Mambo niliyojifunza vita vya Urusi katika maisha ya kawaida

matunduizi

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2018
Posts
7,968
Reaction score
19,368
1: Kabla sijaanzisha vita na mtu lazima nijue nani yuko nyuma yake.

2: Ukiwa huna nguvu sana jitahidi kushambulia mahala ambapo pataleta matokeo makubwa kwako na maumivu makubwa kwa adui kwa kutumia rasilimali chache. Ukraine wanapukutisha majenerali wa Kirusi.

3: Ukiamua kuingia vitani pigana. Iite vita. Usiseme najaribu maisha pambana. Russia wanapata hasara za kivita huku wanaiita Operation.

4: Sio kila vita upigane. Nyingine tafuta mjingamnjinga apigane kwa niaba yako bila wewe kuathilika moja kwa moja. Ukraine anatumiwa na US na NATO.

5: Ukiamua kuingia kwenye mapambano, usiongee sana. Tenda zaidi. Warusi hawaongei sana.

6: Usijiingize kwenye ugomvi wa watu usiojua wanagombania nini. Unapoteza nguvu na muda kijinga. Fanya yako. Hata Mkuu wa Usalama wa taifa wa ufaransa alishtumiwa kwa kutojua kinachogombaniwa huko. Wewe wa Legangabilili unakomaa utadhani in CEO wa FSB.

7: Ukitaka kuua tatizo au kuleta tatizo tumia vyombo vya habari. Vita hivi vyombo vya habari vimeishabikia na sasa Covid imekufa. Ukitaka kufanikiwa haraka tumia media zikunufaishe.
 
Sisi jumuiya ya Warusi waliopo katika mikoa mbali mbali tunasema Putin piga hao ng'ombe wa Ukraine 🐒
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…