SoC04 Mambo matatu yatakayoibadili Tanzania na kupata ndani ya miaka 10 Tanzania niitakayo

SoC04 Mambo matatu yatakayoibadili Tanzania na kupata ndani ya miaka 10 Tanzania niitakayo

Tanzania Tuitakayo competition threads

kandamba

New Member
Joined
Oct 21, 2016
Posts
3
Reaction score
4
MAMABO MATATU MATATU YATAKOIBADILI TANZANIA NA KUPATA NDANI YA MIAKA 10 TU TANZANIA NITAKAYO.

Tanzania ni nchi tajiri ambayo inapsawa kuwa mbali sana kiuchumi na kuiingiza kwenye nchi tajiri duniani. Miongoni mwa mambo matatu ambayo tunapaswa kuyazingatia ili kupata maendeleo ni, Moja kuwekeza kwenye matumizi ya gesi asilia ambayo mwenyezi Mungu ametupatia katika mikoa ya Mtwara na Lindi, Pili matumiazi ya tehema katika sekta zote na jambo la tatu ni kuondokana na matumizi ya pesa tasilimu (Cash Economy) ili kufanya malipo kwa yote kupitia krediti kadi ili miamala yote isome kwenye mifumo.

Nianze na hoja ya kwanza ya matumizi ya gesi asilia, Kupitia mikoa ya Lindi na Mtwara nchi yetu imebahatika kupata gesi ya kutosha ya kuwezesha kuinua uchumi. Gesi hiyo asilia kwa asilimia 99 inatumika kuzalisha umeme ambao unatumika viwandani na majumbani. Aidha, viwanda vichache nchini vimeanza kunufaika na gesi asilia na watumiaji wa majumbani ni wachache hasa maeneo ya mikocheni. Gharama ya umeme asili ni ndogo kwa hiyo endapo wananchi wengi wangepata huduma hiyo ingeweza kuiniua uchumi wetu .

Pia, gesi asili inafaa kutumika kuendesha vyombo vya usafiri kama magari ya watu binafsi, mabasi ya habiri, bajaji na pikpiki. Watumiaji wa vyombo vya usafiri ni watanzania wa kawaida. Kwa hiyo kama mifumo ya kubadili teknolojia kutoka kutumia diezeli au petrol kwenda mfumo wa gesi asilia tungeleta mapinduzi makubwa ya kiuchumi ya nchi yetu. Aidha, huduma ya gesi asilia kwa nchi yetu kwa vyombo vya usafiri ipo Dar es salaam pekee na vituo ni viwili tu Ubungo na Tazara jambo ambalo linasababisha usumbufu mkubwa kwa wahitaji. Pia, Chuo cha Teknolojia cha Dar es salaam (DIT) ni kituo pekee chenye uwezo wa kuunga mfumo wa gesi asilia kwenye vyambo vya usafiri nilivyotaja hapo juu.

Jamba la kushangaza ni kwamba kwa nini gesi asilia haijasambazwa na mikoa mingine ili watanzania wengi waweze kunufaika na mali hiyo asili na kupunguza makali ya maisha. Nilitarajia serikali, sekta binafsi zijikite katika kuwekeza kwenye gesi asilia ili kuisaidia nchi kupunguza matumizi ya fedha za kigeni kununua mafuta (Diesel na Petrol) kutoka nchi za nje.

Jambo ambalo kila Mtanzania anatakiwa kujiuliza kwa nini serikali yetu, wanasiasa hususani wabunge wamekaa kimya juu ya kuhimiza serikali na sekta binafsi kuwekeza kwenye gesi asilia. Pia, inatia shaka kwamba labda watunga sera ndio wanamiliki vituo vya nishati ya mafuta ya vya Dizeli na Petrol ambavyo wanamaslahi navyo kusuasua kuwekeza kwenye gesi asilia. Hoja nyingine ni kwa nini nchi yetu inaendelea kuagiza mafuta nje ya nchi badala ya kuwekeza kwenye gesi asilia na kutumika kwenye vyombo vya usafirishaji na kuendesha mitambo yetu nchini, hii ingeondoa malalamiko ya kupanda bei ya mafuta mara kwa mara yanayotoka nje ya nchi.

Kutokana na uchambuzi huu hapo juu nashauri serikali ifanye maamuzi mazito kwa kushirikisha sekta binafsi kuhakikisha gesi asilia inatumika nchi nzima kwa kutoa ruzuku kwa Chuo cha Teknolojia Dar es salaam ili gharama za kuunda mfumo wa gesi asilia kwenye vyombo usafiri upungue na kuwawezesha watanzania wengi kulipia na kuutumia, DIT wapeleke taalumu hii kwenye vyuo vingine vya ufundi nchi ili watanzania wa mkioani waweze kutumia, vituo vya gesi asilia vijengwe nchi nzima kwa kuanza, wajenge kwenye barabara kuu nchi ili vyombo vya usafiri vipate huduma hii. Ajenda ya kutumia gesi asilia iende sambamba na kampeni ya kuepuka matumizi ya mkaa inayoendelea nchi.

Hoja ya pili ni kwamba uwekezaji kwenye technolojia na tehama kutailetea Tanzania madiliko makubwa kwa miaka 10 ijayo. Tanzania ni moja nnchi ambayo ianaendelea kiuchumi lakini kama hatutawekeza kwenye technolojia na tehama bado maendeleo yetu yataendelea kuwa nyuma. Tanzania ina rasilimali za kutosha katika nyanja za kilimo, utalii, bandari, nyanzo vya maji, ardhi, Wanyama pori, misitu nk. Pamoja na nchi kuendelea kuvuna na kutumia rasilimali hizo lakini taasisi zetu bado hazijatufikisha watanzania tunakotaka na kutuleta maendeleo.

Changamoto zinazoikabili nchi yetu ni pamoja kuwepo kwa vitendo ubadhirifu wa mali za umma, uzembe, kukosekana kwa uadilifu katika kusimamia mali za umma nk. Changamoto hizo ndizo kwa njia moja au nyingine zimesababisha nchi yetu kuendelea kuwa masikini pamoja na utajiri uliopo.

Njia moja wapo kwa nchi yetu ni kuwekeza kwenye technolojia za kisasa na Tehama ambazo zitasaidia kupunguza urasimu katika kutoa huduma, kuzalisha mali na kudhibiti wale ambao wamekuwa wakifanya ubadhirifu wa mali za umma. Serikali iamuru taasisi zote ziakishe zinawatua wataalamu wa Tehama kutengeneza mifumo ya udhibi wa mali za umma katika maeneo ya kazi na kuzisimamia.

Uwepo wa mifumo ya kisasa ya kiteknolojia na matumizi ya Tehama yatasaidia kuwalazimisha watumishi wa umma kuwa waadilifu. Uadilifu ni hulka ya mtu na hautokani na kufundishwa darasani. Kwa hiyo ili kuwabana wale ambao si waadilifu matumizi ya mifumo ya Tehama ya udhibiti itasaidia kwani mifumo hiyo inaleta uwazi na ni rahisi kufanya usimamiaji. Pia, maeneo yote ya uzalishaji na kutolea huduma za umma na sekta binafsi lazima zifungwe CCTV Kamera na mitambo mingine ya kuweza kungamua na kutunza matukio mbalimbali yanayotokea ili kupata ushahidi pale inapojitokeza matukio ambayo si ya kawaida.

Hoja ya tatu ni Tanzania kuondokana na uchumi matumizi ya fedha taslimu (Cash Economy) kutatuletea Tanzania tuipendayo kwa miaka kumi ijayo. Miongoni mwa mambo ambayo yamekuwa yakichelesha kukuwa kwa uchumi wa Taifa la Tanzania ni matumizi makubwa ya fedha taslimu katika kufanya manunuzi. Watanzania wamekuwa na tabia ya kupenda kutembea na pesa taslimu badala ya kubadilika na kutumia kadi za kufanyia miamala (Credit Card). Matumizi ya fedha taslimu yamekuwa yakisababisha serikali kushindwa kujua hasa mzunguko wa fedha upoje kwa malengo mapana ya nchi.

Matumizi ya fedha taslimu yamechangia kiasi kiasi kikubwa kuikosesha serikali mapato hususani yanayotokana na kodi. Matumizi ya fedha taslimu yamekuwa yakitoa mwanya kwa wafanyabiashara kutokutoa risiti ili pesa zisionekane kwenye miamala wanayofanya. Matokea yake wafanyabiashara wamekuwa wakitumia mwanya huo kuikosesha serikali mapato yake. Nashauri nchi lazima itengeza sera ya kuondokana na matumizi ya fedha taslimu ili kupata mapato halisi ya serikali kuisaidia nchi kukusanya kodi. Nchi ambayo haikusanyi kodi haiwezi kupata maendeleo. (No Tax No Development).

Nihitimishe kwa kusema kwamba iwapo mapoha ya matatu yatazingatiwa nan chi yetu ndani ya miaka kumi tutaipata Tanzania tupendayo.

Imeandaliwa na,

Email. gobagoba2001@gmail.com

Simu. 0755 650 221
 
Upvote 7
Back
Top Bottom