Mwanamayu
JF-Expert Member
- May 7, 2010
- 11,662
- 6,888
Mkuu nadhani uliileta hii kama utani lakini nataka kuiunga mkono ifuatavyo.
(Miaka ya late 80s na early 90s kulikuwa na kundi kama hili - likiitwa Tanzanet, na nafikiri ndio chanzo cha hii JF. Katika kundi hilo nilitoa mada kama hii kuhusu ukichaa - katika mjadala wa death penalty. Wale tuliokuwa nao enzi zile kama wakipitia hapa wanaweza kuongeza. Lakini msitoe identity yangu)
Ukichaa ni scale.
Sisi sote tuna ukichaa wa aina fulani.
Tunaojiita sisi ni wa kawaida ni kwa kuwa ukichaa wetu ni wa kawaida au wa wastani. Wale ambao ukichaa wao ni chini ya wastani basi tunawaita "wapole, hawana ghadhabu, wala hawajikuzi, nk." Wale ambao ukichaa wao ni zaidi ya wastani tunasema wale "machachari, utamjua tu akiingia hapa, wamezidi ngebe, nk." Wale wenye ukichaa ulikubuhu basi saa nyingine inabidi wafungwe kamba au kupewa madawa watulie.
Tunachoita ukichaa ni chemical imbalance kwenye ubongo. Hawa watu hawana tofauti na sisi ("normal" people). Wakipatiwa matibabu muafaka wana hisia zote tulizokuwa nazo sisi "wazima".
Tatizo moja ni kuwa society is very cruel. Watu wakishakujua au kuelezwa kuwa wewe ni mkichaa basi huponi tena!
Kwa sababu, siku ukifurahi na kucheka sana watu wataangaliana na kuulizana "vipi anarudiwa nini?" Ukiwa mkimya siku hiyo watu wataulizana tena, "vipi amekunya dawa zake?"
Jamii ikishakuita wewe ni mkichaa kwa kweli huponi tena. Salama yako ni kuhama mji au nchi.
Disclaimer: Mimi sio medical doctor. Wenye taaluma zao wanaweza kuja hapa na kunichana chana vipande. Ninachokielezea hapa ni experience yangu katika maisha.
Kama ukichaa ni 'scale', hiyo scale ikoje? Kama ni kama ile ya number line haswa kuanzia zero kwenda juu basi kuna wengine sio vichaa kabisa yaani wale ambao wataangukia kwenye zero kwenye hiyo scale.