Mambo haya yanaliua jukwaa la Biashara na Uchumi

October man

JF-Expert Member
Joined
Nov 23, 2017
Posts
3,635
Reaction score
5,012
Moja ya sehemu ambayo utawapata watu siriasi Tanzania ni hapa jamii forums, lakini kwa sasa jukwaa limekuwa na watu wa ajabu ajabu ambao wanauwa jukwaa zima na kufukuza watu wenye tija kabisa na vitu vyenye tija, moja ya vitu vinavyolipelekea jukwaa hili kufa ni kama:-

a) Kuwasakama watu wenye tija kwenye jukwaa, kama uwanja wa ujasiriamali tunahitaji manguri wa huu uwanja lakini, kinachoshuhudiwa watu wenyewe wanapigwa vita mpaka wanalikimbia jukwaa, mfano usioweza kuukimbia ni ONTARIO.



ONTARIO, jamaa kimsingi alikuwa na pande kuu tatu

· Mada za ujasiriamali wa kweli zilizo wavutia wengi, binafsi nimekuwa mfuasi wa jukwaa hili kwaajiri ya stori zake za ujasiriamali na mafanikio, kiukweli zile stori siwezi jua nitazipata wapi tena.

· Stori za kawaida za maisha kama zile za south, technology na intelligensia.

· Network market.

Kimsingi watu wasioona umuhimu wake kwenye mada za ujasiriamali wamemsakama kwenye kipengere cha network market mpaka sisi wengine tumekosa faida zote tatu, nakumbuka kuna jamaa alikuwa maarufu kumshusha kwenye mada zake, lakini baada ya kuondoka jamaa hakuna anachoposti zaidi ya ujinga ujinga tu mpaka kapotea kabisa.

Usishangae siku ukaenda kwenye jukwaa la intelligence ukakuta THE BOLD anaogeshwa maneno



b) Kuwa clash watu wanaoleta mada zenye tija na ku-inpire, yaani mtu analeta mada kwa faida yako, hata umripi lakini izo comment anazopokea, mfano kuna mtu anaitwa CHASHA FARM uyu mtu analetaga vitu vya msingi ila anakoma kwenye replies za watu.



c) Kujengeka kwa kauri za ajabu kama “UKIONA UNAITWA KWENYE FURSA JUWA WEWE NDIO FURSA YENYEWE”, hakuna msemo ninaouchukia kama huwo na sitegemei mtu timamu ataongea msemo kama huwo, ukiitwa kwenye fursa ichambue fursa umepewa akili, ila kwa kuwa na akili za kizembe kama uwo msemo, hutabadilika kamwe.



d) Mtu akitoa hoja, kuanza kuchunguza post zake za zamani



Kama unakauri kama hizo ni muda kubadilika sasa humu jf hakuna anayekejua wala kumjua, pambania binafsi yako sio kufuata mkumbo, binafsi jf imenipa fursa kubwa ambayo sitokuja kujutia kuitumia jf maisha yote (uwekezaji), ila ukiletewa wewe fursa kama hiyo utafuata mkumbo wa maneno ya watu "ukiitwa wenye fursa jua wewe ndio fursa", kimsingi neno fursa limebadilishwa na kuwa aina furani ya dhambi.



FRASH BACK

Hapo nyuma kidogo mdau anaitwa CHASHA FARM, alianzisha mada kuhusu wachina kuungana, na mimi nikaona ndio muda sahihi nikaandika kuhusu kuungana hakukuwa na response yoyote ya watu na kuna mdau akaandika UKIONA UNAITWA KWENYE FURSA JUA WEWE NDIO FURSA MWENYEWE, tokea hapo nimejua kwa Tanzania kuwa mbinafsi huwenda ikawa neema kwa mungu na mungu akakupa swawabu pia.

mpaka mtu umpate msoto ndio ajue vitu vya msingi time will tell kila mtu kwa upande wak, itapoteli haiteli kwa jf bali kwako pekeyako hutomuona mwana jf muda huwo.

jifunze kutumia privacy ya jf kupata fursa, vitu vyenye tija kwa maisha yako sio kufuata mkumbo na kumuonea mtu aibu, hakujui mtu anayekujua humu.
 
