Mambo saba muhimu kuelekea maandamano ya kitaifa bila kikomo

Ni kweli mkuu mambo hayo ni muhimu sana.

Haiwezekani Mtu wa Paje aje kuuza bandari za Bara wakati za kwao Forodhani wameziacha.
 
Anza kwanza mwenyewe mkuu wakikufinya kende ndo utaelewa we jichanganye😁😁😁😁😁
 
Mtaandamana wenyewe
 
Anza kwanza mwenyewe mkuu wakikufinya kende ndo utaelewa we jichanganye😁😁😁😁😁
Soma historia ya Biblia pengine inaweza kubadili namna yako ya kufikiri na kiyatazama maswala..

==============================================
Kut 14:1‭-‬31 SUV

BWANA akasema na Musa, akamwambia, "...Waambie wana wa Israeli, kwamba warudi na kupiga kambi yao mbele ya Pi-hahirothi, kati ya Migdoli na bahari, kukabili Baal-sefoni; mtapanga mbele yake karibu na bahari. Naye Farao atasema katika habari za wana wa Israeli, Wametatanishwa katika nchi, ile jangwa imewazuia wasitoke. Nami nitaufanya uwe mgumu moyo wa Farao, naye atafuata nyuma yao; nami nitajipatia utukufu kwa Farao, na kwa jeshi lake lote; na Wamisri watajua ya kuwa mimi ndimi BWANA.."

Basi wakafanya hivyo. Mfalme wa Misri aliambiwa ya kuwa wale watu wamekwisha kimbia; na moyo wa Farao, na mioyo ya watumishi wake, iligeuzwa iwe kinyume cha hao watu, nao wakasema, Ni nini jambo hili tulilotenda, kwa kuwaacha Waisraeli waende zao wasitutumikie tena? Akaandalia gari lake, akawachukua watu wake pamoja naye; tena akatwaa magari mia sita yaliyochaguliwa, na magari yote ya Wamisri, na maakida juu ya magari hayo yote. Na BWANA akaufanya moyo wake Farao mfalme wa Misri kuwa mgumu, naye akawafuata wana wa Israeli; kwa sababu wana wa Israeli walitoka kwa ujeuri. Wamisri wakafuata nyuma yao, farasi zote na magari yote ya Farao, na askari zake wenye kupanda farasi, na jeshi lake, nao wakawapata hali wamepanga pale karibu na bahari, karibu na Pi-hahirothi, kukabili Baal-sefoni.

Hata Farao alipokaribia, wana wa Israeli wakainua macho yao, na tazama, Wamisri wanakuja nyuma yao; wakaogopa sana; wana wa Israeli wakamlilia BWANA. Wakamwambia Musa, "..Je! Kwa sababu hapakuwa na makaburi katika Misri umetutoa huko ili tufe jangwani? Mbona umetutendea haya, kututoa katika nchi ya Misri? Neno hili silo tulilokuambia huko Misri, tukisema, Tuache tuwatumikie Wamisri? Maana ni afadhali kuwatumikia Wamisri kuliko kufa jangwani."

Musa akawaambia watu, "..Msiogope, simameni tu, mkauone wokovu wa BWANA atakaowafanyia leo; kwa maana hao Wamisri mliowaona leo hamtawaona tena milele. BWANA atawapigania ninyi, nanyi mtanyamaza kimya.."

BWANA akamwambia Musa, "Mbona unanililia mimi? Waambie wana wa Israeli waendelee mbele. Nawe inua fimbo yako, ukanyoshe mkono wako juu ya bahari, na kuigawanya; nao wana wa Israeli watapita kati ya bahari katika nchi kavu. Nami, tazama, nitaifanya mioyo ya Wamisri kuwa migumu, nao wataingia na kuwafuatia, nami nitajipatia utukufu kwa Farao, na kwa jeshi lake lote, kwa magari yake na kwa wapanda farasi wake. Na Wamisri watajua ya kuwa mimi ndimi BWANA, nitakapokwisha kujipatia utukufu kwa Farao, na magari yake, na farasi zake..."

Kisha malaika wa Mungu, aliyetangulia mbele ya jeshi la Israeli, akaondoka akaenda nyuma yao; na ile nguzo ya wingu ikaondoka hapo mbele yao, ikasimama nyuma yao; ikafika kati ya jeshi la Misri na jeshi la Israeli; napo palikuwa na lile wingu na lile giza, lakini lilitoa nuru wakati wa usiku; na hawa hawakuwakaribia hawa usiku kucha. Musa; akanyosha mkono wake juu ya bahari; BWANA akaifanya bahari irudi nyuma kwa upepo wa nguvu utokao mashariki, usiku kucha, akaifanya bahari kuwa nchi kavu, maji yakagawanyika. Wana wa Israeli wakaenda ndani kati ya bahari katika nchi kavu; nayo maji yalikuwa ukuta kwao mkono wa kuume, na mkono wa kushoto.

Na wale Wamisri wakawafuatia, wakaingia ndani kati ya bahari, farasi zote za Farao, na magari yake, na wapanda farasi wake. Ikawa katika zamu ya alfajiri, BWANA akalichungulia jeshi la Wamisri katika ile nguzo ya moto na ya wingu, akalifadhaisha jeshi la Wamisri. Akayaondoa magurudumu ya magari yao, hata yakaenda kwa uzito; na Wamisri wakasema, Na tukimbie mbele ya Israeli; kwa kuwa BWANA anawapigania, kinyume cha Wamisri.

BWANA akamwambia Musa, "Nyosha mkono wako juu ya bahari, ili maji yarudi tena juu ya Wamisri, juu ya magari yao, na juu ya farasi zao."

