Mambo tuliokua tunadanywa/kudhania kipindi cha utoto!

Mambo tuliokua tunadanywa/kudhania kipindi cha utoto!

qarem

JF-Expert Member
Joined
Oct 19, 2018
Posts
626
Reaction score
825
Hi everyone

Hii ni sehemu ya kuburudika, kujifunza, nk
Bas Leo nimekaa zangu sina hili wala lile nikawa nakumbuka harakati za utotoni nilikumbuka mengi ila lilofanya nicheke nikiwa mwenyewe ni hili.

Kipindi cha nyuma sana vijijini huko ilikua ukitaka kunyoa lazima utumie mkasi/wembe saloon zilikua chache au Hamna kabisa

Hivyo basi ilikua mtu ukishanyolewa zako na mkasi/wembe kulikua na utamaduni wa kufukia nywele, jambo hili kwangu lilikua la ajabu kidogo kwani nilikua nalidadisi sana kwanini tufukie nywele baada ya kuzinyoa?

Basi bwana siku moja baada ya kunyoa ilibidi niende kumuliza bibi maana ndo nilikua naishi nae wazee walikua town huko wanatafuta maisha

Nikamuuliza hivi bibi kwanini watu wakimaliza kunyoa lazima wafukie nywele zao?

Bibi akanijibu [emoji23][emoji23][emoji855] kwakua kwa kipindi hicho nilikua pia sijui dagaa zinatokana na nini na zinatoka wapi hivyo,ilikua rahisi kwake kunidanganya na nilidanganyika,

Akasema ukifukia nywele zinaota dagaa [emoji23][emoji23][emoji23][emoji855] dah bibi (RIP huko uliko [emoji22]) basi bwana kidume nikawa nishaelewa kwanini lazima tufukie nywele,

Ikawa ndio tabia nikitoka tu kunyoa naokota nywele zangu naenda kuzitengenezea tuta mfano wa bustani hivyiii, nawekea majani juu yale yaliokauka ili mbegu zisipate direct sun light [emoji23][emoji23][emoji23],

Kila asubuhi na jioni nilikua naenda kumwagilia nywele zangu dah [emoji855][emoji23]..na kukagua kama zimeota ila holaaaaaa,

Kadri siku zilivyoenda ndio nikajua nimedanganywa [emoji22]

LINGINE

Jambo lingine ambalo nilikua nadanganywa na nilidanganyika ni kipindi mdogo wangu wa mwisho anazaliwa,

Hivyo nilipomuona mama na mtoto nilimuuliza umemtoa wapiii akasema katoka kumnunua dah niliamini watoto wananunuliwa hospital [emoji855]

ANOTHER ONE

Halafu nimekumbuka jambo lingine nakumbuka kipindi hicho mvua ikinyesha na ngurumo basi nilikua nikiamini kuwa huko mbinguni kuna mapipa ya maji hivyo zile ngurumo za radii mvua inapokaribia kukata ni kama mungu anakombeleza mabaki ya maji katika pipa la majii,[emoji44][emoji44]

Karibu wana JF Tutoe stress kwa kukumbuka moments za utotoni

NB;kama kuna uzi mwingine kama huu humu ndani mods waunganishe,mana kujua ni ngumu zipo threads nyingi mno!

Welcamuni [emoji58]
 
Nashangaa sana nyuzi zinazozungumzia habari za utotoni watu hawachangii,,Mimi nimesuka Uzi kuhusu swali lolote la akili ulilowahi kuulizwa na mtoto mdogo,,lakini watu hollah hawachangii daah manina wallah
 
Kuna mimea flani ina majani mapana inaota kwa kutambaa ukiyakata yana ute flani usio na rangi tulidanganywa ukipaka sehem za siri baada ya siku 3 umeota vuzy. Kuna jamaa tulisoma nalo lilikuwa na vuzy likawa linatulingishia tukawa tunapaka na sisi yale majani kutwa mara 3 ila hola mzigo hauoti. Tuliteseka sana kutokuwa na hii kitu kwa muda mrefu mpaka tulipokuja kugundua kumbe jamaa nalo halijaota ila hua likinyolewa kichwani linaokota nywele linazibandika huko kwa gundi ya miti fulani inatoa ute mweupe mara nyingi inapandwa kwenye viwanja/mashamba kutengeneza mpaka
 
Nilikua nakatazwa kula huku naimba et ntaolea mbali,,Kipindi icho nna kidemu changu Monduli kwa Babu uko,sasa naambiwa ntaenda kuolea Dar sijui Mtwara uko na nikiwaza ntamkosa Manzi angu apa Monduli nikaoe uko mbali doooh sikuwahi kuimba tena wakati wa msosi
 
[emoji23][emoji23][emoji23] watu wanataka nyuzi za kunyanduana tu
 
Nilikua nakatazwa kula huku naimba et ntaolea mbali,,Kipindi icho nna kidemu changu Monduli kwa Babu uko,sasa naambiwa ntaenda kuolea Dar sijui Mtwara uko na nikiwaza ntamkosa Manzi angu apa Monduli nikaoe uko mbali doooh sikuwahi kuimba tena wakati wa msosi
Haha,kulikua na busara kubwa ndani yake maana madhara ya kula huku unaongea yanajulikana!
 
