Mambo ya 50/50 binafsi mnitoe siyatakiiii

Ujerumani bill huletwa kwa kila mtu. Mke na mume kila mtu analipa alichotumia.
 
Hahahaha uliwakomesha kama nakuona ulivyokua unawachamba, yaani hao bila na wewe kujitia wazimu unaweza ikosa haki yako hivi hivi, btw pole kwa kuibiwa jamani inaumiza
Walinijua wale maana tulimtrak yule mwizi mpk tukamapa akileta mikwamo anapokeq simu ya moto toka juu kwake. Tulivyomalizana nikamtoa hela kidogo wacha afurahi aisee.
 
Kuhudumiahudumia wanawake ishapitwa na wakati mamaa, siku hizi mwanamke naye anatakiwa achangie
 
Ngoja tuweke rekodi sawa. Tatizo lililopo mezani sio la mwanaume, ni tatizo la mwanamke. Mwanaume yeye amenyooka. Baki ndani uhudumiwe, totoke wote tukatafute tugawane bill. Hakuna complications. Hakuna ambacho hakieleweki.

Mwanamke ndie mwenye tatizo . Anataka kuwa na kipato at the same time ahudumiwe yake kifedha. Ni ubinafsi na kimantiki ilo wazo linakosa mashiko kea sababu ukiwa na kipato maana yake automatically unaondolewa kwenye kundi la watu tegemezi.

Ikiwa majukumu ya mama wa nyumbani hauwezi kuyafanya kwa sababu unashinda kazini,na kipato unachopata uko kazini akifiki nyumbani. Sasa wewe kama mke una output gani kwenye hiyo familia?

Unalazimisha sana tatizo lionekane lipo upande wa mwanaume. Hapa tatizo ni la mwanamke.
 
Duh! Inamaana huko ujerumani wanawake wanajilipia Bill wenyewe. Ni Bill za matumizi ya kawaida, yani zile za home au Bill za mitoko mkiwa pamoja.
Katika Mitoko. In fact kuna nchi ambazo sheria zao za ndoa hazifungamani na mapato ya ndoa. Afano Abu Dhabi ni kuwa kila mmoja ana kipato chake. Mkiachana kila mtu anachukua begi lake hakuna ati kugawana mali.Ndiyo maana wazungu wengi wanafungia ndoa zao huko
 
Ni hawa hawa hua wanasema wanawake hawafai kufanya kazi wakae ndani kulea watoto, watarubuniwa blah blah leo hawa hawa wanataka wao na wanawake wagawane majukumu ya kulipa bills[emoji23] wanaume wa jf ni kizunguzungu walai
Nakuambiaaa, [emoji23][emoji23][emoji23]
Hatarii mahiii
 
Duh! Ujeruman kuzuri, yaan inatakiwa uishi Ujeruman ndoa ufungie Abu Dhabi. So, inamaana ukifunga ndoa Abu Dhabi ukaja kuishi Tanzania hapo hiyo sheria ya Abu Dhabi itakuwa applicable Bongo au ndo mkiachana wanakudaka na sheria za hapa??!
 
Kwenye mapenzi ya jinsia 1 hata kwa Gays, kuna Provider na submissive.

Sasa huyu Dr Mari yuko position ya Submissive.
 
Duh! Ujeruman kuzuri, yaan inatakiwa uishi Ujeruman ndoa ufungie Abu Dhabi. So, inamaana ukifunga ndoa Abu Dhabi ukaja kuishi Tanzania hapo hiyo sheria ya Abu Dhabi itakuwa applicable Bongo au ndo mkiachana wanakudaka na sheria za hapa??!
Hilo sijui maana mimi si mwanasheria. Ngoja tuwaulize wenye taaluma yao au tuiulize AI itufafanulie
 
Duh! Ujeruman kuzuri, yaan inatakiwa uishi Ujeruman ndoa ufungie Abu Dhabi. So, inamaana ukifunga ndoa Abu Dhabi ukaja kuishi Tanzania hapo hiyo sheria ya Abu Dhabi itakuwa applicable Bongo au ndo mkiachana wanakudaka na sheria za hapa??!
Soma majibu hapa ya AI

Hili ni swali zuri sana na la msingi, kwa sababu masuala ya ndoa za kimataifa yanayohusisha nchi tofauti (sheria za UAE/Abu Dhabi na sheria za Tanzania) yana mkanganyiko wa kisheria lakini yana utaratibu wake.

Kwa ufupi: Ndio, wanaweza kuachana hapa Tanzania, lakini kuna mambo muhimu ya kuzingatia kuhusu sheria ipi itatumika na mahakama gani itashughulikia.