Musa akaunyosha mkono wake juu ya bahari, na kulipopambazuka, bahari ikarudi kwa nguvu zake; Wamisri wakakimbia mbele yake; na BWANA akawakukutia mbali hao Wamisri kati ya bahari. Yale maji yakarudi yakafunikiza magari na wapanda farasi, hata jeshi lote la Farao lililoingia katika bahari nyuma yao; hakusalia hata mtu mmoja.

Lakini wana wa Israeli wakaenda katika nchi kavu katikati ya bahari; na hayo maji yalikuwa ni kuta upande wao wa kuume, na upande wao wa kushoto. Ndivyo BWANA alivyowaokoa Israeli siku ile mikononi mwa Wamisri; Waisraeli wakawaona Wamisri ufuoni kwa bahari, wamekufa. Israeli akaiona ile kazi kubwa aliyoifanya BWANA juu ya Wamisri, ndipo hao watu wakamcha BWANA, wakamwamini BWANA, na Musa mtumishi wake.
===============================================
Ndugu@Charles kilian hivi ndivyo Bwana Mungu na baba yetu anavyoweza kuokoa watu wake.

Yaani huwa ni kama utani au masihara fulani hivi huku watu wasiomini na wenye kebehi kama wewe wakiwa pembeni wakidhani wenzao wanaoamini ktk matendo makuu ya Mungu ni wehu au wamechanganyikowa.!!

Wengi walikuwa hawamwelewi Musa kabisa kama ambavyo Leo watu hawawaelewi watu kama Mdude Nyangali au Boniface Mwambukusi au Mch. Mbarikiwa Mwakipesile...

Lakini ukombozi
ulipotokeza tu huku matesaji na maadui za Mungu walipoangamizwa, hatimaye watu kama wewe Charles kilian mwisho wa siku mtamtukuza kumuamini Mungu na Mdude Nyangali au Boniface Mwambukusi au Mch. Mbarikiwa Mwakipesile na itashuhudiwa kwa kusema;

"....Ndivyo BWANA alivyowaokoa Israeli Tanganyika] siku ile mikononi mwa Wamisri [wakora wa CCM]; Waisraeli [Watanganyika] wakawaona Wamisri [ma - CCM] ufuoni kwa bahari, wamekufa. Israeli [Tanganyika] akaiona ile kazi kubwa aliyoifanya BWANA juu ya Wamisri [CCM], ndipo hao watu wakamcha BWANA, wakamwamini BWANA, na Musa [Tundu Lissu, Mdude Nyangali, Boniface Mwambukusi na Mbarikiwa Mwakipesile] watumishi wake..."
 
Asante sana kwa neno la mungu akubariki sana
 
Rais ni mshamba tu yaani nashindwa kuelewa CCM kwa nn inafel muda mwingi.Rais anasimama na hakui aongee nn,Hv leo hii unawatukana watu kwamba hawaelewi chochote kuhusu nn kiingie kwenye katiba yetu,Kwa kweli lzm tukubali kwamba Rais hatuna.
 
Habar kamanda[emoji137]
Katika andiko hili Jambo la nane ni kuhusu maswala ya ajira ...wa Tanganyika huwa Hawaruhusiwi kuomba ajira za serikalini Zanzibar wakati wa zanzibar wao wanaruhusiwa kuomba ajira huku bara ...Zanzibar wakitangaza kazi wanaweka kigezo Cha kwamba lazima uwe na kitambulisho Cha mzanzibari mkazi, wakijua wazi mtanganyika hawez kuwa nacho ...wakati wao wakija huku wanaomba tu bila masharti yoyote .
[emoji1732][emoji1732][emoji1732][emoji1732][emoji1732]
 
Hapa umenena. Mungu akupe ujasiri uongoze hayo maandamano ili kila mmoja afaidi urithi alioachiwa na Mungu, muumba wa wote. Hapa umelikoroga. kwani ni nani aliyesema mali za Tanganyika zitakuwa za JMT kama si Nyerere. Yeye ni Mzanzibari? Wenye uchungu ni Watanganyika kwa vile huu ni urithi wao. Akija Mzanzibari anakuja kama Mtanzania mwenye haki na hadhi sawa na Mtanganyika ktk JMT.

Nakazia: Ni wakati sasa akina Mdude tuwaone kwenye hayo maandamano badala ya kupiga domo tu.

Tunasubiri kuwaona barabarani na mitaani ili tuungane nao. Kinyume na hivyo, nikumbushe tu kuwa kelele za mlangoni hazimzuii mwenye nyumba kulala.
 
Katafute kitambulisho cha Mzanzibari mkaazi, wacha kulialia kama mtoto ndogo.

Ajira za Tanzania zinatolewa pia kwa kitambulisho cha Mtanzania. Jee nako kuna ubaguzi? Kama hakuna kwanini iwe nongwa kwa Zanzibar?
 
Hivi kweli mkuu utakua front line ukiandamana!!?

Ngoja tuone!!
 
Kukosekana ulinzi ,uwajibikaji na Matumizi Endelevu ya Raslimali za Asili za Watanganyika ni kwasababu tunazikabidhi na kuziweka kwenye Mikono ya Serikali ya Jamuhuri ya muungano na wazanzibar wote hawana uchungu na Urithi wa Tanganyika
 
Kwamba tutakapo kamilisha taratibu za kisheria na Kutangaza Maandamano wote tuwe tayari kusimama kuhesabaiwa ili kuvuka kwenda Nchi ya ahadi.
 
Umeshashindwa wewe,Magufuli yupo sasa?Mbona Mdude yupo.
 
Tangu nchi ipate uhuru wake hajawahi kutokea kijana wa hovyo kama huyu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…