Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
MAMBO MENGI NI YAKAWAIDA ILA WAMEYA- OVERRATED NA KUWAFANYA WATU DHAIFU KUYAOGOPA ISIVYOSTAHILI. USIWE DHAIFU.
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.
Kama ni msomaji wa makala zangu utagundua kuwa moja ya mambo ninayoyarudia ni pamoja na suala hili la uongo wa makusudi unaovumishwa ili kuathiri vijana na jamii kwa ujumla. Kama ujuavyo sisi Watibeli uongo ni adui kwa sababu ni upotoshaji. Uongo huleta uoga. Na uoga huleta dhulma na uonevu kinyume na Haki.
Uoga kwa kiwango kikubwa huchangiwa na uongo, ulaghai, kuogopa vitu kinyume na uhalisia/ukweli.
Ninaamini yapo mambo mengi ambayo umekutana nayo na kuyaona ambayo uliambiwa ni magumu, na wapo waliya-ovarrate lakini ulipokutana na kuyafanya mwenyewe ukaona ni kawaida sana.
Katika michezo, juzi tuliona Watu wakipiga kelele kuhusu timu ya Mamelody ya Afrika ya kusini kuwa itaipiga Timu ya Yanga mabao mengi. Mamelody ilikuzwa tofauti na uhalisia. Haikuwa na maajabu yoyote ya kutisha kama ilivyosifiwa.
Halikadhalika na timu ya Al ahly NI timu za kawaida ila zipo OVERRATED.
Timu za mataifa ya kiarabu kwenye Afcon tuliona. Ni timu za kawaida ingawaje miaka mingi zilikuwa OVERRATED.
Wazungu pia walikuwa OVERRATED kabla ya Vita ya Kwanza na ya pili ya dunia. Uongo na uzushi ulichagiza propaganda ya kuwa-overrate hao wazuñgu. Ilifikia hatua mpaka ikasemwa wazungu Hawafi. Lakini kwenye vita ya kwanza na ya pili, wale waafrika walioshiriki hiyo vita wakabadilisha mtazamo kuwa kumbe waliwa-ovarrate, na kumbe ni binadamu wa kawaida wanakufa kama wanadamu wengine.
Usipende maneno ya kuambiwa bila kushuhudia na kuthibitisha mwenyewe.
Kumu-overrate mtu ni kumfanya kuwabora kuliko wengine jambo ambalo sio kweli.
Mtu anayeli-overrate jambo lolote mbele yako hujaribu kukudharau na kukudunisha kuwa hauwezi, anajaribu kukútishia na kukukàtisha tamaa kabla haujaanza ili ushindwe. Usikubali kuyasikiliza maneno yao.
Nyakati tunasoma, zipo shule zilikuwa OVERRATED na wanafunzi wao walionekana ni bora. Lakini kwenye uhalisia jambo hilo halipo.
Chuo cha Udsm ni moja ya vyuo ambavyo vipo OVERRATED Hapa nchini lakini kwa tuliosoma humo ni chuo cha kawaida mno. Na wanafunzi wake ni walewale kama wanafunzi wa vyuo vingine.
Taifa la ISRAEL kwa miaka mingi tumekuwa tukisikia ni moja ya taifa lenye nguvu za maajabu mno. Lakini ukifuatilia Uhalisia wake utagundua kuwa hakuna la ziada. Ni kama mataifa mengine tuu.
Tumeona vita yao na Hammas jinsi inavyodhihirisha UKWELI wa mambo.
Ukweli ni rafiki. Ukweli hautishi. Ukweli hauogopeshi. Ukweli ni rafiki wa kweli.
Ukiwa unafanya jambo lolote, hakikisha mtazamo na fikra zako ziwe chanya na sahihi katika jambo hilo. Usiogope. Usijidanganye wala usikubali kuogopeshwa na kudanganywa.
Fanya biashara ujionee mwenyewe, sio ngumu.
Kuwa Daktari, sio mgumu.
Unaweza kuwa vile utakavyo.
Taikon Master nimemaliza. Acha Nipumzike sasa.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam