Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mimi nakumbuka walikua wakisema ukinyoshea kaburi kidole,kidole kinapinda hivyo tulikua tunakunja ngumi ndo tunanyooshea makaburii kumuelekeza MTU!Ukinyooshea kaburi kidole ni lazima uking'ate la sivyo ziwa la mama yako linafanya nini? Malizieni kwa pamoja
Ukimkata mjusi mkia na mkia ukawa unatatarika sharti utamke "mwenyewe mwenyewe mwenyewe" kwa spid ya kuendana na mkia unavyotatarika mpaka utakapotulia kwakua ule mkia unakua unakufanya nini? Malizieni kwa pamoja
Ukifanya kosa na ukataka lisahaulike vidole unavifanya nini? Malizieni kwa pamoja
Mama angu aliniambia mdogo wangu walimuokota pembezoni mwa bahari..kuna siku mdogo angu alininyea kwenye spesheli langu..nikaanza kumlilia Mama twende pembezoni mwa bahari tumrudishe Yule mdogo wangu ..tukamuokote mwingine..[emoji23][emoji23] utoto bwana
Hahahaaa.....umenikumbusha mbali....nling'oa jino asubuh shulen nikaliweka mkononi had nliporud hom ili tu nkalitupe juu bati.....eti la sivyo halioti!Hiyo ya kununua watoto karibu kila mtu alidanganywa
Sisi tuliambiwa uking'oa jino wakati wa kutupa ni lazima utamke maneno la sivyo halioti
Nywele ni lazima utupe chooni ukitupa ovyo hazioti
Hahahaaa.....umenikumbusha mbali....nling'oa jino asubuh shulen nikaliweka mkononi had nliporud hom ili tu nkalitupe juu bati.....eti la sivyo halioti!
Sana!Hahaha utoto bhn anyway wazee wa zamani kwa zle mbinu zao za kuwafunza watoto zilikua konkii sna tofauti na sasa hiv
Mimi nikikumbuka niliambiwa mafuta ya ndege yanatokana na korosho huwa nachoka kabsa