Mambo ya kukumbukwa aliyofanya Hayati Dkt. John Magufuli

Joined
Apr 1, 2019
Posts
96
Reaction score
135
Ni wazi kwamba kila mtu anamkumbuka mwendazake kwa mambo mbali mbali (legacy) aliyofanya wakati wa uhai na uongozi wake. Miongoni mwa legacy hizo ni hizi hapa kwa ufupi

1. Kukandamiza demokrasia
Ni katika kipindi chake tumeshuhudia demokrasia ikibanwa wazi wazi huku vyama vya siasa vikizuiwa kufanya mikutano ya hadhara kinyume kabisa na katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania.

2. Kuminya uhuru wa vyombo vya habari
Magufuli atakumbukwa kwa kunyima haki vyombo vya habari kufanya kazi zake kwa uhuru kwa lengo la kutaarifu umma juu ya mambo mbali mbali yaliyokuwa yanaendelea nchini na katika serikali yake. Ni katika kipindi chake tumeshuhudia vyombo mbali mbali vikiwemo vituo vya redio, television na magazeti vikipigwa faini au hata kufungiwa kabisa.

3. Kujenga hofu kwa watumishi wa umma
Ni katika kipindi chake tumeshuhudia watumishi kwenye sekta mbali mbali za umma wakifanya kazi kwa presha kubwa wakihofia kufukuzwa au kuachishwa kazi.

4. Kutengeneza tatizo kubwa la ajira kwa wahitimu wa fani mbalimbali
Mwendazake atakumbukwa kwa kutengeneza jobless graduates wengi kuliko serikali zote zilizopita kwani suala la ajira halikupewa kipaumbele katika serikali yake.

5. Kunyima stahiki na kutopandisha watumishi madaraja
Ni katika serikali yake watumishi wamelia kuhusu nyongeza ya mishahara na kupandishwa madaraja kwa mujibu wa kanuni za utumishi wa umma lakini machozi yao yalikuwa kama kilio cha samaki kwenye maji.

6. Mwendazake ameacha legacy ya kupandisha makato ya bodi ya mikopo toka 8% hadi 15%.
Awali wanufaika wa mikopo ya elimu ya juu walikatwa 8% ya mshahara kama marejesho(returns) ya deni la bodi ya mikopo(heslb) lakini baada ya kuingia madarakani kinyume kabisa na mkataba wa bodi na wanufaika alipandisha makato hayo maradufu hadi kufikia 15% ambayo ndio inalipwa hadi sasa.

7. Mwendazake ameacha legacy ya chuki kwa kugawa watu kwa misingi ya kisiasa na kikanda katika uongozi wake. Ni katika kipindi chake ameligawa taifa kwa kupandikiza chuki dhidi ya wafuasi wa vyama vya siasa hadi kufikia hatua ya watu kuombeana mabaya yakiwemo matatizo ya kuugua na hata kuombeana vifo.

8. Mwendazake atakumbukwa kwa kuminya uhuru wa watu kujieleza, kutoa maoni na kupashana habari. Maana ni katika kipindi chake tumeshuhudia watu mbali mbali wakiwemo wanasiasa, wana harakati na waandishi wa habari wakifunguliwa kesi za uchochezi na wengine kufikia hata kutekwa au kupotezwa kwa sababu tu ya kuikosoa serikali yake.

9. Mwendazake atakumbukwa kwa kuvuruga uchaguzi na kushindisha wagombea wa chama chake nchi nzima. Haijawahi kutokea tangu tupate uhuru na kuanzishwa mfumo wa vyama vingi vya siasa kikashinda chama kimoja tu katika nafasi zote za uwakilishi kuanzia ngazi ya vijiji kwa maana ya wenyeviti wa mitaa, ngazi ya kata kwa maana ya madiwani, na hata uwakilishi katika ngazi ya taifa kwa maana ya ubunge. Lakini chini ya utawala wake wa kubaka demokrasia na kuvuruga uchaguzi jambo hili limewezekana nchi nzima.

