Mambo sio mazuri DRFA, uongozi wa Lameck Nyambaya haijatulia

Mambo sio mazuri DRFA, uongozi wa Lameck Nyambaya haijatulia

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
BUNDI anaelekea kulia katika Chama cha Soka Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) kwa sababu Mwenyekiti wa chama hicho, Lameck Nyambaya kubananga katiba yake.

Tangu achaguliwe kushika wadhifa huo kwenye uchaguzi uliofanyika karibu miezi minne, Nyambaya hajaitisha kikao cha XCom ambacho kingefanikisha mwenendo wa chama hicho kikubwa hapa nchini.

Ukimya wa Mwenyekiti kuhusu kuitisha kikao hicho nyeti, kumesababisha ukosefu wa imani naye hasa kwa nafasi nyeti kama mweka hazina wa chama ambaye ndiye mwenye fuko la pesa za chama.

Kama hiyo haitoshi baadhi ya wajumbe kuhoji uhalali uwepo wa watendaji ambao wanaibua maswali mengi kutoka kwa wajumbe waliochaguliwa.

Malalamiko ya wadau wa soka hapa nchini ni kwamba, Nyambaya anaonekana kupendelea zaidi vyama vya soka vya Ilala (IDFA) na Ubungo (UFA) katika matukio yanayohusu soka na kuzisahau wilaya nyingine zinazounda mkoa wa Dar es Salaam.

Katika nafasi za uteuzi, anatakiwa ateue mjumbe kutoka Chama cha Soka Temeke (TEFA) ambacho hakina mjumbe DRFA.

Wajumbe wamefika mbali zaidi na kuuliza uhalali wa watendaji wawili ambao majina yao yamehifadhiwa ambao katika utekelezaji wa majukumu ya chama hicho.

Wajumbe wanasikitishwa na kiburi cha Mwenyekiti huyo hata anapokumbushwa kuhusu suala hilo lakini haoneshi ushirikiano na wajumbe wake.

Anayofanya Nyambaya kwenye utendaji wa majukumu ya chama, inaonesha mwenendo mbaya wa maendeleo ya chama.

DRFA ni chama nyeti hapa nchini kwa sababu kimebeba timu kubwa za Simba, Yanga, Azam, KMC na JKT Tanzania.

Mkoa ambao ndio baba wa soka hapa nchini kwa sababu ya miamba hiyo ya soka inayotikisa Afrika, matukio kama hayo, yanaaahiria kutaka kuvuruga heshima ya DRFA.

Pamoja na kasoro nyingine, inaonekana DRFA kuna upendeleo kwa baadhi ya wilaya, zinapendelewa zaidi mbili kuhusu uteuzi wa watendaji ambazo ni Ilala na Ubungo.

Wakati Temeke hakuna aliyeteuliwa, jambo ambalo linazua maswali mengi kutoka kwa wadau.
Jambo ambalo kubwa linawatatiza wadau wa soka ni kutoitishwa kwa Mkutano utakaopendekeza mipango yote inayohusu utekelezaji wa majukumu ya kiuongozi hasa eneo la fedha.

Eneo hilo linaleta hisia mbaya kwa sababu hazijulikani fedha za chama zinatumikaje bila wajumbe kujua.
Kwa matatizo hayo yanayoashiria kutaka kuleta vurugu kwenye mchezo pendwa, wadau wa soka wanamtaka Nyambaya aitishe mkutano haraka ili kuliondoa wingu baya litakalochafua hali ya hewa.
 
Kama yupo kinyume na katiba mna haki kisheria kumfungulia mashtaka! Lakn Kama hajavunja katiba au kanuni yoyote hakuna maana ya kulalamika
 
Back
Top Bottom