Mambo niliyojionea Hospitali ya Magunga wilayani Korogwe

Mambo niliyojionea Hospitali ya Magunga wilayani Korogwe

Kajeku

New Member
Joined
Feb 19, 2023
Posts
2
Reaction score
1
Tukiacha Yale mambo ya ujumla kama vile uhaba wa madaktari, dawa , vifaa n.k yafuatayo ni mambo nimejionea wakati namuuguza mdogo wangu aliyevunjika mguu

1. Vyoo vya wodini havina Maji

Yaani ni mpaka unashangaa kama upo hospitali ya Wilaya au zahanat ya Kijiji. Kama una mgonjwa inabidi uwe na ndoo na ukatafute Maji nje.. lakini hili linapelekea harufu kali wodini na uchafu chooni.

2. Kupata huduma weekend na wakati wa jioni ni changamoto..

Ni kama Magunga hospital wamekubaliana kwamba hakuna kuumwa wakati wa jioni au au siku za weekend!! Unaweza kuhangaika kutafuta daktari usimuone!

3. Mfumo wa mtandao kugawa dawa kwa baadhi ya manesi ni changamoto

Kuna mmoja alikuwa anagawa dawa hata kushika mouse inamsumbua! Mpaka unajiuliza nani kamuweka dukani!! Yaani watu wawili mnaweza kukaa masaa mawili au matatu kwa dawa chache tu!!

4. Huduma ya X-ray ni hadi utoe rushwa kidogo

Wanasema mtu wa x-ray ni mmoja tu hospital nzima kwa hiyo lazima 'kumlinda' na analindwa kweli!

5. Baadhi ya dawa unaweza tu kuambiwa hazipo ila mwingine akaambiwa zipo hususan ukiwa na bima!

6. Hakuna watu wanajua kulindana kama hawa jamaa wa Magunga!!
Unaweza kushuhudia kabisa dokta kapanda Bajaj au pikipiki kasepa lakini ukimuuliza nesi anakuambia yuko ofisini.

Nitaendelea
 
Ume raise very irritating issues, tuzipeleke kwa nani? shida kubwa ni hiyo!
 
Write your reply...The same like handeni boman
 
Back
Top Bottom