Ambition plus
JF-Expert Member
- Feb 23, 2018
- 6,101
- 11,381
Technics+Timing+Luck=Miaka 5 nyuma techiniques zilitubeba saana na timing!..ukilipanda august tikiti unalivuna oct kiangazi fulan...ss hv panda hyo hyo august ukitegemea mtakuwa wachache sokoni...unkuta fuso km 20 ziko sokoni!ishu labda kipatikane kiwanda cha kusindika matunda!
Technics+Timing+Luck=
Luck depends good or bad!
Ila shamba ni Risk sana..
Viwanda vya kusindika inawezekana.Ila nina doubt kwanini bidhaa za ndani zina bei kuliko za nje?
Haya mambo bwana ukiyasoma kwenye maandishi, utayaona ni rahisi kweli kama vile bushman alivyokuwa anaichambua report ya CAG, kwa kukopa namba, hiiunaitoa huku, unaiweka hapa mambo yanajipa!!! Baba ingia uwanjani, ndio utaona kumbe ni shughuri!!! Na tatizo lenu huwa hamuongelei kabisa risk zilizopo kwenye kilimo, hasa kwenye haya mazao ya muda mfupi!!, nyanya, bamia, tikiti, vitunguu, kuwa yakishaaiva, ni kukubaliana tuna bei yasoko, kwani huwezi yatunza, tofauti namazao mengine!! Juzi kuna mdau humu, alisema alilima tikiti kama la milioni 2.5,akalileta sokoni, hapo alikula hasara ya milioni 2!!!kilimo sio rahisi ki hivyo.
Tatizo ni elimu tuliyopewa darasani ndio inaharibu watu wengi wasiwe matajiri, tumekaririshwa 1+1=2 kumbe hali halisi 1+1=11 maisha ukiyaelewa ndani ya mda mfupi utakuwa billionea mpaka utaitwa Freemason au muuza ngada.Sio kwa amount hiyo unayoisema laki tano?!! Mimi nipo kwenye shughuri hizi za kilimo, nazifahamu sana!! Sio rahisi hivyo, bora nibaki poor, bila deni la mtu, kuliko nikachukue pesa kwa mtu, ambayo itaenda kuzama, nibaki poor, na madeni juu!! Kwanini taasisi za fedha kwenye mikopo ya kilimo wanakuwa wagumu kutoa pesa?!!
Sikatai ni kweli biashara ukiipatishia muda mfupi tu unakuwa tajiri sana lakini sio kwa mtaji huo wa laki tano!!labda kama kwa biashara haramu!!lakni biashara halali ni kiwango kidogo sanaTatizo ni elimu tuliyopewa darasani ndio inaharibu watu wengi wasiwe matajiri, tumekaririshwa 1+1=2 kumbe hali halisi 1+1=11 maisha ukiyaelewa ndani ya mda mfupi utakuwa billionea mpaka utaitwa Freemason au muuza ngada.
Leo nikucheka uku tuUmenikumbusha yule Dada kule insta kulikuwa hakutoshi, kila siku mtu anaweka 200,000-500,000/- kwa kibobo, hakii kina mama tulipata tabu sana. Unajiulizs anafanya kazi gani ? Kumbe duuuh!
Watu tukakomaa na kujibana hadi vihela vya mboga mweeeh kumbe mwenzetu anafanya mishe za madawa ya kulevya na mumewe puuuumbaaaaavuuuu zake. Japo alitumotivate kupiga kazi ila ..mwisho wa kuvunja kibobo mwenzio ana million mpaka 60-70 huko! Aiseeeee not fair kabisa.
Swala la masanja ...kilimo siyo rahisi kama maandishi ya kutype nyuma ya keyboard! Yeye anajua sana hustle alizopitia, aache kudanganya watz...kuwa laki tano unakodi sijui heka ngapiiii...haya mbegu unanunua na sh ngapi? Madawa? Hizo hekari huwez hudumia mwenyewe lazima uweke watu! Wale washibe walale....aiseee asiwachanganye.