Kama unakauri kama hizo ni muda kubadilika sasa humu jf hakuna anayekejua wala kumjua, binafsi jf imenipa fursa kubwa ambayo sitokuja kujutia kuitumia jf maisha yote,
Kwa hili tuko kwenye boti moja.
tokea hapo nimejua kwa Tanzania kuwa mbinafsi huwenda ikawa neema kwa mungu na mungu akakupa swawabu pia.
Hili ndilo linatumaliza na kutufanya tuendelee kuwa maskini. Ubinafsi usio na Tija.
 
mkuu! hawa member wa humu jf ndyo sampo ya watanzania tulivyo! hatuamini ktk chochote tupo negative mno

kila ukileta fursa humu utaonekana mwizi tu! unatka kuibia watu

hebu ona kilichomtokea ontario nadhan mpaka leo anajuta kuifahamu jf

hyo chasa farming ubishi tu ndyo unamfanya aendelee kuwa humu la sivyo na yeye angekuwa ashaondoka

wabongo ni ubishi na ujuaji na kupenda short cut

ukiwaletea ishu ya kustruggle ya kutolea jasho ili watusue..watafanya wiki mbili tu wakikutana na ugumu tu!

kesho yake utafunguliwa thread humu na kuitwa tapeli
 
Usigeuke nyuma utageuka jiwe.....ukifanya chochote wapo watakaokupigia kelele na kukukatisha tamaa. Wewe songa mbele tu usisikilize kelele zao, huwezi kuzuia watu kusema.
Haya ndiyo majibu sahihi
 
Baadhi ya watanzania ni watu ovyo sana ndio wanafanya paka wasiyo ovyo kuonekana ni ovyo kwa kweli mimi uwa nakomaa na chenye manufaa tu hizi kilele ni nyingi sana kikubwa achana nazo
 
namuonea huruma ontario wa watu kwa vita aliyopigwa ila bora nimeijua jf wakati sahihi na akili za watu wa humu nishazizoea mwanzo nilipojiunga nilikua nafurah kwa majibu ya watu humu haijalishi kitu ni siriasi au utani
 
ONTARIO anatetewa sana aisee,
Yaani kila kukicha ni Watetezi wake wanakuja kwa gia tofauti,
 
katika watu 100 usitegemee wote watakuwa upande wako.

naamini hamkukabwa.
 
Tatizo Kuna watu waliibuka kwenye Hilo jukwaa wakawa wanatapeli watu waliowaamini.

Sasa watu wana-question na kudadisi kitu ambacho wengine hamtaki.

Unamjua kitomai WA batabukini alivyoliza watu huko.

Ukiona watu wote wanakubaliana kila kitu jua wengine hawafikirii sawasawa.
 
Ukiona group la watu wote wanasema NDIO basi ujue watu wanapelekeshwa hapo. Sijawahi ona mada hapa JF ikose negative comment angalau hata moja haijalishi hiyo mada ikoje.
 
Ukiona group la watu wote wanasema NDIO basi ujue watu wanapelekeshwa hapo. Sijawahi ona mada hapa JF ikose negative comment angalau hata moja haijalishi hiyo mada ikoje.
Jamaa kamaindi kisa Ontario kusakamwa,
Alitaka wote tukubaliane na Ontario.

Ukiona katika Jamii kila mtu anafikiri sawa sawa basi wengine kati yao watakua wamewakabidhi akili zao waliobaki wawasaidie kufikiri kwa niaba yao.
 
Watanzania ni watu Wa ajabu sana.
Mtu kawatapeli watu lakn bado mnataka watu wasiseme ukweli mnataka aendelee kusifiwa tu..
Huu ni udhaifu Wa hali ya juu sana.
 
Hao ndio waTANZANIA chief wazoee tu,

Kuna jamaa mmoja pia alikuja na uzi kuuliza

"Watanzania mnajionaje?"

Hile mada mm niliipenda maana nilijua tutajadili mambo mengi ila jamaa alishambuliwa hahaha...

aliewaroga waTZ asee ana dhambi kubwa sana [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Jamaa kamaindi kisa Ontario kusakamwa,
Alitaka wote tukubaliane na Ontario.

Ukiona katika Jamii kila mtu anafikiri sawa sawa basi wengine kati yao watakua wamewakabidhi akili zao waliobaki wawasaidie kufikiri kwa niaba yao.
Watu wanapoteza hela zao tena kuf
Jamaa kamaindi kisa Ontario kusakamwa,
Alitaka wote tukubaliane na Ontario.

Ukiona katika Jamii kila mtu anafikiri sawa sawa basi wengine kati yao watakua wamewakabidhi akili zao waliobaki wawasaidie kufikiri kwa niaba yao.
sijui ni kivipi ontario atakwepa lawama hasa kwenye hili la forex na kampuni yake ya TMT, watu wamepoteza hela tena kwa kufuata maelekezo wa mentor wao uchwara Cre.
 
duu mada aihusu ONTARIO bali katokea kama mfano, ila imegeuka mada ya ontario na mifano mingine hata aiyonekani, CHASHA FARM katajwa mara nyingi kuliko ONTARIO lakini watu ONTARIO tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…