Mambo Mabaya Ambayo Mkazo (Stress) Huyaleta katika Mwili Wako

Mambo Mabaya Ambayo Mkazo (Stress) Huyaleta katika Mwili Wako

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Mambo Mabaya Ambayo Mkazo (Stress) Hufanya kwa Mwili Wako:

Ni hatari kwa afya ya moyo! Kila kipindi ambacho mtu anakuwa na mkazo, homoni ya adrenalini hutokezwa ambayo huongeza mapigo ya moyo na shinikizo la damu.

Hufanya ngozi kuonekana mbaya! Watafiti wanadai mkazo huamsha matatizo kama chunusi, upara na kizema (mzio unaofanya ngozi kuvimba). Na ikiwa mtu ana matatizo haya toka mwanzo yanaweza kushamiri zaidi.

Huongeza hatari ya mtu kuugua! Tafiti moja ilidai watu walio na mkazo sugu wana hatari mara mbili ya kuugua mafua na kikohozi.

Ubongo na mfumo wa umeng'enyaji wa chakula wa mtu unaendeshwa na homoni zinazofanana sana. Ubongo ulio na mkazo wakati mwingine husababisha kiungulia, vyakula kutomeng'enywa vizuri, kuhara, kichefuchefu na kutapika.

Huharibu usingizi! Mkazo hufanya akili kukumbwa na wasiwasi mwingi. Mawazo mengi hufanya mtu akose usingizi. Na kukosa usingizi humfanya mtu awe na mkazo zaidi.

Nini Unaweza Fanya Kuepuka Mkazo (Stress)?
Madaktari wanasema ulaji chakula bora kiafya hasa matunda na mboga za majani husaidia sana. Pia, wanashauri kuushughulisha mwili kwa mazoezi na kusinzia angalau masaa 8 kila usiku.

Kupata usingizi wa kutosha angalau saa 7 hadi 8 wakati wa usiku husaidia mwili kupambana na mkazo (stress) na kuimarisha mifumo ya mwili.


Tiba Fasta
 
Back
Top Bottom