ToniXrated
JF-Expert Member
- Sep 21, 2022
- 1,134
- 2,993
Amani iwe nanyi
Katika siku za hivi karibuni mara baada ya Simba kumteua Master Guardiola Mgunda, nimeweza kugundua masuala kadhaa! Ungana nami uweze kuyajua mambo hayo.
1. Mzamiru amezaliwa upya, nikiri kuwa nilikuwa miongoni mwa watu waliokuwa wakikosoa sana uchezaji wa Mzamiru Yasin kutokana na mpira wake wa kupiga pasi fyongo, kurudisha mipira nyuma na kufanya mikimbio isiyokuwa na umuhimu. Toka Mgunda aingie Simba nimemuona mzamiru mpya.
Mzamiru wa sasa hana mambo mengi, anasafa uwanjani kukata umeme na pindi akiupata mpira amekuwa na maamuzi bora sana ya kuachia pasi zenye macho kwa mchezaji aliyekaribu naye. Hivi ndivyo kiungo mkabaji wa kati anatakuwa awe. Mzamiru ameongeza kujiamini uwanjani na kitete kimemtoka. Hongereni benchi la ufundi la simba kwa kumfanya mzamiru awe bora.
2. Kibu denis, licha ya kiwango chake cha kazi kuwa kikubwa uwanjani lakini bado anasumbuliwa sana na kutokuweza kufanya maamuzi sahihi anapokuwa na mpira. Hajui ni wakati gani anatakiwa akimbie na mpira na wakati gani anatakiwa atoe pasi na wakati gani apige shuti golini.
Kibu anatakiwa ajue kuwa Simba haimpi presha ya yeye kufunga kila mechi. Hivyo inampasa atulize mchecheto awapo uwanjani. Yote kwa yote nafurahishwa sana na uchezaji wake pindi anapokuwa hana mpira. Leo amemsaidia sana Israel Mwenda kwenye kukaba.
3. Safu ya ulinzi ikiwa chini ya kapteni Tshaba imetulia, hofu yangu ipo sana kwa Kennedy Juma, huyu jamaa sijui ni uzito wa mwili au nini, ila anaonekana anakosa kujiamini sana. Simba ilishatoka katika zama za butua butua. Tunataka tuweke boli chini ila kennedy akipata mpira huwa ni kubutua tu. Ajifunze utulivu na kujiamini kutoka kwa Kitasa Inonga Varane, Babu Onyango kama kawaida yake ni marufuku kucheka na nyau.
4. Putin kama Putin kwenye michezo mitatu iliyopita ameonesha kujiamini sana na utulivu umeongezeka kiwanjani, Nimependa ushirikiano wake na Mzamiru, leo walitawala dimba vilivyo.
5. Chama, Okrah na Generali Phiri waongezewe mikataba. Wana mengi ya kuisaidia Simba. Okrah ameziba pengo la Morison kabisa kiasi kwamba hatukumbuki kama tulikuwa na mchezaji anaitwa Bernard Morrison. Phiri na Chama sina haja ya kuwaelezea sana, wanayofanya uwanjani yanajieleza.
6. Israel Mwenda ni mchezaji anayeleta matumaini, kila siku anaendelea kukua bado ana muda wa kusahihisha makosa yake.
VAMOOOOOOOS SIMBAAAAAAAAA!!!