Wacha janja janja.
Ulimwengu wa roho hakuna wakuingia kimzaha hivyo.
Ndoto na maono unayopata yote hufanyika ktk ulimwengu wa nafsi na sio Roho.
Rohoni kulishafungwa na Muumba baada ya adamu kuanguka dhambini, hivyo upeo wa maono ya kiroho kwa mwanadamu haupo tena isipokuwa kinafsi na kimwili tu.
Note: Hao mnaoita mashetan&mapepo ni roho zinazodeal na nafsi zenu na sio Roho, Roho sikuzote ni innocent/hainahatia ndiomaana ukifa inarudi kwa Muumba na nafsi kulala mautini(kuzimu) mpaka ufufuko wa adhabu na hukumu na kikawaida baada ya Uumbaji wa Muumba hakuna uumbaji mwingine unaoweza kufanyika ukihusisha Roho ya mtu ama nafsi kwa ushirikiano na Roho ya kiumbe tofauti na mwanadamu pasipo kuhusika kwa Nguvu za Muumba ama amri yake,
Unapoota ama kufanya zinaa usiku haiwezi kuathiri hali ya roho uliyoshiriki nayo kupata mtoto, huwezi kupata mtoto kwa njia ya zinaa za kiroho ama kinafsi, hiyo haiwezekana na haitokuja kuwezekana, acheni kupotosha jamii.
Mkija na stori zenu muwe mnaweka na ushahidi, ingekuwa roho inauwezo wa kuipa mimba roho nyingine waingilianapo kiroho basi wachawi wangeshawapa mimba watu wengi na kuwazalisha watoto wasio julikana wamepatikanaje, pia wachawi wa kike wangebeba mimba nyingi,
Pia unatakiwa ujuwe, baada ya Uumbaji wa Muumba na kufungwa na uwepo wa muingiliano wa uzao kati mapepo na binadamu(nephilims period) basi hakuna uwezekano tena wa kiumbe yeyote wa kiroho kuongezeka dunian, mashetani na mapepo waliopo leo ni wale wale waliokuwepo kipindi cha akina Nuhu,
Asikudanganye mtu kuwa ana mimba ya kijini ama ana watoto wa kijini, huo ni uongo na upotoshaji, maana roho kwa roho haziwezi sababisha uumbwaji wa roho mpya, pia pepo hawez beba ujauzito sabbu ya muingiliano na roho ya binadamu, ingewezekana kama mapepo wangekuwa na miili ya kibinadamu TU,
Wengi mnaoletaga stori za hivi ni kwamba mmepagawa na uongo wa ushawishi wa hizo stori zenu za kijinga, mikosi na mabalaa yanaweza kukukumba ukishiriki na roho chafu lkn sio kusababisha Uzao wa roho mpya, hata wao pepo kwa pepo hawana uwezo wa kuleta uzao wao mpya, maana Nguvu hizo zilishafungwa, ingekuwa easy hivyo basi majeshi ya mapepo yangeshaumaliza uzao wa watu dunian maana wangekuwa wengi kiidadi.
Pepo, shetan, hawezi kufa mpaka kihama, wala hawez kuonekana isipokuwa kiroho ama kinafsi tu, na hawezi kukupa mimba ama yeye kupata mimba, acheni uzushi.