10. Mwendazake atakumbukwa kwa legacy ya kujali maendeleo ya vitu hasa upande wa miundo mbinu ya kisasa kuliko maendeleo ya watu na hali zao
. Tumeona na kushuhudia suala la miundo mbinu ya vitu likipewa kipaumbele kikubwa katika serikali yake huku hali na maisha ya watu yakidhoofu na pale walipojaribu kufikisha kilio chao wakidai vyuma vimekaza aliwaonya na kutishia kuwafunga. Lengo likiwa ni kuwafunga midomo ili wasipaze sauti zao.

11. Mwendazake ameacha legacy ya double standard serikalini. Tumeshuhudia na kuona wateule wake mbali mbali kama vile wakuu wa wilaya na mikoa wakifanya mambo kinyume cha sheria na taratibu za nchi lakini wakiachwa katika nafasi zao za utumishi wa umma na mifano yao ipo dhahiri. Vile vile marehemu magufuli ameacha double standard ya upendeleo wa kikanda ambapo tumeshuhudia nyadhifa mbali mbali za juu zikishikiliwa na watu kutoka kanda ya ziwa.

12. Mwendazake atakumbukwa kwa msemo wake maarufu unaosema ''msema kweli ni mpenzi wa Mungu''

Apumzike anako stahili. Amiiin
 
Ndiyo Ukweli Wenyewe.

Nasema Uongo Ndugu Zangu.

😆😅😄😃😂😁😀😃😂😁😅
Apumzike Kwa Amani.

Tutamkumbuka Sana
 
Katika mambo aliyofanya Magufuli ni upimwaji wa viwanja kwa wingi, huu umepunguza rushwa katika upatikanaji wa viwanja. Viwanja vilivyopimwa vinavyouzwa bei ya serikali ni vingi. Ukitaka makubwa labda utake sehemu iliyokwisha changamka.
 
Mambo ya kukumbukwa:

1.Kuondoka duniani wakati hahitajiki.

2.Kuteka wapinzani wake kama akina Azory Gwanda.

3.Kutesa wapinzani wake.

4.Kuua wapinzani wake na wakosoaji wake kama akina Ben saanane na kuwapiga wapinzani wake risasi kama ilivyokuwa kwa Tindu Lissu.

5.Kuua vyombo vya habari.

6.Kuua uhuru wa kujieleza.

7.Kuiba kura.

8.Kuua biashara za watu kupitia sera mbovu za uchumi.

9.Kudanganya katika takwimu za uchumi wa nchi.

10.Kuweka mihimili yote mitatu mfukoni mwake.

11.Kuua uchumi wa nchi kupitia sheria mbovu za uwekezaji.

12.Kuua watu kwa Corona kupitia leadership negligence.

13.Kuhakikisha kuwa akina Ben Saanane na Azory Gwanda walikipata cha mtema kuni.

14.Ukabila kwa kuhamishia rasilimali nyingi za nchi Chato na kujaza wasukuma serikalini.

15 Ukanda kwa kupeleka SGR mwanza wakati siyo economic strategic zone.

16.Ubaguzi wa rangi kwa kuwakandia wanawake weusi.

17.Kugandamiza demokrasia kwa kukataza vyama vya upinzani kufanya siasa wakati CCM kufanya siasa ni ruksa.

18.Kunyanyasa malaika-watoto wa kike wasirudi shule wakipata mimba.

19.Ufisadi wa kutisha kwa kufanya miradi mikubwa bila budget kupita bungeni.

20.Wizi wa kutisha wa mali ya uma kupitia Mayanga constructions LTD.

21.Kubambikizia kesi za kuhujumu uchumi wapinzani wake nchi nzima

22.Kugushi report ya CAG ya hasara za mabilion za ndege za TTCL.
 
