kwanza kabisa hakikisha ufundishe aweze kujitegemea mambo binafsi, usije fanya kosa la kumnyima kazi za nyumbani ila ziwe zinaendana na umri wake.
Mtoto mdogp tu wa miaka miwili inabidi aanze kujifunza kurudisha mahali panapostahili kitu akichochukua, nashangaa watoto wanaletewa mahausi geli mtu anafika miaka 13 hana mazoea hata ya mtoto wa miaka mitano anaejitandikia kitanda kila siku.
Ukiona mtoto kafika 13 hajamjengea mazoea ya kazi za nyumbani basi wewe kama mzazi umefeli sana, umri huo ndio mwisho wa kuwa mtoto, baada ya hapo ngumu sana kumfundisha
MIAKA 3
Majukumu binafsi
Kuoga mwenyewe chini ya uangalizi
kupiga mswaki kila akiamka na kabla ya kulala
Kuweka nguo chafu kwenye tenga
Akimaliza kula apeleke chombo sehemu ya kuoshea
akimaliza kutumia kitu ajue pa kukirudisha na kukipanga (toys, midoli, vitabu, rimoti. n.k)
MIAKA 4 - 5
Majukumu Binafsi
Kuchota maji yakuogea na kujiogesha bila kufunga mlango
kufua nguo nyepesi za ndani, leso na soksi.
kufuta meza baada ya kula.
kuosha sahani yake aliyolia.
kukunja nguo zake
Majukumu ya kifamilia
kufuta vyombo vilivyooshwa kasoro vyenye ncha kali
fatilia zaidi 👇👇
Kumnyima mtoto kazi za nyumbani sio kumjali bali ni kumuharibu. Hizi ni orodha za kazi inazobidi azoee kulingana na umri wake