish la liga, 1 Spanish super cup, 3 European Super cup. NA pia ameshinda tunzo ya kipo bora ulaya 2018.
 
Back
Top Bottom