Alichoandika hapo NI UONGO MTUPUUUUU.......hakifanikiwi katika uhalisia.
Laki tano unalima heka moja tu! Na unaweza pata faida ama usipate!
1. Kukodi shamba
2. Kulima shamba
3. Kuweka matuta
4. Mifereji ya maji
5. Kununua mbegu
6. Kutengeneza kitalu
7. Kuhamisha mbegu
8. Kuweka mbolea
9. Usiku kumwagilia
10. Kupiga sawa
11. Kuvuna
12. Kununua chakula cha wakulima
13. Kuwalipa wakulima
14. Kutafuta mteja na kukubaliana nae shambani
15. Umetumia 500,000/
16. Unapata 700,000. Na hujawalipa wakulima. Pumbaaaaaaavuuuuu zako masanja acha uongo tuliolima tunaeleewa bhanaaa
Asante kwa kunikumbusha kilimo. Ntarudi soon huko ha h ha haaaà
hii hamna hii labda sio huku home ndo moja ni 100/=, sasa hiyo 500/= uta muuzia nani?Lakini , Laki Tano hii ina uwezo wa kukodi shamba Ekari 13 pale Kiteto au Mpwapwa na ikakutengenezea Million 15 baada ya Miezi MITATU kwa kulima Matikiti maji. Laki Tano hii hii ina uwezo wa kununua SIMTANK la lita 5000 ( ndoo 250 za lita 20) ambal inaweza kutumika kusolve shida ya maji mtaani kwako kwa kuuza ndoo 1 Sh 500 na ukaingiza 125,000 kwa kila SIMTANK unalouza.
Mi nna 750000Laki tano
Watanzania ndio utamaduni wetu watu wasio na kazi rasmi kusingizia kilimo na wenye pesa nyingi ambazo zimepatikana kwa utata pia hukimbilia kwenye kilimo Kama sehemu ya kujifichia.Mkuu, ebu funguka kidogo hasa hapo kwenye umaluziaji pamepatia mashaka kana kwamba kuna lilio jificha kwa nyuma ya neno kilimo
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]wako vizur Sana halafu Cha ajabu wenyewe wanaishi mjini.Motivational speakers kwa kilimo cha karatasi wako vzr sana.
Laki tano ni lugha ya picha tu ujumbe ndio muhimu kwamba angalia jinsi unavyo zitumia pesa zako, je unazalisha au hauzalishi?Sikatai ni kweli biashara ukiipatishia muda mfupi tu unakuwa tajiri sana lakini sio kwa mtaji huo wa laki tano!!labda kama kwa biashara haramu!!lakni biashara halali ni kiwango kidogo sana
absolutely"If you tell a poor man the trials of getting rich, he will decide to remains poor! "
Kweli aiseeNdio wale wale wanafikiri Faida lazima iwe pesa "toungible material"
kwa mawazo hayo hayo,atakae amua kuingia shambani akalima,hata kama akipoteza laki 5 yote
akirudi round two ana uhakika wa kurudisha ile laki 5 na zaidi,tatizo letu watanzania (sio wavumilivu)
mtu unatiririsha mlolongo mzimaaaaaa sjui madawa sjui nini sjui nini,hivi mmeambiwa vyote lazima mfanye?
Mimi nilianza lima mboga mboga bila kutia dawa yoyote zaidi ya kitalu changu na mbegu na mboga zilistawi na hela nilipiga
hela huna mtaji mdogo halafu unataka ulime kisasa (akili zenu za wapi nyie)
laki 5 kilimo inatosha kwa mwanzo vizuri kabisa,tusivunjane moyo hapa.
Mnaojitia wazoefu huo uzoefu mngeupata wapi kama sio kuamua ingia huko kilimoni?
au huo uzoefu mlitegemea nani angekuletea bure bure? Aseee kuna watu mnajua kukatisha wengine tamaa sana
Nasema HIVIIIIII
kijana kama una laki 5 tafuta Pori kalime achana na hao wakatisha watu tamaaaaa..Yamewashinda hao hawana lolote.