Tiba
JF-Expert Member
- Jul 15, 2008
- 4,605
- 3,176
Unamanisha mbele saizi 15 nyuma saizi 16 Au mapana ya tairi Au irefu wa tairi? Mostly fuel usage, balance ya gari inakuwa imetatizwa,
Yes, hiyo ndio maana yangu. Nimekutana na hali hiyo hivi karibu. Kuna gari lina kama miezi mitatu sasa tangia liingie Tanzania kutoka Japani lakini tairi zake za mbele hazikuwa na ubora niliokuwa na utaka mimi. Zilikuwa zimekwisha hivi. Nilipotaka kubadilisha hizo tairi (nilitaka the same size) nilizunguka mpaka nikachoka na kuna mtu akaniambia hizo itakuwa taabu kuzipata. Nikaweka size tofauti na za nyuma. Kuna ukweli kwani kwa sasa kwa mbele gari linaonekana liko juu zaidi ya nyuma kwa sababu ya ukubwa wa tairi. Madhara ya hali hii ni nini? Ni gari kukosa balance tu?
Tiba