JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 685
- 1,124
Mtoa taarifa ni mtu yeyote ambaye anafichua mabaya yanayofanywa kwenye jamii kwa kuzingatia miongozo ya Sheria ya mtoa taarifa na shahidi ya mwaka 2015.
Kifungu cha 4 (1 )cha sheria hiyo kinaeleza kuwa mtu yeyote anaweza kutoa taarifa yenye maslahi kwa jamii mbele ya mamlaka sahihi kama mtu huyo anaamini kuwa :-
a) Uhalifu umekwishafanyika, unakaribia kufanyika au kuna uwezekano ukafanyika
b) Mtu Fulani hajafuata sheria, yupo kwenye mchakato wa kuvunja sheria au kuna uwezekano akavunja sheria
c) Afya au usalama wa mtu au jamii upo hatarini au kuna uwezekano ukawekwa hatarini
d) Kwenye taasisi za Umma kuna au kunaweza kuwa na upotevu au usimamizi mbovu wa rasilimali za Umma au matumizi mabaya ya ofisi
e) Mazingira yameharibiwa, yanaharibiwa au kuna uwezekano yakaharibiwa
Kifungu 4(2) kinaeleza kuwa mtoa taarifa anaweza kutoa taarifa za matendo mabaya kwa mtu ambaye ana mamlaka au kwa mtu ambaye anamuamini na mtu huyo aliyeaminiwa atapeleka taarifa hizo kwenye Mamlaka husika.
Kifungu 4 (3) kinaeleza kuwa mtu ambaye mtoa taarifa anaweza kumpa taarifa anaweza kuwa:-
a) Mwenyekiti au mjumbe wa Baraza la Kijiji
b) Kiongozi wa dini inayotambulika
c) Diwani, Meya au Mwenyekiti wa Baraza la halmashauri
d) Mbunge
Kifungu 4 (4) kinaeleza kuwa mtu anayepokea taarifa anapaswa kutunza siri ya taarifa hizo na mtoa taarifa.
Upvote
1