Mambo muhimu anayopaswa kuzingatia kijana katika maisha yake

Mambo muhimu anayopaswa kuzingatia kijana katika maisha yake

Showio

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2019
Posts
254
Reaction score
481
Naam! Nawaletea neno la siku; tupo likizo kidogo.

1. KUWA NA MARAFIKI AMBAO WANA FAIDA KATIKA MAISHA YAKO: Unaweza kuta mtu katika simu yake ana marafiki zaidi ya 200 lakini hawa wote anapopata tatizo au shida akianza kuomba msaada katika hao marafiki hata shilingi laki 5 haifiki, sasa kuna haja gani ya kuwa na marafiki wasio na faida. Tafuta marafiki wanaofurahia uwepo wako na kuwa nao katika shida na raha.

2. ISHI KUTOKANA NA UWEZO WAKO: Maisha tunatofautiana kuna anayepata shilingi 100 na anayepata elfu moja , wewe kama unapata shilingi mia ishi maisha yale yanayoendana hiyo shilingi mia hadi pale utakapofanikiwa kupata shilingi elfu moja ndio uishi maisha ya shilingi elfu moja . Masuala ya kuiga maisha utaumbuka

3. NIDHAMU YAKO YA FEDHA: Hapa namaanisha matumizi yako kwa pesa unayoipata, jitahidi sana kupunguza matumizi yasiyo na lazima katika fedha uzipatazo , maana ukiendekeza matumizi yasiyo muhimu utakuwa unaonakila siku kuwa fedha haitoshi hata kama utakuwa unaingiza milioni 1 kwa siku.

4. HESHIMU KILA MTU: Asikudanganye mtu heshima ndio kila, iwe kwa mkubwa hata mdogo. Usomi wako au uzuri wako usikufanye ukawa na dharau na kutowaheshimu wengine maana katika dunia kuna mambo mengi sana, yule ambaye haumuheshimu leo kesho ndio anaweza kuwa msaada wako mkubwa katika maisha yako

5. JITAHIDI KUTIMIZA MALENGO: Watu wengi sana wanaweka malengo ila tatizo sasa linakuja katika kuyatimiza hayo malengo , kila siku hakosi sababu . Utasikia mara ooh nilitaka fanya hili ikawa hivi hadi miaka inaisha huyu mtu hajatimiza malengo aliyopanga miaka 10 . Kila mwaka weka malengo halafu kabla mwaka haujaisha jitahidi hayo malengo uwe umeyatimiza japo robo 3 yake ndio mwanzo wa mafanikio

6. JITAHIDI KUWA NA FURAHA MUDA MWINGI: Usipende kuruhusu moyo wako ukawa na hasira sana , jenga kuwa na furaha muda mwingi haijalishi hauna fedha au una fedha maana wewe ndio kiongozi wa maisha yako. Ukiruhusu huzuni itawale maisha yako utakuwa na huzuni kila siku hata kama utakuwa na fedha vipi . Hata kama ukikosa fedha tafuta tena huku ukiwa na furaha maana mawazo yanaua.
 
Kiukweli umeongea points za nguvu sana kuhusu vijana na siyo vijana pekee, hata watu wa makamo huu ujumbe unawahusu.
 
Kiukweli umeongea points za nguvu sana kuhusu vijana na siyo vijana pekee, hata watu wa makamo huu ujumbe unawahusu.
Asante sana huu ni ujumbe kwa watu warika zote
 
Back
Top Bottom