Robert Heriel Mtibeli
Platinum Member
- Mar 24, 2018
- 40,153
- 93,069
MAMBO YA KUZINGATIA UNAPOKUWA NA WATU WAKUBWA KAMA VIONGOZI WA NCHI AU MATAJIRI.
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli
Vijana wengi wamekuwa wakitamani na kuomba Kila Siku ndoto yao ya kukutana na watu wakubwa kama Rais, mawaziri, wafanyabiashara, wanamuziki mashuhuri, waandishu mashuhuri wakiwa na sababu mbalimbali.
Lakini wengi waliowahi kukutana na watu hao wakubwa walijikuta wakiharibu futsal Hiyo baada ya kukosea baadhi ya mambo.
Mtibeli kama kawaida Yangu, nitaleta mada hii ili tujifunze wote kwa manufaa ya watu wote. Wapo walioniomba niandike mada hii na wapo waliotamani kuona mada hii. Wote tutafaidika
Bila kupoteza muda, ikitokea ukakutana na mtu mkubwa lazima uelewe kuwa watu unaowaona Wakubwa wengi wao ukikutana nao watakushangaza. Kwani watakuwa wakawaida Sana pengine ukasema jamaa hana mambo mengi, jamaa simple, yaani hakompliketishi.
Zingatia haya kijana/binti;
1. Epuka Ujuaji.
Usikimbilie kuonyesha unajua kila kitu. Ubishi ubishi au maneno mengi epuka kadiri iwezekanavyo.
Watu wakubwa hukutana na watu wengi wanaotaka kuwavutia kila siku. Ukiongea kwa utulivu na ukasikiliza zaidi, unaonekana mwenye akili kuliko kuwa MTU anayekatiza kila sentensi. Mara nyingi heshima huanza kwenye uwezo wa mtu kujizuia, si kujionyesha. Vijana wengi hutafuta kujionyesha hasa Kwa kujieleza au kwa muonekano
2. . Muonekano na haiba yako.
Muonekano wako utoe ujumbe kabla hujaongea.
Sio lazima uwe na suti ya milioni, lazima uwe msafi, mpangilio wako uwe na nidhamu, na harufu yako iwe nzuri sio Kali yenye kuondoa utulivu na kuvuta attention. Watu wenye nafasi kubwa huangalia detail ndogo sana kuliko vijana wengi wanavyodhani. Dakika ya kwanza inaweza kuamua namna watakavyokuchukulia kwa miaka.
3. Kuombaomba na kujilizaliza.
Usiwe mtu wa kuombaomba unapokutana nao
Vijana wengi wakipata nafasi ya kukutana na watu wakubwa wanaanza moja kwa moja kuomba pesa, connection au msaada.
Hilo huwafanya waonekane mzigo badala ya mtu mwenye thamani. Wakati mwingine acha mtu akumbuke tabia na akili yako kwanza kabla hajajua shida zako.
Kuombaomba, kulialia, kulaumu laumu watu, kulaumu laumu serikali, epuka hayo mambo. Epuka kujieleza sijui umetokea familia maskini. Haisaidii kitu.
Viongozi na matajiri na watu wakubwa hukimbia ugumu na mizigo kwenye maisha yao.
4. Jifunze ku-control hisia zako
Ukikutana na mtu mkubwa usitetemeke kama umeona miujiza, wala usijifanye “too familiar.” Utulivu huonyesha confidence na maturity. Hata ukiwa ndani ya moyo una excitement kubwa, nje baki mwenye balance(kujidhibiti)
Maneno machache yenye uzito yana nguvu kuliko maongezi mengi
Watu wenye shughuli nyingi huchoka haraka na maongezi yasiyo na direction. Ukiongea, sema kitu chenye maana, chenye fikra, au chenye kumbukumbu. Kuna vijana wanaondoka kwenye kikao watu hawakumbuki hata walichosema, ila kuna wengine wanakumbukwa kwa sentensi moja tu.
5. Usimdharau mtu aliye pembeni ya mkubwa
Mara nyingi dereva, secretary, mlinzi au msaidizi wa karibu ndiye anayejua nani ana tabia gani. Vijana wengi wanataka kumheshimu boss tu, wakiamini wengine hawana maana. Kumbe wakati mwingine mlango wa kesho unashikiliwa na yule uliempita bila salamu leo.
Nikuambie tuu watu wakubwa huwaamini madereva, watumishi wao uliowakuta tofauti na wewe mgeni.
6. Ondoka ukiwa umeacha picha nzuri
Sio kila meeting unatakiwa uombe connection, au kuelezea matatizo yako na kupewa ahadi . Wakati mwingine ushindi mkubwa ni mtu kusema, yule kijana ana akili na adabu. Dunia ya watu wakubwa hukumbuka sana energy ya mtu kuliko maneno yake yote.
Kufikia hapo sina la ziada
TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam