Mambo mazito, Mawakili wa Thabo Bester wajitoa kwenye kesi

Mambo mazito, Mawakili wa Thabo Bester wajitoa kwenye kesi

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
1682160610922.png
Mawakili wanaosimamia kesi ya Thabo Bester wamemtaarifu mteja wao kujitoa katika kesi inayomkabili huku ikielezwa huenda akawatumia mawakili waliokuwa wanamtetea Dr Nandipha Magudumana.

Hatua hiyo inamfanya Thabo kuanza kutafuta mawakili wengine baada ya Mawakili hao wa Ishmail kumtaarifu kujitoa.

Mei 16, 2023 mtuhumiwa huyo anatarajiwa kurejeshwa mahakamani ambapo atalazimika kuwatumia mawakili wengine katika kesi inayomkabili.

Wiki iliyopita mahakamani hapo mtuhumiwa huyo alimwomba wakili wake waieleze mahakama kuhusu hofu yake ya kula chakula kwa madai ya kuwekewa sumu kwa ajili ya usalama wake kiafya huku akihoji uvunjwaji wa sheria walivyomrudisha kutoka Tanzania.

Chanzo kimoja kimeeleza kwamba huenda mawakili hao wameamua kujitoa kwa sababu ya ugumu wa kesi kwani mteja wao tayari alikuwa anatumikia adhabu ya kifungo na kinachoonekana huenda akakabiliwa na adhabu zaidi ya kifungo kutokana na kutoroka gerezani.

Ikumbukwe Thabo Bester na mpenzi wake Dk Nandipha Magudumana walikamatwa Aprili 7 na Polisi wa Tanzania kwa ushirikiano na Jeshi la Polisi la Afrika Kusini na Jeshi la Polisi la kimataifa (Interpol).

Pia, Serikali ya Afrika Kusini ilitumia kiasi cha Sh175 milioni (R1.4 milioni) ili kukodi ndege kwa ajili ya kuwarejesha Thabo Bester na mpenzi wake Dk Nandipha waliokamatwa jijini Arusha.

MWANANCHI
 
Ndio nauliza anakuwa amefuata penzi au nayeye anakuwa na element za ujambazi?au anakuwa kapenda boga na ua lake?
ukichunguza sana hawa mademu wazuri wanaoolewa na majambazi na wahalifu wengine na wao huwa wako hivyo hata kama wana sura nzuri na ni warembo. Hapa hapa bongo kuna warembo wazuri lakini ni wavuta bangi
 
Ndio nauliza anakuwa amefuata penzi au nayeye anakuwa na element za ujambazi?au anakuwa kapenda boga na ua lake?
Lavishly life, si unajua hawana bajeti hao za kujibanabana km sisi tia maji pangu pakavu.
 
Back
Top Bottom