Mambo ya kuzingatia kwa wanawake waliopo kwenye ndoa kwa kizazi hiki

Mambo ya kuzingatia kwa wanawake waliopo kwenye ndoa kwa kizazi hiki

mhogoz

JF-Expert Member
Joined
Oct 16, 2021
Posts
739
Reaction score
1,195
1. Usikope bila mumeo kujua.

2. Kaa mbali na ma ex wako wa zamani ambao ulikuwa nao kabla ya ndoa. Futa mawasiliano yao ukiwezekana.

3. Rafiki au mgeni yeyote wa kiume asije nyumbani kwenu na ukaribishe ndani wakati mumeo hayupo.Hata kama ni rafiki wa mumeo.

4. Usiende kwenye nyumba ya mwanamume yeyote bachelor hata kama ni rafiki, mchungaji,co worker, hata kama haonyeshi dalili zozote za kukutaka kimapenzi.

5. Kataa offer za vyakula ama outing unazopewa na wanaume wengine,iwe ni rafiki, family friend, classmate kama mazingira hayo yatawafanya muwe peke yenu.

6. Hakuna Siri yeyote chini ya jua, kama unachepuka Kuna siku Siri hiyo itakuwa wazi.

7. Kama unaishi mbali na mume wako kwa sababu za kazi,hakikisha kwa namna yeyote mkae pamoja na mume wako.

8. Epuka kupokea ZAWADI kwa mwanamume ambaye si ndugu yako.

9. Usimlinganishe mumeo na mwanamume mwingine.

10. Njaa ya siku moja isikufanye uuze utu wako.

11. Kwenye ndoa Kuna kupata na kukosa, usimdharau mumeo siku akipungukiwa.

12. Mstahi mume wako hata kama unamzidi mshahara a.u kipato

13. Usikubali kutoka rushwa ya ngono kwa sababu yeyote ya kupanda cheo au kupata upendeleo kwa bosi au kiongozi.

14. Ishi kulingana na kipato chenu kwa muda huo.

15. Usiwe na tabia ya kurudi nyumbani usiku baada ya mumeo.

16. Kama huna sababu yoyote ya ugonjwa usimnyime mumeo tendo la ndoa.

17. Usiongee na mume wako kwa sauti ya juu.

18. Vaa mavazi yanayositiri mwili wako, uzuri na maumbile yako yaonekane kwa mume wako peke yake, kujipamba kuwe ni kwa kiasi, usitumie muda mwingi saluni, vinginevyo tumia muda huo kwa mambo ya uzalishaji.

19. Usieleze ubaya au uzuri wa mume wako kwa watu wengine, mambo ya ndani yabakie ni Siri.

19. Elewa kuwa Mara zote mwenye maamuzi ya mwisho kwenye Kila jambo ni mumeo.

20. Chagua marafiki wa kuambatana nao,usiambatane na wanawake walioachika au Malaya kuwa marafiki.

21. Housegir akianza kumdharau mume wako kwa jambo lolote umfukuze.

22. Usimwachie Binti wa kazi majukumu yote nyumbani,jitengee muda wa kufanya mambo yako.

23. Usiajiri Binti mdogo sana Kuwa mdada wa kazi.

24. Elewe kuwa ukichepuka ndio umevunja ndoa yako ,hutawweza kumheshimu mume wako Tena.

25. Usitumke muda mwingi kwenye kuangalia tamthilia ama kuchati wakati mumeo ameshaenda kulala tayari,jitahd uwe unalala mapema.

26. Dhibiti matumizi ya simu hata kama ni za ofisini pindi unapokuwa upo na mumeo.

27. Siku zote ni ngumu mwanamume kumsameme mwanamke anahecheat kwa sababu yoyote,hata kama ingekuwa mwanamke anafanya hivyo ili kumtoa mume wake jela

28. Hakuna ndoa isiyokuwa na changamoto .

29. Ni rahisi sana mwanamume kumucheat.ila haimaanishi kuwa hakupendi kwa dhati.

30. Ukitambua makosa yako omba msamaha.

31. Hata kama u nahisi mumeo anakucheti, mweleze namna unavyomwamini na unavyompenda.

32. Fanya matumizi kwa busara, huku ukiiweka na akiba kwenye kibubu.

33. Usionheshe dharau yeyote kwa ndugu wa mume wako hata kama ni watu wasioeleweka,jaribu kuwaheshimu hivyo hivyo.

34. Kama unatatizo linalotokana na ndoa yenu usikimbilie kuwaeleza wa nyumbani kwenu.mtafute ndugu yake mmja mwenye busara mweleze.

35. Kama mnamatatizo yoyote au unajambo la kumwambia mumeo usiseme mbele ya watoto au mtu yeyote.

36. Kama mumeo hajakufukuzza usichukue maamuzi ya kuondoka.

37. Mara nyingi wanaume Hawaoi kwa kuangalia uzuri wa nje,kwa hyo usijione mzuri ndiyo maana umeolewa.

38. Tii jambo lolote ambalo mumeo amekukataza kulifanya.

39. Usinywe pombe,haifai kwa mama mwenye familia kuwa mlevi.

40. Tafuta fedha hata kama ni kidogo kwa njia halali .

41. Usimfananishe maisha yenu na maisha ya familia nyingine yoyote.

42. Mama ananafasi kubwa kwenye majukumu ya kulea watoto wake.

43. Epuka kukaa kwenye vijiweni na kufanya umbea

44. Vaa kwa stara hata kama unaenda mwenye sherehe.

45. Mche Mungu wako kwa unyenyekevu siku zote.

46. Jiheshimu siku zote epuka,mizaha na utani,ishi na majirani vizuri.

47. Kama mumeo ameanza kuchepuka, Hilo ni tatizo lako wewe mwenyewe, unatakiwa ukae nae vizuri na kwa busara,usiruhusu mumeo kwenda kwa mwanamke mwingine.

48. Usiende kwa mganga ili ukubalike na mumeo.

49. Uwe msafi, kimwili ,kiroho.Safisha mazingira ya kulala yawe safi.

50. Epuka makelele yasiyo ya lazima na gubu, baada ya mtu kutoka kazini ametoka kufokewa na bosi na wewe unakuja na kelele zako nyingine,ifanye nyumba yako iwe sehemu inayotamaniwa na mume wako.
 
Kwakizazi hiki tulicho nacho nawanao kuja mwenye kufuta ushauli wa namna hii hayupo,hatakuepo nawala uwezekano wakuwepo haupo.dunia ishavaa bukta haijari vumbi wala baridi kali.
☺☺☺
 
Back
Top Bottom