Kenya 2022 Mambo ya kushangaza kutoka uchaguzi wa Kenya

Kenya 2022 General Election
1. Hakuna mgombea aliyezuiliwa kuchukua fomu za uchaguzi kama katimiza vigezo.

2. Hakuna mgombea aliyekosea kujaza fomu.

3. Hakuna Afisa uchaguzi aliejifungia ndani au kukimbia na kutelekeza ofisi ili kuwazuia wapinzani kurudisha fomu kwa wakati.

4. Hakuna polisi au Usalama wa Taifa waliongilia zoezi la uchaguzi kwa namna yoyote ile.

5.Kampeni zilifanywa kwa amani, uhuru na utulivu mkubwa.

6. Vyombo vya habari vimekuwa huru kuripoti habari na kuendesha mijadala ya wazi kwa wagombea bila upendeleo wala kumuonea mtu.

7. Wananchi wamepiga kura za wazi bila dalili za kununuliwa au kutishwa.

8. Kura zinahesabiwa live bila kificho.

9. Hakuna gari ya polisi iliyokamatwa ikikimbia na maboksi ya kura.

10. Serikali haijazima wala kuuchezea mtandao wa Internet.

11. Licha ya Rais kumuunga mkono mgombea mmojawapo lakini hajajihusisha wala kuingilia uchaguzi ili kumpendelea.

12.Tume ya uchaguzi kila mara inazungumza na waandishi wa habari na kuwaruhusu kuuliza maswali.

13.Matokeo yote yakitangazwa muda huohuo yanawekwa kwenye tovuti ya tume which means anyone anywhere can access it.

Kuna nchi fulani mwaka wa 3 toka ifanye uchaguzi lakini tovuti ya tume iko nyeupeeeee!

14. Hatujasikia matukio ya Kura kuharibika kama ile nchi ya Cuba ambapo eneo lenye nguvu kubwa ya upinzani swala la kura kuharibika huwa ni kawaida.

15. Hakuna mtu aliyepita bila kupingwa. Kila govana au mbunge kapitia kwenye tanuru la moto.

16. Hadi uchaguzi unaisha hakuna kiongozi au vijana wa upinzani waliopotezwa na watu wasiojulika au kupewa kesi ya uhaini, madawa ya kulevya au uhujumu uchumi.

Big up Kenyans!

[emoji122][emoji122][emoji122]

Nawasilisha.
Huu uchaguzi wa Kenya hakika ni darasa tosha, nchi zingie inakuwa ni vurugu tupu!
Hadi hivi sasa mahabusu zingekuwa zimejaa wapinzani!
 
Zitto yupo sahihi sana kupigania Tume huru kabla ya Katiba mpya.

Tanzania tunahitaji tume huru kwanza ili waingie watu wanaostahili ambao hao sasa ndio tutawadai Katiba mpya..
Yaani kwa akili yako ni sawasawa na kupigania mtoto wakati mimba hukuhusika nayo !! what comes first ?
Tume huru ni zao la Katiba, sasa kama katiba ina mapungufu unategemeaje tume huru ya uchaguzi ikawa genuine?
 
1. Wanahabari wanaonekana kujua wanachofanya kuanzia marepoter hadi wale wa studio na wachambuzi wao hawana mihemko wala ushabiki maandazi.

2.Wasanii wamekaa wametulia wakisikilizia matokeo sio kama wa huku kwetu huwa wanapapatika kama kuku waliokatwa vichwa.

3. Tume inajitahidi kutoa updates na kufafanua mikanganyiko kwa kadri iwezavyo.

4. Wagombea binafsi nimeona wengine wameshika nafasi ya pili kwenye majimbo yao, hii ni hatua kubwa sana kwa mgombea binafsi.

Kwa kweli majirani wameset bars too high sisi kufikia hata kwa 30%, na wanasema hawatarudi nyuma kwa chaguzi zijazo kwa maana watazidi kuboresha, kikiharibika kitu sasa tujue malengo yalikua mazuri. Mapungufu hayakosekani, tuwapongeze majirani na kuwatakia wamalize salama.
 
Huu uchaguzi wa Kenya hakika ni darasa tosha, nchi zingie inakuwa ni vurugu tupu!
Hadi hivi sasa mahabusu zingekuwa zimejaa wapinzani!
Yaani kwa uchaguzi wa Kenya ulivyofanyika sisi wa TZ tunaongekana ni ngombe kabisa, yaani hata robo yake hatujawafikia.

Yaani matokeo ya wadau wa mitandani yame tally na matokeo ya tume yenyewe - sasa vita itatoka wapi? Sisi bado tunakimbizana na mapolice na mapolice nao wanaiba mabox ya kura mchana mchana.... inasikitisha.
 