Hapa kuna mchanganuo wa jinsi suala hilo linavyokuwa kwa mujibu wa Sheria ya Ndoa ya Tanzania (Law of Marriage Act, Cap 29):

1. Kutambulika kwa Ndoa ya Abu Dhabi nchini Tanzania​

Tanzania inatambua ndoa zilizofungwa nje ya nchi (Foreign Marriages) ikiwa ndoa hiyo ilifuata sheria za mahali ilipofungwa (Lex Loci Celebrationis). Kama ndoa yenu ilikuwa halali kisheria kule Abu Dhabi, basi Tanzania inaitambua kama ndoa halali.

2. Je, Mahakama ya Tanzania Inao Uwezo (Jurisdiction) wa Kuvunja Ndoa Hii?​

Ndio, Mahakama ya Tanzania (kuanzia Mahakama ya Wilaya hadi Mahakama Kuu) ina uwezo wa kusikiliza kesi ya talaka ya ndoa iliyofungwa nje ya nchi, Mradi tu masharti yafuatayo yatimizwe:

  • Makazi (Domicile/Residence): Angalau mmoja wenu (mdai au mdaiwa) awe na makazi ya kudumu hapa Tanzania, au awe ameishi Tanzania kwa muda usiopungua mwaka mmoja kabla ya kufungua kesi ya talaka.

3. Sheria Ipi Itatumika Kutoa Talaka?​

Hapa ndipo palipo na utofauti mkubwa kulingana na aina ya ndoa mliyofunga kule Abu Dhabi:

  • Kama ilikuwa ndoa ya Kiislamu (Sharia Law):

    Abu Dhabi inafuata sheria za Kiislamu kwenye ndoa za Waislamu. Ukija Tanzania, Sheria ya Ndoa inaruhusu talaka za Kiislamu kufuata taratibu za Kiislamu (kama vile kutoa talaka nje ya mahakama na kisha kuisajili mahakamani, au kwenda Baraza la Utatuzi kama BAKWATA). Mahakama ya Tanzania itaiangalia kama ndoa ya Kiislamu.
  • Kama ilikuwa ndoa ya Kiraia ya Abu Dhabi (Civil Marriage kwa Wasio Waislamu):

    Abu Dhabi hivi sasa ina sheria mpya ya kiraia ya familia kwa wasio Waislamu (Sheria Na. 14 ya 2021). Kama mlifunga ndoa ya aina hii, mkija Tanzania, kesi itabidi ifunguliwe Mahakamani. Mahakama ya Tanzania itatumia Sheria ya Ndoa ya Tanzania kushughulikia talaka hiyo, sio sheria za Abu Dhabi.

4. Sharti la Lazima Kabla ya Kwenda Mahakamani (Tanzania)​

Tanzania ina taratibu ngumu kidogo za talaka kuliko Abu Dhabi. Kabla ya kufungua kesi mahakamani, ni lazima jambo lenu lipitie kwanza kwenye Baraza la Usuluhishi wa Ndoa (Marriage Conciliatory Board).

  • Baraza hili linaweza kuwa la kidini (kama BAKWATA, Makanisa) au la kiserikali (Ustawi wa Jamii).
  • Kama baraza likishindwa kuwasuluhisha, litatoa Hati ya Kushindwa kusuluhisha (Certificate of Failure), ambayo ndiyo inakupa ruhusa ya kwenda kufungua kesi ya talaka Mahakamani.

5. Mgawanyo wa Mali na Matunzo ya Watoto​

Kama mna mali mlizochuma pamoja (iwe ziko Tanzania au Abu Dhabi) au mna watoto, Mahakama ya Tanzania itatumia sheria za Tanzania kuamua:

  • Mali: Hugawanywa kwa kuangalia mchango wa kila mtu (kazi au fedha) katika kuzipata.
  • Watoto: Maslahi bora ya mtoto (Best interest of the child) ndiyo huangaliwa kwanza kwenye kuamua nani akae naye na nani atoe matunzo.
 
So wewe haujawahi kuwa kwenye mahusiano na mwanaume?
 
Sio kama wewe ndio una akili nyepesi kama unyoya? najiongelea mimi unaleta ya mwengine, ya kwake yanakuhusu nini hadi utake kuyajua, huo ni upeku peku na ufukunyuku ndio wanaume wa siku hizi mlichojaaliwa nacho.
Kwani huyo ambaye upo kwenye ndoa nae si ni mwanamke mwenzako? Wapi ambapo umeshindwa kumuelewa The Icebreaker
 
🤣🤣🤣 Utajuaje nae anataka kusagwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…