12. Alitamani matajiri wote wawe kwenye kundi la wanyonge, halafu masikini wasipande daraja la utajiri bali wabakie pale pale kwenye unyonge.

Aisee kweli huyu alikuwa raisi wa wanyonge
Naaam! Kwa mara ya kwanza tulipata kiongozi ambaye alichukizwa na matajiri na kuhaidi kuwafanya waishi kama mashetwani huku akijinasibu kuwa yeye ni Rais wa wanyonge kitu ambacho ni laana hata kwa mujibu wa maandiko matakatifu.
 
Ni wazi kwamba kila mtu anamkumbuka mwendazake kwa mambo mbali mbali (legacy) aliyofanya wakati wa uhai na uongozi wake. Miongoni mwa legacy hizo ni hizi hapa kwa ufupi

1. Kukandamiza demokrasia
Ni katika kipindi chake tumeshuhudia demokrasia ikibanwa wazi wazi huku vyama vya siasa vikizuiwa kufanya mikutano ya hadhara kinyume kabisa na katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania.

2. Kuminya uhuru wa vyombo vya habari
Magufuli atakumbukwa kwa kunyima haki vyombo vya habari kufanya kazi zake kwa uhuru kwa lengo la kutaarifu umma juu ya mambo mbali mbali yaliyokuwa yanaendelea nchini na katika serikali yake. Ni katika kipindi chake tumeshuhudia vyombo mbali mbali vikiwemo vituo vya redio, television na magazeti vikipigwa faini au hata kufungiwa kabisa.

3. Kujenga hofu kwa watumishi wa umma
Ni katika kipindi chake tumeshuhudia watumishi kwenye sekta mbali mbali za umma wakifanya kazi kwa presha kubwa wakihofia kufukuzwa au kuachishwa kazi.

4. Kutengeneza tatizo kubwa la ajira kwa wahitimu wa fani mbalimbali
Mwendazake atakumbukwa kwa kutengeneza jobless graduates wengi kuliko serikali zote zilizopita kwani suala la ajira halikupewa kipaumbele katika serikali yake.

5. Kunyima stahiki na kutopandisha watumishi madaraja
Ni katika serikali yake watumishi wamelia kuhusu nyongeza ya mishahara na kupandishwa madaraja kwa mujibu wa kanuni za utumishi wa umma lakini machozi yao yalikuwa kama kilio cha samaki kwenye maji.

6. Mwendazake ameacha legacy ya kupandisha makato ya bodi ya mikopo toka 8% hadi 15%.
Awali wanufaika wa mikopo ya elimu ya juu walikatwa 8% ya mshahara kama marejesho(returns) ya deni la bodi ya mikopo(heslb) lakini baada ya kuingia madarakani kinyume kabisa na mkataba wa bodi na wanufaika alipandisha makato hayo maradufu hadi kufikia 15% ambayo ndio inalipwa hadi sasa.

7. Mwendazake ameacha legacy ya chuki kwa kugawa watu kwa misingi ya kisiasa na kikanda katika uongozi wake. Ni katika kipindi chake ameligawa taifa kwa kupandikiza chuki dhidi ya wafuasi wa vyama vya siasa hadi kufikia hatua ya watu kuombeana mabaya yakiwemo matatizo ya kuugua na hata kuombeana vifo.

8. Mwendazake atakumbukwa kwa kuminya uhuru wa watu kujieleza, kutoa maoni na kupashana habari. Maana ni katika kipindi chake tumeshuhudia watu mbali mbali wakiwemo wanasiasa, wana harakati na waandishi wa habari wakifunguliwa kesi za uchochezi na wengine kufikia hata kutekwa au kupotezwa kwa sababu tu ya kuikosoa serikali yake.

