Wahubiri wa imani ya Kikristo, ni muhimu kutoa maelezo fasaha mnapozungumzia masuala ya ulimwengu wa roho. Mara nyingi, unamsikia mhubiri akisema, "Naona katika ulimwengu wa roho..." lakini ni vema tukajiuliza, roho ni nini? Je, ninyi pia mmekaririshwa tu kwamba roho siyo kitu chenye asili ya kimaada?
Mnasema ni kitu kisichoonekana, lakini wakati huo huo mnahubiri kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani ya mtu, au kwamba ndani ya mtu kuna roho. Pia mnasema kuwa mambo ya kiroho ni mambo ambayo akili ya binadamu haiwezi kuyaelewa.
Kauli kama hizi zinaweza kuonekana kama njia ya kujificha ili kufanikisha ajenda za siri. Ikiwa huwezi kufafanua roho ni nini, ni vyema usihubiri jambo ambalo huwezi kulielezea kwa ufasaha. Inakuwa ni kama kuongoza watu kwenye barabara ya giza.
Acheni kuidhalilisha imani. Yesu ni mwanga, siyo giza.