Mambo matano ya kutia moyo kwenye tukio la muuaji Hamza

Mambo matano ya kutia moyo kwenye tukio la muuaji Hamza

kifupi kirefu

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2018
Posts
539
Reaction score
3,507
1. Polisi wamefika eneo la tukio kwa wakati na kupambana kiume. Hongereni Sana.

2. Wananchi kwa umoja wao wamezuia baadhi ya watu kutofika eneo la tukio yakiwemo magari, may be wasingewazuia waendesha magari madhara yangekuwa makubwa zaidi ikiwemo kukutana na risasi.

3. Clip zinaonyesha wananchi wamezuia polisi kushambuliana, hii ilitokea wakati wa Westgate.

4. Wananchi pamoja na kuwa kwenye hatari wametumia technology kuweka kumbukumbu. Wamekuwa waandishi wa habari, hii hali ikiendelea kwenye jamii uhalifu utakuwa unarekodiwa na ushahidi kupatikana.

5. Wananchi wamemtambua muuaji kabla ya dola na hivyo kusaidia kupatikana kwa taarifa zake,naamini itasaidia sana uchunguzi huko mbele hasa kuhusu tabia za muhusika na Kama ana watu wengine wa kariba yake.

Ushauri
Tutumie utaratibu uliotumiwa na Kenya wa kuwa na kikosi kimoja Cha kupambana na Ugaidi kinachoundwa na vyombo vyote na chenye commanding system moja.

Nakumbuka Bunge la Kenya lilipofanya tathimini ya athari za tukio la Westgate walibaini askari walipotea kwa sababu walirespond at a time lakini wakiwa na uniforms mbalimbali na wakiwa na viongozi tofauti, kila kikosi kikawa kinajifanyia kinavyoona na kufanya washambuliane ndani.

Kongole kwa jeshi la Polisi.
 
Tutumie utaratibu uliotumiwa na Kenya wa kuwa na kikosi kimoja Cha kupambana na Ugaidi kinachoundwa na vyombo vyote na chenye commanding system moja. Nakumbuka Bunge la Kenya lilipofanya tathimini ya athari za tukio la Westgate walibaini askari walipotea kwa sababu walirespond at a time lakini wakiwa na uniforms mbalimbali na wakiwa na viongozi tofauti, kila kikosi kikawa kinajifanyia kinavyoona na kufanya washambuliane ndani.
Sasa huoni hapa pekee tofauti iliyopo katika muundo wa jeshi la polisi la Kenya na Tanzania? Au ushauri wako ni kutaka Tanzania iige tu kwa vile Kenya walifanya!

Ukichukua mfano wa 'Westgate', halafu ufananishe na hili tukio la mtu mmoja (at least kwa sasa, bado inajulikana ni 'lone ranger', halafu ufananishe na tukio lililopangwa na kundi la watu, bado unaonyesha kwamba matukio haya huyaelewi vizuri.
 
Raia wamefanya mambo out of ignorance, wangekuwa wanajua athari za kuwa eneo lile tena wamesimama wangesaidia zaidi polisi wetu. Mtu anaona mtu anapiga risasi na bado amesimama wima wima.

Kurekodi ni 50/50 na ni hatari bado sio swala la kuhimiza, raia anatakiwa kutawanyika kutoka eneo la tukio, sio kuzagaa zagaa. Pale jamaa angewageukia saizi tungeongea na kushauri tofauti na uzi wako.

Silaha ya moto sio kitu chakucheza nacho hata kidogo.
 
Ni jambo la kheri sana hawa Polisi wanaoitumikia CCM badala ya wananchi kuendelea kuuawa.Mungu bariki sana yule gaidi.

8860003675.jpg
 
Mi nimeoana jinsi social media ilivyoiacha mbali traditional media.

Nimefurahia ujasiri wa yule askari aliyekuwa mlangoni kwenye mlango wa ubalozi wa Ufaransa.

Mwisho nimpongeze bwana Hamza kwa kutodhuru wananchi japo alikuwa na nafasi kubwa ya kufanya hivyo na mtu kwenye position desperate kama aliyokuwanayo angeweza fanya hivyo.
 
Swali kujiuliza kwanini polisi walikuwa wanataka washambuliane? Je inawezekana jamaa hakuwa mhalifu ndio maana askari mwenzao akawa anazuia wenzake wasimuue? Na wakati huo huo wenzao wanataka kuondoa ushahidi?

Maana kama jamaa alikuwa ni muuaji mbona hajashambulia raia yoyote, maana yake ni kwamba kuna kitu kilikuwa kinaendelea kati ya askari na jamaa.

Hii inanifanya nikubaliane na wale wanao sema hii Zombe style, kama ni Zombe style askari wanatakiwa wawe jela na sio kupongezwa kwa mauuaji kwa mtu asiyekuwa na hatia.
 
Polisi wana special unit ya kupambana na ugaidi na uhalifu inayoitwa CRT (Crisis Response Team) Kama ilivyo RECE Squad ya Kenya, e.t.c
Hate versus Police ni kubwa sana kutokana na dhuluma zao na kubambikiza wananchi makosa, jokes aside unahitaji kuwa na ngozi ya mamba kuwaonea huruma Polisi

Jana kwenye hotuba ya Kikao Kazi na TANPOL Rais SSH ameongea mambo yanayuhusu dhuluma na unyanyasaji wa Polisi. Kuna aya kama 3 amerudia Rais kuhusu upelelezi usiokamilika na watu kukamatwa.
 
Mtu mmoj anataka achote mawazo ya wananchi kwamba hawawapendi polisi.

Kisa bana ake yuko ndani, haiwezekani.
 
Nilitegemea ungeshauri polisi wafanye kazi waache dhuluma.

Maana jamaa anaonekana ni mtu na shughuli zake na anaheshimika mpaka kuwa kwenye kamati kuu ya CCM ilala, mfanyabiasha mwenye migodi.

Mi naona kuwaua ha watatu na kujeruhi sita kawaonea huruma ila ilitakiwa kupiga kituo kizima.

Polisi wanabambikiza kesi, wanadhulumu, badala ya kusimama na raia wao kutwa kuwasaidia CCM kuzidi kutawala.

Polisi wasipobadilika yatakuja maafa makubwa zaidi ya haya ni suala la muda.
 
Back
Top Bottom