Nafaka
JF-Expert Member
- Feb 17, 2015
- 12,154
- 31,246
Huyu jamaa alikuwa na akili nyingi sana. Ni mmoja kati ya waanzilishi wa kampuni ya apple. Yeye na Billgates walikuwa mahasimu wakubwa sana kila mmoja akimdharau mwenzake.
Mfano Steve Jobs alikuwa anasema Billgates hana taste ya vitu vizuri, hata OS yake ya ovyo tu, ila ni bahati tu business model yake imefanya kazi. Gates naye alikuwa anamdharau Steve anamuona kama ni kichaa tu.
Wakati apple inataka kumrudisha Jobs kazini, (Jobs japo alikuwa mwanzilishi wa apple, ila aliwahi kufukuzwa kazi na bodi ya wakurugenzi halafu wakamteua jamaa ambaye jobs ndiye alimleta mwenyewe apple).
Baada ya miaka mingi apple ikawa haifanyi vizuri wakaamua kumrudisha Jobs. Gates aliposikia alipiga simu apple akawambia hivi wamechanganyikiwa. Wanataka kumrudisha mtu ambaye hajui lolote kuhusu technology, wala hawezi kucode hata mstari mmoja wa program. Akasisitiza kwamba kama wataendelea kubisha watakuja kujuta mbeleni.
Jobs alimprove gates wrong baada ya kurudishwa aliiletea apple mafanikio makubwa kwa bidhaa safi, kama ipod, iphone, ipad, na piakubadili comp za mac kuwa bora sana.
Baadhi ya mambo ya kufurahisha kuhusu Jobs.
1. Jama alikuwa ana patent kila kitu hata ubunifu mdogo, mfano stair case zilizoko kwenye ofisi za apple zilizo tengenezwa kwa kioo, alizipatent. Staircase hizi uwa zinawavutia watu kuingia kwenye maduka yao kununua bidhaa.
2. Alikuwa anaamini katikaa kufanya vitu kwa usafi na umakini. Alikuwa akisema haifai kufanya kitu ovyo ovyo kwakuwa hakitaonekana. Mfano kabati kwakuwa upande wa nyuma utakuwa umetazama ukuta hivyo hakuna atakayeuoana, eti ndo utumie mbao mbovu mbovu na usipige rangi. Jobs hakuwa mtu wa hivyo.
3. Alikuwa akiendesha gari lisilokuwa na plate namba. Jobs alikuwa akiendesha gari aina ya Mercedes-Benz SL55 AMG. Sheria ya California inamruhusu mnunuzi wa gari kutumia gari kwa miezi sita pasipo kupachika plate number. Jobs alitumia hii nafasi kuwa ananunua gari na kuliendesha kwamiezi sita kisha anauza na kununua gari lingine same model same color.
4. Aliunda timu ya wataalamu kufanya research juu ya shauku (emotions) pale ambapo mteja anapokuwa akifungua box la bidhaa aliyonunua anajisikiaje. Ndiyo maana matokeo ya utafiti wao yakapelekea apple kutumia utaalamu mwingi katika kupack bidhaa zao. Hata box lazima liwe zuri na mpangilio bora.
5. Alikuwa akivaa simple sana. Alipendelea kuvaa jeans za levis na tisheti zenye collar ndefu. Inasemekana alikuwa na jeans zaidi ya 100 za levis ana sneaker.
6. Alitaka kubadili dini ya kuwa Mbudha baada ya kutembelea India. Na hii ilibadili mtazamo wake maisha yake yote.
Jobs amekuwa inspiration kwa wavumbuzi wadogo duniani kote. Amebadili mambo mengi. Alikuwa pia anajua marketing sana jamaa. Presentations zake wakati wa kuintroduce bidhaa ilikuwa za kipekee, ambapo naona makampuni mengi sasa yanafuata style hiyo.