Mdude_Nyagali
Member
- Dec 11, 2022
- 79
- 1,444
1. Msajili wa Vyama vya siasa wala Rais au serikali yake hawana Mamlaka ya kuamua au kutupangia kuhusu Katiba tunayo itaka. Hicho kigenge walichokiunda hakina Mamlaka hayo kikatiba na kikanuni. Hivyo Kinachofanyika ni Ukora na ni Ultra vires Act kabisa. Ni muendelezo wa uvunjaji wa katiba na Sheria za Nchi. Kwa mazingira hayo Slsisi wananchi Tutaandika Katiba yetu wenyewe inayotokana na maoni yetu kabla ya uchaguzi mkuu 2025. Hiyo wanayo kwenda kuifanya kwa jina sijui la minimum ammendment ni yao na chawa wao na haina ridhaa ya Bunge.
Tume Huru na Katiba Huru vitatengenezwa na Watanzania wenyewe kupitia sheria husika na ushiriki wa pamoja ulio huru, wazi na Jumuishi. Huu Ukora ulaaniwe na kukataliwa.
2. Katika zile siku 30 tulizowapa serikali kutekeleza matakwa ya wananchi kuhusu IGA na katiba kwasasa zimebaki siku 25 ili Kabla ya kupanga tarehe ya maandamano. Kwamba maandamano hayo yatahakikisha Ngorongoro na Ardhi yake inatambulika kuwa Ardhi ya Wamasai kama ardhi yao ya asili kwani siyo tu kuwa Maasai ni Indegenous Community (aboriginal) bali pia Ardhi ya mababu zao. Kwamba maisha, mila, uchumi na utamaduni wao umefungamana na ardhi ile na kuwaondoa katika eneo hili ni kutaka kuwafuta katika sura ya dunia kama ilivyotokea kwa wahindi wekundu kule Marekani.
Sambamba na hilo lengo kuu la maandamano ni kuhakikisha IGA inafutwa kwa ujumla wake na Bunge linafuta Azimio Lake la Kinazi na zaidi kwamba Tume Huru ya Uchaguzi na Katiba Mpya vinapatikana watake wasitake kabla ya 2025.
3. Maandamano yanalenga kuhakikisha kuwa Mali za Zanzibar zinasimamiwa na wazanzibar kupitia Serikali yao, Raslimali za Asili za Tanganyika zinasimamiwa na Watanganyika Kupitia serikali yao na zile Mali ambazo ni za Muungano zitasimamiwa kwa pamoja chini ya serikali ya Jamuhuri ya Muungano itakayoundwa kwa usawa na pande Mbili za Tanganyika na Zanzibar. Lengo ni kuwa Tanganyika inakuwa na Rais wake na Bunge lake na Zanzibar iwe na Bunge Lake na Rais wake na Serikali ya Muungano iwe na Rais wake na Bunge Lake.
4. Kukosekana ulinzi ,uwajibikaji na Matumizi Endelevu ya Raslimali za Asili za Watanganyika ni kwasababu tunazikabidhi na kuziweka kwenye Mikono ya Serikali ya Jamuhuri ya Muingano na wazanzibar wote hawana uchungu na Urithi wa Tanganyika .( Rejea Mkataba wa Kifisadi wa IGA)
Msingi wa hoja hii ni kwamba Kama ambavyo Mtanganyika hawezi simamia na kubinafsisha au kukodisha Mali za Wazanzibar hivyo hivyo Mzanzibar hawezi kuruhusiwa Kuuza au kukodisha Mali za watanganyika. Hizi ni nchi mbili tofauti na kila moja ina ardhi yake na Ardhi siyo suala la Muungano.
5. Teuzi nyingi zinafanywa kimkakati ili kuwadhibiti au kuwaondoa kabisa viongozi wenye angalau nakisi ya uadilifu na kuteuwa Manyapara au chawa wengi wao wakiwa watanganyika watakao simamia mikataba ya kizembe yenye athari hasi kwa Tanganyika kwasababu ya Bakuli la Dengu.
6. Kila Mwananchi na Mtanganyika aingie kwenye Maombi kujiandaa katika Kusudio hili la Maandamano ya Umma yatakayofanyika bila kikomo. Kwamba tutakapo kamilisha taratibu za kisheria na Kutangaza Maandamano wote tuwe tayari kusimama kuhesabaiwa ili kuvuka kwenda Nchi ya ahadi.
7. Tuache kabisa jitihada za kujifungamanisha katika vyama ni wakati wakuungana kama watanganyika na vyama vitumike tuu kama Njia ya kutufikisha katika lengo kuu la kuirejesha Tanganyika ili watoto watanganyika wapate haki ya kufaidi raslimali zao na kuzilinda kwa wivu na uzalendo kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kizazi kijacho. Kiongozi yeyote anayeona aibu kuitamka na kuitetea Tanganyika nasisi tuone aibu kushirikiana naye.
Hawa Viongozi mnao waona wakiwatesa, kuwatisha, kuwadhulumu, kuwapoka haki zenu, kuwasweka mahabusu Kama Mungu aishivyo hamtawaona tena na hawatakuwa na mahala pa kusimama na wala Mahali pao hapata onekana tena kwasababu Mungu amekwisha ondoa nafasi yao na kuwakataa kwasababu ya ushirikina wao uliokithiri.
Aluta Continua. Mapambano yanaendelea
BAK Mwabukusi
Shambani Busokelo.