Aliko Musa
JF-Expert Member
- Aug 25, 2018
- 209
- 315
Kanuni mama ya uwekezaji kwenye viwanja na nyumba ni kutengeneza fedha wakati wa kununua nyumba. Kanuni hii inamhusu mwekezaji yeyote anayewekeza kwenye viwanja na nyumba.
Kwa kutumia mbinu yoyote ya uwekezaji huu na kwa wakati wowote unatakiwa kutengeneza fedha wakati wa kununua nyumba.
Kwangu mimi nyumba ya kuishi sio aseti, hivyo unaweza kuachana na somo hili maana halitakusaidia chochote kuhusu nyumba yako ya kuishi unayotaka kununua.
Lengo la maisha yangu ni kuwasaidia wawekezaji kwenye viwanja na nyumba kujenga utajiri mkubwa wanaotegemea kuwa nao.
Kwa lengo hili la maisha yangu, sitegemei kuwasaida wanaotaka kumiliki nyumba za kuishi tu. Badala yake ninaweza kuwasaida wanaotaka kumiliki nyumba kwa ajili ya kuishi na kupangisha.
Kanuni ya kutengeneza fedha wakati wa kununua nyumba ya kupangisha ndiyo inayobeba ujumbe wa somo hili.
Je utawezaje kutengeneza fedha wakati wa kununua nyumba yako ya kupangisha?.
Kiasi Cha Fedha Unachotakiwa Kutengeneza.
Kiasi kinachopendekezwa kutengenezwa wakati wa kununua nyumba ni 10% au zaidi.
Ni kosa la kiuwekezaji kutotengeneza fedha wakati wa kununua nyumba. Ni rahisi kutengeneza fedha wakati wa kununua nyumba kutoka kwa wauzaji waliohamasika.
Makundi ya wauzaji wa nyumba waliohamasika ni kama ifuatavyo;-
✓ Wanandoa waliotalakiana.
✓ Waajiriwa waliohamishwa vituo vyao vya kazi.
✓ Wawekezaji walioshindwa kukamilisha marejesho ya mikopo kutoka vyanzo vya fedha.
✓ Watu waliofiwa na watu wao wa karibu.
✓ Wamiliki wa nyumba waliorithi nyumba zao za kupangisha.
✓ Wamiliki wa nyumba wenye kesi mahakamani.
✓ Wamiliki wa nyumba waliosomewa hukumu za kifungo magerezani.
Kuna makundi tofauti tofauti ya wauzaji wa nyumba za kupangisha waliohamasika. Kazi kwako kuwatambua wauzaji waliohamasika.
Unaponunua kutoka kwa wauzaji waliohamasika sio kwamba unafurahia chanagamoto zao za maisha. Badala yake unawapa suluhisho la chanagamoto zao.
Pia, ni kosa na kosa kubwa kutumia nafasi ya kunyanyasa wauzaji waliohamasika kutokana na chanagamoto zao.
Unapofanya hivyo unajiharibia jina lako la utoaji wa huduma za uwekezaji kwenye ardhi na majengo.
Mambo 5 Ya Kuzingatia Wakati Kuomba Punguzo La Bei.
Moja.
Ofa Ya Punguzo La Bei.
Ikiwa muuzaji wa nyumba ameweka ofa kubwa kiasi kwamba bei ya kuuzia inakuwa chini kwa zaidi ya 10% ya bei ya sokoni sio lazima uanze kuomba punguzo zaidi.
Unachotakiwa kufahamu ni kutathimini kati ya bei ya kuuzia na bei ya sokoni ya nyumba husika.
Mbili.
Jumla Ya Gharama Za Ukarabati Zinazohitajika.
Hapa unatakiwa kupata makadirio ya ujumla ya gharama za ukarabati. Kisha unatumia makadirio hayo kuomba punguzo la bei.
Kwenye makadirio ya gharama za ukarabati unatakiwa kujumlisha na jumla ya gharama za fundi wa kukarabati nyumba.
