Mambo manne muhimu ya ufunguaji mlango aliyotaja Rais wa China kwenye CIIE yatanufaisha dunia

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,116
Reaction score
1,121
042234284m1o.jpg

Maonyesho ya Nne ya kimataifa ya Uagizaji Bidhaa China (CIIE) yamefunguliwa mjini Shanghai, tayari kwa mikusanyiko ya wanaviwanda, wafanyabiashara na wajasiriamali zaidi ya elfu tatu kutoka nchi 127 duniani. Maonyesho hayo ambayo ni ya nne kufanyika toka yalipoanza kufanyika mwaka 2018, ni mwendelezo wa juhudi za China kuchangia maendeleo yake na nchi nyingine duniani.

Kwenye hotuba ya ufunguzi wa maonyesho hayo iliyotolewa kwa njia ya video, Rais Xi Jinping wa China amekumbusha na kusisitiza kuwa China haitabadilisha dhamira yake ya kufungua mlango, na haitabadilisha nia yake ya kuchangia fursa za maendeleo yake kwa dunia, itaendelea kuhimiza mafungamano ya kiuchumi, na kuhakikisha uchumi wa dunia unakuwa wenye usawa, shirikishi na wenye manufaa kwa wote. Rais Xi amekumbusha kuwa China ikiwa ni nchi pekee kati ya nchi zenye uchumi mkubwa duniani kurekodi ongezeko chanya la biashara katika kipindi cha maambukizi ya COVID-19, imejitahidi kutoa mchango mkubwa katika kutuliza hali ya viwanda na biashara duniani.

Msisitizo wa ahadi ya Rais Xi Jinping kuhusu utayari wa China kuendelea kuwa wazi katika kuchangia fursa za maendeleo na nchi nyingine ni alama iliyo wazi ya China katika zama hii, na inatokana na kutambua kuwa China ikiwa ni nchi ya pili kwa nguvu ya uchumi duniani, ina wajibu na nafasi muhimu katika kuchochea maendeleo ya uchumi wa duniani. Ikumbukwe kuwa mbali na athari za janga la COVID-19 kwa uchumi wa dunia, kabla ya hapo dunia ilikuwa inakabiliana changamoto nyingine za kiuchumi zilizotokana na kuibuka vitendo vya kujilinda kibiashara, vilivyofafanya hali ya kufufuka kwa uchumi iwe kwenye hatihati.

Baadhi ya nchi za magharibi zilizokuwa vinara wa kanuni za biashara huria duniani, zilibadilika ghafla na kuanza kuweka vizuizi vya kibiashara kwa visingizio mbalimbali na kufanya ufufukaji wa uchumi uendelee kuwa na changamoto. Lakini tofauti na nchi hizi, China iliamua kuchukua hatua za kufungua mlango zaidi na kuruhusu bidhaa nyingi zaidi kutoka nchi zilizoendelea na zinazoendelea kuingia kwenye soko lake. Rais Xi amekumbusha kuwa China ina tabaka kubwa la watu wenye mapato ya kati ambao wanafikia milioni 400, na thamani ya uagizaji wa huduma na bidhaa kwa mwaka imefikia dola za kimarekani trilioni 2.5, hii ni fursa kubwa wa uchumi wa dunia.

Kwenye hotuba yake Rais Xi Jinping ametoa mifano ya mambo ambayo yanaendelea kufanywa na China kufungua zaidi soko lake. Kwa mfano katika kipindi cha miongo miwili iliyopita tangu China ijiunge na shirika la biashara duniani (WTO) kiwango cha kodi kimepungua kutoka asilimia 15.3 hadi asilimia 7.4, na serikali imepitia upya na kuzifanyia marekebisho sheria 2300, hali ambayo imeweka urahisi mkubwa kwa wawekezaji kutoka nje kufanya uwekezaji na biashara zao nchini China.

Kwenye hotuba yake Rais Xi pia amesisitiza kuwa China itaendelea kufungua maeneo zaidi ya mfano ya kuhimiza uagizaji wa bidhaa, na kurahisisha utaratibu wa biashara ya kwa njia ya mtandao wa Internet ya kuvuka mpaka. Wizara ya biashara ya China imesema China kwa sasa ni nchi ya pili kwa uagizaji wa bidhaa duniani kwa mwaka wa 11 mfululizo, Rais Xi amesema China itafanya juhudi zaidi ili kuongeza uagizaji wa bidhaa kutoka nje.
 
Mungu ajaalie tz yangu siku moja iwe km china
 
Back
Top Bottom