[emoji23][emoji23][emoji23] dah kwahio vu**** vumbi la kokoto mkajua ni dili kubwa dah utoto raha haha
Kuna mimea flani ina majani mapana inaota kwa kutambaa ukiyakata yana ute flani usio na rangi tulidanganywa ukipaka sehem za siri baada ya siku 3 umeota vuzy. Kuna jamaa tulisoma nalo lilikuwa na vuzy likawa linatulingishia tukawa tunapaka na sisi yale majani kutwa mara 3 ila hola mzigo hauoti. Tuliteseka sana kutokuwa na hii kitu kwa muda mrefu mpaka tulipokuja kugundua kumbe jamaa nalo halijaota ila hua likinyolewa kichwani linaokota nywele linazibandika huko kwa gundi ya miti fulani inatoa ute mweupe mara nyingi inapandwa kwenye viwanja/mashamba kutengeneza mpaka
 
Sisi katika utoto tulikuwa hatuamini/ hatujui kwamba mwanamke huzaa kupitia ukeni bali kupitia njia ya haja kubwa. 🤓
 
Sisi katika utoto tulikuwa hatuamini/ hatujui kwamba mwanamke huzaa kupitia ukeni bali kupitia njia ya haja kubwa. [emoji851]
Hahahaha mlikua mkiwaza nini mkuu?
 
Hiyo ya kununua watoto karibu kila mtu alidanganywa
Sisi tuliambiwa uking'oa jino wakati wa kutupa ni lazima utamke maneno la sivyo halioti
Nywele ni lazima utupe chooni ukitupa ovyo hazioti
 
Mama angu aliniambia mdogo wangu walimuokota pembezoni mwa bahari..kuna siku mdogo angu alininyea kwenye spesheli langu..nikaanza kumlilia Mama twende pembezoni mwa bahari tumrudishe Yule mdogo wangu ..tukamuokote mwingine..😂😂 utoto bwana
 
Ukinyooshea kaburi kidole ni lazima uking'ate la sivyo ziwa la mama yako linafanya nini? Malizieni kwa pamoja

Ukimkata mjusi mkia na mkia ukawa unatatarika sharti utamke "mwenyewe mwenyewe mwenyewe" kwa spid ya kuendana na mkia unavyotatarika mpaka utakapotulia kwakua ule mkia unakua unakufanya nini? Malizieni kwa pamoja

Ukifanya kosa na ukataka lisahaulike vidole unavifanya nini? Malizieni kwa pamoja
 
Nywele zinafukiwa kwa ajili ya kukwepa mambo ya kishirikina.

Mtu akichukua nywele zako ni rahisi sana kukuroga.
 
Nashangaa sana nyuzi zinazozungumzia habari za utotoni watu hawachangii,,Mimi nimesuka Uzi kuhusu swali lolote la akili ulilowahi kuulizwa na mtoto mdogo,,lakini watu hollah hawachangii daah manina wallah
Wana JF wengi hatujapitia utoto, tumezaliwa tukiwa university Havard, Cambridge etc nyie mliopitia utoto hivi mlikosea wapi? Haya simulieni experience zenu tuwasikilize.
 
Ukinyooshea kaburi kidole ni lazima uking'ate la sivyo ziwa la mama yako linafanya nini? Malizieni kwa pamoja

Ukimkata mjusi mkia na mkia ukawa unatatarika sharti utamke "mwenyewe mwenyewe mwenyewe" kwa spid ya kuendana na mkia unavyotatarika mpaka utakapotulia kwakua ule mkia unakua unakufanya nini? Malizieni kwa pamoja

Ukifanya kosa na ukataka lisahaulike vidole unavifanya nini? Malizieni kwa pamoja
1. Linaoza
2. Unakutukana
3. Unaweka kijiti(chelewa) kwenye nywele kichwani
 
Kuna Yale maneno sijui kunguru chukua jino hili......
Nmesahau [emoji23][emoji23] utoto bhna
Hiyo ya kununua watoto karibu kila mtu alidanganywa
Sisi tuliambiwa uking'oa jino wakati wa kutupa ni lazima utamke maneno la sivyo halioti
Nywele ni lazima utupe chooni ukitupa ovyo hazioti
 
Hahah umevurugwa wewe
Wana JF wengi hatujapitia utoto, tumezaliwa tukiwa university Havard, Cambridge etc nyie mliopitia utoto hivi mlikosea wapi? Haya simulieni experience zenu tuwasikilize.
 
Back
Top Bottom