Mambo gani muhimu ya Kumfundisha Mtoto mapema kabla hajawa nunda?

Mambo gani muhimu ya Kumfundisha Mtoto mapema kabla hajawa nunda?

Enzi za utoto
FB_IMG_1700581328734.jpg
 
Ukiwa Mzazi bila shaka unabeba jukumu kubwa la malezi na jinsi unataka kumshape mwanao. Ni mambo gani unahakikisha mwanao anayajua mapema?
Mambo ya msingi ya mwanao kujua mapema navofikiri ni kutopenda kukaa peke yake, na asiwe muoga wa kuzungumza. Wakati akikua zaidi, mfundishe Maandiko Matakatifu na kumuabudu Mungu akiwa mdogo, mfundishe umuhimu wa kuwa na Mungu katika maisha yake .

Alafu kama kuna stadi ya kazi unaijua, mfundishe mapema sana, mfundishe pia kufagia uwanja, kupika kwa mtoto wa kike, kupanga vizuri chumba chake, kutandika kitanda .
 
kwanza kabisa hakikisha ufundishe aweze kujitegemea mambo binafsi, usije fanya kosa la kumnyima kazi za nyumbani ila ziwe zinaendana na umri wake.

Mtoto mdogp tu wa miaka miwili inabidi aanze kujifunza kurudisha mahali panapostahili kitu akichochukua, nashangaa watoto wanaletewa mahausi geli mtu anafika miaka 13 hana mazoea hata ya mtoto wa miaka mitano anaejitandikia kitanda kila siku.

Ukiona mtoto kafika 13 hajamjengea mazoea ya kazi za nyumbani basi wewe kama mzazi umefeli sana, umri huo ndio mwisho wa kuwa mtoto, baada ya hapo ngumu sana kumfundisha

MIAKA 3

Majukumu binafsi

Kuoga mwenyewe chini ya uangalizi
kupiga mswaki kila akiamka na kabla ya kulala
Kuweka nguo chafu kwenye tenga
Akimaliza kula apeleke chombo sehemu ya kuoshea
akimaliza kutumia kitu ajue pa kukirudisha na kukipanga (toys, midoli, vitabu, rimoti. n.k)


MIAKA 4 - 5

Majukumu Binafsi

Kuchota maji yakuogea na kujiogesha bila kufunga mlango
kufua nguo nyepesi za ndani, leso na soksi.
kufuta meza baada ya kula.
kuosha sahani yake aliyolia.
kukunja nguo zake


Majukumu ya kifamilia

kufuta vyombo vilivyooshwa kasoro vyenye ncha kali

fatilia zaidi 👇👇

Kumnyima mtoto kazi za nyumbani sio kumjali bali ni kumuharibu. Hizi ni orodha za kazi inazobidi azoee kulingana na umri wake
 
Yote yalio tajwa yapo sawa lakin mlinzi wake ni kumfundisha mtoto umoja na ushilikiano na wenzake topic hii inasahaulika Sana lakin ni muhimu ata akikosa hayo mliotaja umoja wake na ushilikiano na wenzake utampa itaji hilo
 
Cha kuongezea, mfundishe jinsi ya kuhesabu hela na kuwa na nidhamu ya pesa toka akiwa mdogo, mfundishe jinsi ya kupanga bajeti ya matumizi yake na ikiwezekana ayaandike kwenye daftari. Msimamie kabisa uhakikishe anayafanya yote haya.
Mie wanangu nawapaga buku buku wikendi,nawaambia mwanaume hatakiwi kukosa hela,Ila iwe halali.
 
Cha kwanza dini mfundishe imani ni nini
Cha pili mila za kwenu kuwa kipi kinatakiwa
Cha tatu upendo, kusamehe na uvumilivu

Ila yote kwa yote, mtoto ana haki ya kucheza hakikisha anaipata hiyo fursa vizuri
 
Mfano mzuri unaanza kutoka kwako wewe kwanza...
 
Ukiwa Mzazi bila shaka unabeba jukumu kubwa la malezi na jinsi unataka kumshape mwanao. Ni mambo gani unahakikisha mwanao anayajua mapema?
1. Usafi. Mzoeshe kunawia mikono kwa sabuni kila anapojisaidia. Mzoeshe kufanya hivyo tokea akiwa "mchanga", kila ajisaidiapo, akishasafishwa, anawishwe kwa maji safi na sabuni. Hiyo tabia itazama kwenye ufahamu wake wa ndani na kuwa sehemu ya maisha yake.

2. Kujitegemea.
Kama nyumba ina nafasi, mzoeshe kulala chumbani kwake peke yake tokea akiwa mdogo, labda miezi sita.

Hata anapozaliwa, ikiwezekana, akute kuna kitanda chake, hivyo hata kama mwanzoni atalala chumbani kwa wazazi wake, iwe ni kitandani kwake.

Hiyo inaweza kumsaidia kuwa jasiri maishani mwake katika utu uzima wake. Siyo unamkuta mtu hawezi kwenda nchi ngeni peke yake kisa hajazoea "kujitegemea" tokea awali.

Sijathibitisha, lakini nafikiri, mtu aliyezoeshwa kujitegemea tokea akiwa mtoto, ana ujasiri zaidi wa "kutake risk" kuliko aliyezoeshwa kutegemea.
 
Back
Top Bottom