Mambo tunayaona sasa hivi magumu, miaka inayokuja huko mbele yatakuwa ya kawaida sana

Mambo tunayaona sasa hivi magumu, miaka inayokuja huko mbele yatakuwa ya kawaida sana

APPROXIMATELY

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2021
Posts
2,035
Reaction score
2,715
Habari za mda huu ndugu zangu wanajamii forum.

Dunia imepita kipindi tofauti tofauti sana, kipindi kile enzi za binadamu wa mwanzo kabisa walitumia dhana za mawe kujipatia chakula,kipindi chuma hakijaja.

Kipindi chuma kimekuja kilikuwa kinaonekana ni kitu cha muhimu sana,binadamu wote akili zao zilikuwa kuzalisha vifaa vinavyotokana na chuma.

Ujio wa computer ulileta mapinduzi sana, duniani ulisaidia sana binadamu kuongoza na kutenda mambo mengi kwa wakati mmoja..

Technology imerahisisha mambo mengi sana, kwa hali inapokwenda na kuhakikishia baada ya miaka kadhaa huko mbele, binadamu watakuwa na ujuzi wa kila kitu, fani kama udaktari utakuwa wakawaida sana mtu yeyote atafanya upasuaji tena simple akiwa anakula bigiji mdomoni.

Technology itawezesha binadamu yoyote kutenda mambo yanayoonekana sasa hivi mpaka usomee kwa mdaa mrefu darasani, baadae maroboti yatakapokuja kuteka dunia, itawasaidia binadamu kutenda mambo makubwa kwa urahisi sana.

Kwa sababu ya maendeleo ya dunia na viwanda kuwa vingi, basi itapelekea dunia nzima hali ya hewa kuwa chafu sana, binadamu watakufa sana kwa hali mbaya ya hewa, moshi utatanda dunia nzima, mchana kutakuwa kama usiku, ozone layer itaharibika ukitembea mchana unaungua ngozi, yani hali itakuwa mbaya sana.

Utakuwa unaseti roboti lako linafanya upasuaji wewe unalitazama tu yani simple, maisha yatakuwa mafupi sana, mtu kuishi miaka 30 itakuwa umeishi sana, uzazi utapungua sana,mwanaume kuhitaji mtoto itakuwa unatoa pesa ndefu kupata mdada wa kukuzalia mtoto.

Ushoga utakuwa biashara ya kawaida sana, mpaka shule unafundishwa jinsi ya kuwa shoga, hakuna atakaye kushangaa kila mtu ataishi maisha yake kivyake.

Dar es salaam itaharibika sana, hali ya hewa itakuwa mbaya sana, watu watatembea wamevaa mask muda wote, kutembea itakuwa mwishoo saa 10 jioni maana kwanzia saa 11 ukikutwa mtani unatolewa viungo, vinaendwa kuuzwa kwa watu wenye matatizo mbali mbali kama Figo, bandama, damu n.k

Technology itakuwa kubwa sana kila kiungo kwenye mwili wa binadamu kitakuwa deal,kama mguu wako umevunjika unaagiza mguu mpya unatafutiwa uraiani.

Dunia nzima serikali itakuwa moja,dini itakuwa moja ,pesa zitapotea kabisa, ukitaka kitu unascaniwa mwili kwenye paji la uso au mkononi, pesa zitakuwa hazina deal tena, biashara kubwa itakuwa chakula na maji tu..

Uhalifu utakuwa mkubwa sana,vita kilasiku, kila mtaa utakuwa na ngome zao na sheria zao, ukiingia mtaa usio wako imekula kwako.

Ukimwi utakuwa kama kama mafua,dawa itapatikana,ila utakuja ugonjwa ambao ukipata dakika 2 umekufa, idadi ya binadamu duniani itakuwa ndogo sana, wanaume watakuwa deal sana.
 
502016185_univ_lsr_md.jpg
 
Back
Top Bottom