Mengi uliyoandika yametokea makura feki yapo mengi tu na watu wengi tu wamekufa
 
1. Hakuna mgombea aliyezuiliwa kuchukua fomu za uchaguzi kama katimiza vigezo.

2. Hakuna mgombea aliyekosea kujaza fomu.

3. Hakuna Afisa uchaguzi aliejifungia ndani au kukimbia na kutelekeza ofisi ili kuwazuia wapinzani kurudisha fomu kwa wakati.

4. Hakuna polisi au Usalama wa Taifa waliongilia zoezi la uchaguzi kwa namna yoyote ile.

5.Kampeni zilifanywa kwa amani, uhuru na utulivu mkubwa.

6. Vyombo vya habari vimekuwa huru kuripoti habari na kuendesha mijadala ya wazi kwa wagombea bila upendeleo wala kumuonea mtu.

7. Wananchi wamepiga kura za wazi bila dalili za kununuliwa au kutishwa.

8. Kura zinahesabiwa live bila kificho.

9. Hakuna gari ya polisi iliyokamatwa ikikimbia na maboksi ya kura.

10. Serikali haijazima wala kuuchezea mtandao wa Internet.

11. Licha ya Rais kumuunga mkono mgombea mmojawapo lakini hajajihusisha wala kuingilia uchaguzi ili kumpendelea.

12.Tume ya uchaguzi kila mara inazungumza na waandishi wa habari na kuwaruhusu kuuliza maswali.

13.Matokeo yote yakitangazwa muda huohuo yanawekwa kwenye tovuti ya tume which means anyone anywhere can access it.

Kuna nchi fulani mwaka wa 3 toka ifanye uchaguzi lakini tovuti ya tume iko nyeupeeeee!

14. Hatujasikia matukio ya Kura kuharibika kama ile nchi ya Cuba ambapo eneo lenye nguvu kubwa ya upinzani swala la kura kuharibika huwa ni kawaida.

15. Hakuna mtu aliyepita bila kupingwa. Kila govana au mbunge kapitia kwenye tanuru la moto.

16. Hadi uchaguzi unaisha hakuna kiongozi au vijana wa upinzani waliopotezwa na watu wasiojulika au kupewa kesi ya uhaini, madawa ya kulevya au uhujumu uchumi.

Big up Kenyans!

[emoji122][emoji122][emoji122]

Nawasilisha.
Safi sana Kenya, Nchi za magharibi utaona yafuatayo:
KAA MITA 200 KUTOKA KWENYE KITUO..
UKISHAPIGA KURA KAA NYUMBANI..
Magari ya washawasha kibao barabarani..
Mawakala kamata kamata..
Upinzani na utawala sio uadui, ni njia mbadala ya kuongozana.
 
3. Hakuna Afisa uchaguzi aliejifungia ndani au kukimbia na kutelekeza ofisi ili kuwazuia wapinzani kurudisha fomu kwa wakati.
Wala kuzama mtoni na fomu za wengine ili wino ufutike
Nchi hii!!! Ila basi tu!!!
Ghadhabu ya Mungu kwetu siku ya mwisho tutajuta kuzaliwa
 
KAA MITA 200 KUTOKA KWENYE KITUO..
UKISHAPIGA KURA KAA NYUMBANI..
Magari ya washawasha kibao barabarani..
Mawakala kamata kamata..
Mkwere ndiye alileta huu ujinga, na asivyo na aibu alikuja na hoja ya kuiga uchaguzi wa West Africa kuwa tuwe na transparency kwenye uchaguzi wakati yeye ndiye chanzo cha kuvuruga uchaguzi nchini
 
Hii ndio Tanzania taifa lenye watu watiifu wenye upendo na wakarimu...karibu TanZania
 
Na waambie na wawe na taarifa kuwa sisi ndio tunaendesha ushagusi ya KEN maana tumemleta mzee wa bao la mkono kutoka mzoga yupo hapo Nai...

Wajiandae
 
Kabla hujafa hujaumbika
Yale machafuko ya 2007 ndio yamechochea haya yote. Wakenya walishajifunza tayari hawataki kurudi kaanani
 
Tanzania inabidi tuamke, mabadiliko hayaji kilelemama tu. Inabidi tufanye jambo, ata wao kufika hapo walichapana sana.
 
Mengi uliyoandika yametokea makura feki yapo mengi tu na watu wengi tu wamekufa
Hakuna chaguzi duniani ambayo ni perfect 100%. Wenzetu wamejitahidi kupunguza hayo mapungufu kwa kiasi kikubwa. Hivi kwa mfano kwenye nchi ya CUBA polisi hubambikia mpinzani kesi za uhaini na uhujumu uchumi ili mradi tu asipige kura au kuchagiliwa ni jambo la makusudi au bahati mbaya?
 
Huyu amesema hakuna hiki hakuna kile, angesema kwamba vipo Ila kwa kiasi kidogo. Aache uongo na ujinga
 
Back
Top Bottom