5..Well spoken, usimdharau aliye karibu na mtu mkubwa....Hili mimi limewahi kunitokea live....nimewahi kutatuliwa kero yangu iliyonisumbua miaka 7 na katibu wa mbunge ambaye pia alikuwa wakati huo pia waziri wa uchukuzi,
Alinikutanisha na Waziri....tukakaa watatu, mchezo ukaishia hapo.
Wewe unayejipendekeza kwa Samia leo hauna equal status na aliyejuana naye miaka 6 au 7 before kabla hajawa Rais...kipindi hicho wewe ulikuwa bize kujikomba kwa Magufuli..
Asiyeona umuhimu wa Majaliwa Kassim leo, au Makamba, au Mwigulu au Nchimbi au Lissu nk ( hiyo mifano tu) halafu akavizia hadi awe rais ndiyo aanze kummwagia sifa uchwara atakuwa anajisumbua bila kujijua.
Tujifunze kuheshimu watu wote leo
Upo sahihi Kabisa.
Nakumbuka wakati natafuta Uhamisho wa shule Advance, niko Mbeya nahama kuelekea Kilimanjaro
Nimefika Mbeya Mjini, kwa Afisa Elimu Mkoa. Nakuta bonge la msururu.
Kama ujuavyo, mambo ya ofisi za umma hizi. Mstari mrefu, haumaanishi mtoa huduma atatoa harakaharaka. Hivyo huduma zinaenda polepole n wakati mwingine kusimama hata nusu saa.
Mimi nilipofika kuanzia Kule Reception, nikusalimia na kutaniana na wafanyakazi, walinzi, na wahudumu wa usafi. Ungedhani ninafahamiana nao.
Kipindi hicho ninamiaka 17 kidato cha tano. Nikiwa nimevalia Sare ya shule na kunyuka tai. Nadhifu kijana mtanashati.
Sasa nilipofika kwenye foleni. Nikasalimu huku nikiwatania mbona wamenuna wamekunywa chai kweli au ndio wamedamkia pale. Watu wakacheka.
Nikaakaa kama nusu saa, huku nikidodosa huduma zinaendaje pale. Aiseeh! Karibu Kila niliyemuuliza ananiambia yeye anafuatilia uhamisho Siku ya tano yaani karibu wiki nzima. Hivyo kama mimi ndio nimeanza nisitegemee kumaliza Leo.
Nikauliza kumaliza nini, wakati mimi ninachohitaji ni sahihi tuu ya Afisa Elimu mkoa ambayo haimalizi hata dakika. Wakaniambia nitaona.
Nikahisi kuingia upepo.
Mara nasikia watu wanasema ati Afisa elimu Mkoa anatoka sijui Anaenda wapi. So turudi jumatatu. Hiyo ikiwa ijumaa.
Niliposikia nikachoka mwili na roho.
Mara namwona dada mmoja akiwa amebeba chupa ya chai na chapati akiwa anakuja upande wetu akielekea ulipo mlango wa ofisi ya Afisa Elimu Mkoa.
Nikamuwahi upesi, tukakutana pale mlangoni. Kwa vile nilishasalimiana na kutaniana naye wakati nakuja hakuniona stranger tayari kulikuwa na mazoea
Nikamwambia acha nikusaidie walau mara hii tuu. Akawa anagoma. Huku tunafungua mlango. Watu wanashangaa.
Mlango umefunguka Yule dada akaniachia chupa, ndani napokelewa na sura ya mwanamke Mtu mzima hivi aliyevaa miwani. Huyu ndiye Afisa Elimu wa mkoa wa Mbeya
Akawa ananishangaa, tukaingia ndani nikiwa na Yule mdada.
Nikamsalimu Afisa Elimu Mkoa kwa bashasha, huku nikimtania asishangae.
Akawa anacheka tuu. Nikajitambulisha, kisha nikaeleza shida Yangu. Alifurahi kuniona.
Huku Mhudumu yule naye akinisifia kama kijana mwenye ucheshi na adabu.
Nikatoa fomu ndani ya bahasha. Akanisainia. Alafu akanipa elfu 10 akaniambia nikanywe chai.
Jambo langu likamalizika hivyo.