DaudiAiko
JF-Expert Member
- Dec 2, 2012
- 372
- 310
Wana bodi,
Kwanza kabisa nina furaha kubwa kuona jinsi ambavyo watanzania wame endelea kuheshimu maamuzi ya watanzania wenzao katika zoezi zima la uchaguzi. Utulivu huu na amani tuliyo nayo vime wezekana kwa wao kukataa ku shawishika kwa njia yoyote kufanya yasiyo sahihi.
Vile vile katika kipindi hiki ni vyema sana ku elekeza jicho katika nchi zilizo na demokrasia iliyo dumu kwa muda mrefu kuliko yetu. KIpindi hiki, nchi ya Marekani ilifanya uchaguzi na kinacho endelea sasa hivi ni moja kati ya mfululizo wa matukio yanayo ashiria kwamba aliyeshindwa uchaguzi amekataa ku kubali kwamba uchaguzi uliofanyika ulikuwa wa huru na haki.
Jambo la msingi na ambalo lingekuwa jema ku fumbulia macho ni kwamba baada ya miaka mingi sana, uchaguzi wa Marekani wa mwaka huu ulifanyika kwa njia ambayo wananchi walipiga kura kwa posta. Njia hiyo ilisababisha kura zilizo nyingi ku hesabiwa kwa mkono. Wamarekani kwa kawaida huwa wanapiga kura kwa njia ya ki elektroniki ila kwa sababu ya janga la virusi vya korona, walibidi kutumia njia mbadala kupiga kura.
Nchi kama Marekani ni mfano wa kuigwa katika suala zima la demokrasia na sio kitu cha kawaida kwa mzozo mkubwa kuwepo baada ya uchaguzi. Kitu tunachoweza kuji uliza ni kama kuhesabu kura kwa mkono kunaweza kuleta mianya kwenye zoezi la uchaguzi vikiwemo wizi wa kura au kuchelewesha matokeo ya uchaguzi. Vile vile ni jambo zuri kuona jinsi gani wenzetu wanaweza kupinga matokeo mahakamani kwa ushahidi na sio barabarani kwa maandamano.
Tafakari,
Alkhamis Kareem...