Kwa wanaonijua toka enzi za MBEYA day...
Au wakati bado mdogo MAMA aliponita MAY...
Miaka chini ya kumi tu nna jina Mtaani...
Kila mtu alinijua mimi, ni Mtoto wa nani...
Ni hivyo hivyo mpaka WALIMU Shuleni...
Na ndio maana mpaka leo mimi sishangai kuShine...
Nilipoanza MUZIKI, sikujua mafanikio yangeambatana na CHUKI...
Mara ngapi nakiukwa na nawaita MARAFIKI...
Sasa nalala macho, wanafiki siwataki...
Maana kila ninachofanya wanaonekana hawataki... "HAA"
Na sijali wanachosema...
BABA alinifundisha kutazama mbele DAIMA...
Na moto ni ule ule tu hakuna wa kuuzima...
Najua wanachotaka...
Kuona SUGU kachoka ili wapate kucheka...
Watasubiri watachoka...
Watapanda watashuka...
Mimi nabaki vile vile kila Siku kila Mwaka...
Na bado nawakilisha tu CHAMA la MADEIWAKA...
Mie ni Fighter naFight bila kuchoka...