Mfano; endapo umepata jumla ya gharama za ukarabati kuwa ni shilingi milioni mbili (tshs.2,000,000). Baada ya hapo kitumie kiasi hiki kuomba punguzo la bei.
Kwa kawaida unatakiwa kuomba punguzo la Tshs.2,000,000 au zaidi. Wakati unaomba punguzo la bei unatakiwa kuianisha gharama zote zinapelekea jumla ya kiasi hiki.
Kuomba punguzo kwa kuonyesha sababu ndiyo njia bora ya kumshawishi muuzaji kuliko kumpa maneno matupu yasiyokuwa na sababu za kiuwekezaji.
Tatu.
Kiasi Cha Kipato Endelevu Cha Kila Mwezi.
Nyumba ambayo inaingiza zaidi ya 2% ya kodi ya nyumba kila mwezi ya bei ya nyumba ni nyumba nzuri hata kama inauzwa bila punguzo la bei.
Njia nyingine ya kupima unafuu wa bei ya nyumba za kupangisha ni kutumia kanuni hii ya 2% ya nyumba za kupangisha.
Kwa lugha nyingine nyumba ambayo bei yake ni 2% ya kodi ya nyumba ya kila mwezi, nyumba hiyo huuzwa kwa bei nafuu.
Mfano; nyumba ya thamani ya milioni ishirini (tshs.20,000,000) inatakiwa kupangishwa kwa shilingi laki nne (400,000) kila mwezi.
Hiyo laki nne ni kipato ghafi. Laki nne ni kipato kabla ya kutoa gharama zote za ukarabati wa nyumba.
Kipato halisi (net rental income) baada ya kutoa jumla ya gharama za ukarabati na gharama za usimamizi wa nyumba kinatakiwa kiwe 1% au zaidi ya thamani ya nyumba kila mwezi.
Nne.
Ukuaji wa Ongezeko La Thamani.
Sehemu ambazo nyumba huongezeka thamani kwa zaidi ya 7% ya bei ya nyumba kila mwaka, zinafaa zaidi kuwekeza kwenye nyumba hizo. Kwenye maeneo haya hata ukinunua nyumba kwa bei ya sokoni haina shida yoyote.
Pia, kiwango ambacho ninawapendekezea wawekezaji kumiliki nyumba zinazoongeza thamani kwa 10% ya bei ya nyumba kila mwaka.
Pia, sehemu ambazo ardhi hupanda thamani kwa zaidi ya 100% kila mwaka ni nzuri sana kwa ajili ya uwekezaji.
Hivyo maeneo yenye sifa hizi, hutakiwi kunga'ang'ania kupata punguzo la bei la bei. Hii ni kwa sababu upandaji wa thamani hufidia fedha unayotakiwa kutengeneza wakati wa kununua nyumba ya kupangisha.
Lakini ni rahisi sana kununua kwa punguzo la bei la zaidi ya 10% ya bei halisi ya nyumba kutoka kwa wauzaji waliohamasika.
Tano.
Fedha Inayotengenezwa Kabla Ya Mazungumzo.
Kuna nyumba ambazo zinauzwa kwa bei pungufu kabla hata hujaomba punguzo la bei.
Kama nyumba inauzwa kwa punguzo la bei la zaidi ya 10% ya bei ya sokoni na nyumba hiyo ina sifa zote nilizoeleza hapo juu.
Hutakiwi kutumia muda na maneno mengi kuomba punguzo la bei ya kununulia nyumba ya kupangisha.
Mambo yote haya yatakusaidia kufanya maamuzi sahihi ya jinsi ya kutengeneza fedha wakati wa kununua nyumba ya kupangisha.
Nipigie simu kupitia namba 0752 413 711 ili upate maelezo zaidi kuhusu somo hili katika kipengele ambacho unahitaji maelezo ya ziada.
Rafiki yako,
Aliko Musa.
WhatsApp: +255 752 413 711