Mambo mengine yabaki kuwa masuala mtambuka, si lazima kuwekwa kwenye mtaala

Lanlady

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2019
Posts
1,836
Reaction score
6,303
Kumekuwa na wanaharakati wengi sana wa masuala mbalimbali ya kijamii, ambao wamekuwa wakitamani kile wanachokitetea au kuelimisha kiwekwe kwenye mitaala ya elimu.

Binafsi nadhani si kila kitu lazima kiwekwe kwenye mtaala. Wanafunzi wana mambo mengi sana ya kujifunza ili waweze kujitegemea na kujiajiri baada ya kuhitimu.

Masuala mengine yawekwe hata kwenye vipeperushi au yafundishwe kama masuala mtambuka kutegemea na mazingira husika
 
Nilitamani watoto wafundishwe kuuwajibikia muda bila kufegemea kengele mashuleni!
 
Tutaweka tu si tunategemea misaada tutafanyaje
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…