9. Mwendazake atakumbukwa kwa kuvuruga uchaguzi na kushindisha wagombea wa chama chake nchi nzima. Haijawahi kutokea tangu tupate uhuru na kuanzishwa mfumo wa vyama vingi vya siasa kikashinda chama kimoja tu katika nafasi zote za uwakilishi kuanzia ngazi ya vijiji kwa maana ya wenyeviti wa mitaa, ngazi ya kata kwa maana ya madiwani, na hata uwakilishi katika ngazi ya taifa kwa maana ya ubunge. Lakini chini ya utawala wake wa kubaka demokrasia na kuvuruga uchaguzi jambo hili limewezekana nchi nzima.

10. Mwendazake atakumbukwa kwa legacy ya kujali maendeleo ya vitu hasa upande wa miundo mbinu ya kisasa kuliko maendeleo ya watu na hali zao. Tumeona na kushuhudia suala la miundo mbinu ya vitu likipewa kipaumbele kikubwa katika serikali yake huku hali na maisha ya watu yakidhoofu na pale walipojaribu kufikisha kilio chao wakidai vyuma vimekaza aliwaonya na kutishia kuwafunga. Lengo likiwa ni kuwafunga midomo ili wasipaze sauti zao.

11. Mwendazake ameacha legacy ya double standard serikalini. Tumeshuhudia na kuona wateule wake mbali mbali kama vile wakuu wa wilaya na mikoa wakifanya mambo kinyume cha sheria na taratibu za nchi lakini wakiachwa katika nafasi zao za utumishi wa umma na mifano yao ipo dhahiri. Vile vile marehemu magufuli ameacha double standard ya upendeleo wa kikanda ambapo tumeshuhudia nyadhifa mbali mbali za juu zikishikiliwa na watu kutoka kanda ya ziwa.

12. Mwendazake atakumbukwa kwa msemo wake maarufu unaosema ''msema kweli ni mpenzi wa Mungu''

Apumzike anako stahili. Amiiin
Mwenda zake alikuwa mnafiki na katili sana huku akijificha kwenye mgongo wa maneno ya mungu

Jamaa alikuwa mlaghai wa maneno sana na alipenda kujiosha kwa watu wasio na elimu kwa kugawa gawa fedha majukwaani na kufokea fokea watendaji wake wa chini na kuwadhalilisha mbele ya hadhara ili awafurahishe hao alio waita wanyonge na ili kutafuta huruma za wajinga wasio tumia akili kuchuja mambo na kwakweli aliwapata wajinga wengi sana kwa ujanja huo.

Jamaa alikuwa mjanja sana kwa kukimbizia ufisadi wake ikulu na kwenye jeshi ili asikaguliwe jamaa alikuwa tapeli wa maneno sana

Alikuwa hayaishi maneno yake yaani maneno na matendo yake tofauti kabisa ukisikiliza maneno yake utasema ni mcha mungu na mnyenyekevu kweli kweli lakini nyuma hayo ni ukatili mkubwa kwakweli bora kaenda na hatuhitaji aje atokee tena mtu wa aina yake nchi hii.
 
Zile siku 14 za maombolezo zilikuwa sawa kabisa...tena hata hivyo ni nyingi..Hawa wanaotunga nyimbo za kumlilia zinaishia kwenye dari
 
Sahizi watu hata Tv hatuwashi maana ukiwasha tu ni nyimbo za magufuli magufuli aaaagh! Utadhani huyo mtu alikuwa mtakatifu maana wamemkuzaa

kilichopo kumbe kuna watu wako nyuma ya manyimbo haya wana fanya hivyo kumtisha mama ili ionekane jamaa alikuwa anapendwa sana hivyo mama hawezi kuvaa viatu vyake na nasikia kuna baadhi wamefadhiliwa kufanya hivyo na wanaambiwa hadi maneno ya kuyaweka kwenye hizo nyimbo ndio maana asilimia kubwa ya nyimbo hizo ukisikiliza maneno ni yale yale yana shabihiana. UJINGA HUU!
 
Back
Top Bottom